SI KWELI Pen zinazotoa risasi kama Bunduki zinagawiwa na kuuzwa kwenye Shule za Tanzania

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Leo nimeona video ambao imewekewa sauti ya mtu akisema wametumiwa video hiyo kwenye group la shule ya Themihill, video hiyo inaonesha mtu akifungua kitu kinachoonekana kama pen (kalamu) ambacho ndani yake kina risasi na b
Zimeua wangapi?
 
Upo serious kabisa ukaja ku post hiki kitu? Aisee, achana na hizo kelele za huyo mwanamke anayeongea, jitahidi usikilize sauti ya huyo jamaa hapo.
Uchambuzi mwingine tuuweke kando japo hata hauhitaji akili timamu
Huyo mama ameshasema shule gani hapo Bongo unataka ushahidi gani mpaka watoto wafe ndipo utakapo amini? Miafrika Bwana Ndivyo ilivyo. Kazi hiyo nimewapa Polisi Waifanyie kazi Sio kazi yangu na wala sio kazi yako kuthibitisha acha kubisha kitu haukijuwi. Jambo usilolijuwa ni kama usiku wa giza tototoro.
 
Kwa akili zako na wewe unaamini kabisa?
Kila kitu kinawezekana Wazungu wanatulazimisha tuwe mashoga SisiWafrika ili tusipate kuzaliana Wazungu wameleta ugonjwa wa korona wakapeleka nchini china ili kupunguza watu duniani itakuwa kutengeneza silaha ya peni kuwa maliza watoto wetu? Kwa Akili yako wewe unafikiri Wazungu wanawapenda Watu weusi?
 
Hiyo shule ipo Tabora, huyo mama ni mzushi ameamua kuzua taharuki tu.
Huyo aliyeshika pen ukimsikiliza uongeaji wake, wala hayupo Tanzania.
Kwa akili za kawaida hiyo silaha wewe unaona inaweza ikauzwa kwa bei ya Pen hata zisambazwe mashuleni? Ili iweje?
Huo mlio umeisikia?
 
Unaweza kuta Kuna mtoto alichukua ya mzazi au mlezi wake mtu wa kitengo au muhalifu au ya kujilinda mtoto alidhani peni .
Sasa nyie mnakuja kusambaza uzushi.
Kwanza aliye shika ktk video anaonekana siyo mtanzania kwa jinsi anavyo ongea.
Hapa mnaichafua shule tu.
 
😂😂 kwa hiyo pen ya risasi iuzwe 200 ili watoto wauane , halafu kwa faida ya nani sasa ?

Kweli huenda zimetengenezwa lakini sio kwa ajili ya kuuzwa kwa watoto na huenda shule ikafika kwa mazingira ya mtoto kuichukua nyumbani kwa baba bila kujua madhara yake. Kama ambavyo mtoto anaweza kuchukua kisu nyumbani kuja kukatia maembe shuleni ila mzozo ukatokea watoto wakauana.

Ila eti kusambazwa mashuleni hapo msituzuge mnatafuta attention tu kuonekana mpo makini na jamii kumbe ni kwenye kufuatilia vitu visivyo na msingi na kuzua taharuki.
 
Kwa akili zako na wewe unaamini kabisa?
Upo serious kabisa ukaja ku post hiki kitu? Aisee, achana na hizo kelele za huyo mwanamke anayeongea, jitahidi usikilize sauti ya huyo jamaa hapo.
Uchambuzi mwingine tuuweke kando japo hata hauhitaji akili timamu
Swali: Je, Silaha au vifaa vya namna hii vipo au havipo ktk uhalisia?Jibu ni kuwa; Vipo.
Swali la Pili: Je, kwa hapa Tanzania vifaa vya namna hii tayari vimeshaingia au bado?Jibu ni kuwa: Haijulikani bayana kama tayari vimeshaingia au bado.

Lakini yawezekana ni kweli kwamba vifaa vya namna hii tayari vimeshaingia hapa nchini Tanzania. Aidha, hata kama vifaa hivyo tayari vimeshaingia hapa nchini, haviwezi kuuzwa kiholela ktk maduka ya Wafanyabiashara wa kawaida kwa sababu kwa 'nature' ya kifaa chenyewe jinsi kilivyo ni LAZIMA kitakuwa 'classified' kama 'Military Equipment', hivyo hakiwezi kutumika kiholela na watu ambao hawako ktk Mifumo ya kijeshi. This device is designed for Military purposes only, and most probably for the Secret Intelligence Operations, such as "Clandestine Covert Operations' ili kutekeleza 'missions' zao mbalimbali.
 
Watanzania hawana akili za utambuzi. Unadhani hizo pen zinauzwa tsh 5000?watu hadi condoms mnapewa msaada mnadanganywa na watoto vitu vya kipumbavu mnabebelea. Hizo siyo peremende nyie vilaza. Hakuna anayeweza gawa kwa watoto hizo silaha si rahisi kama mnavyodhani. Tumieni akili kidogo.
 
Wabongo wanapenda haya mastory , eti mchele wa plastic , mara kuna mayai yanatengenezwa huko china ni rahisi sana kuzua taharuki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…