MKAKA WA CHUO 2
Member
- Aug 15, 2022
- 5
- 0
Asili ya mwanadamu ameumbwa na MUNGU na akajaaliwa kuwa na neema tofautitofauti katika mwili wake. Neema hizi amepewa mwanadamu ili apate urahisi katika kuendesha maisha yake hapa ulimwenguni.
Katika neema kubwa ambazo sisi wanadamu tumebarikiwa naweza kusema ni neema tatu ambazo ni kuona, kusikia, kuongea na kufikiria (akili). Akili ni nyenzo kuu ambayo hufanya kazi kwa ufanisi na Kasi zaidi baada ya kusikia au kuona matukio mbalimbali au Hali mbalimbali, ni jambo la wazi ya kwamba akili ndio husaidia katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika maisha yetu ya Kila siku.
Kuona ni neema ya muhimu pia ambayo kwa mwanadamu husaidia kupata muongozo katika nyakati mbalimbali, pia akili itamsaidia kufanya maamuzi kutokana na mazingira hayo ambayo mwanadamu anayoyaona au kukutana nayo kulingana na wakati husika.
Neema ya kuona ni neema ya msingi Sana kwasababu ndio msingi mkubwa wa kufanya maamuzi kwasababu mtu akiwa anasikia lakini haoni anaweza akasikia hatari lakini asijue akimbilie upande gani.
Kwa MTU anayeona lakini hasikii yaani kiziwi anaweza kuona hiyo hatari na akaona upande wa kukimbilia, lakini siwezi kusema kwamba kuona ni Bora kuliko kusikia ,jambo hili linategemea na mtazamo wa MTU mmoja mmoja. Tunapokuja kuzungumzia neema ya kuongea.
Hiki ni kipengele kingine Cha msingi katika maisha yetu ya Kila siku, Ni kweli kwamba kuongea ni miongoni mwa misingi ya harakati nyingi katika maisha yetu ya Kila siku, lakini katika kuongea kuna vitu mbalimbali vya kuzingatia ukiwa Kama kijana au mtanzania unapozungumza, vitu hivi ndivyo ambavyo UNAPO weza kuvifuata kikamilifu ndio unaoneka ni mzungumzaji mwenye hekima na busara lakini pia utabakia salama kutokana na midomo ya watu wengine kunako matusi, kejeli, dharau na mengineyo.
Miongoni mwa vitu vya msingi katika kuongea kwanza sikiliza watu ili ujuwe ni nini shida Yao hasa, au ni Nini wanahitaji kufahumu zaidi, au ni Nini matumaini Yao kutoka kwako na vitu vingine Kama hivyo.
Unapowasikiliza watu kabla ya kuongea ndio utajua na kujifunza Nini cha kuongea nao kulingana na Yale uliyoyasikia kutoka kwao, mfano Waziri wakilimo anapotembelea wilaya yeyote kabla haja Anza kuongea anakuwa na taarifa za kutosha kuhusu wilaya hiyo, taarifa hizo ndio zinazo muongoza wakati wakuzumguza na viongozi wa ngazi za chini na wananchi kwa ujumla.
Jambo la pili katika kuongea ni kuepuka kuongea maneno Fulani ili kuwaridhisha watu Fulani. Katika maongezi yako Kama kijana hakikisha unaongea Mambo kwa usahihi wake, na siyo ili mradi tu aridhike MTU Fulani.
Mara nyingi katika harakati tofautitofauti za kutafuta maisha vijana tunajikuta tunaongea maneno ili kuwaridhisha mabosi wetu, lakini lazima ukumbuke kumdanganya huyo bosi wako siku moja kunaweza kukaweka nafasi yenye hatari kuliko kusema ukweli ambao ungekuweka mahali salama, kwa kawaida unapofika wakati wakuongea lazima ujue kwamba katika mazingira hayo watu wanahifadhi maneno yako kwa njia tofautitofauti inaweza kuwa vinasa sauti, au katika makaratasi kwa njia ya maandishi ambayo yatakuja kutumiwa baadaye pindi utakapo kwenda kinyume na Yale uliyokuwa ukiyasema.
Suala la jingine kama kijana katika harakati za Kila siku za kutafuta maisha ni vyema ukawa ni mpenzi wa kusikiliza zaidi kuliko kuongea, kwasababu unaposilikiliza unajifunza jambo jipya lakini unapoongea unarudia kile ambacho unakijua isipokuwa wakati unauliza swali.
Lakini hii ni changamoto kubwa Sana kwa WATANZANIA tulio wengi kwasababu wengi wetu tunapenda kuongea zaidi kuliko kusikiliza, wakati mwingine MTU anaweza akaingilia mada ambayo hata mwanzo wake haujui mradi tu amesikia neno moja ambalo analijua kwa uchache basi na yeye anaunga mazungumzo mwisho wa siku yeye ndio anakuwa mzungumzaji mkuu wakati alitakiwa yeye awe msikilizaji ili aweze kujifunza vitu vingi zaidi kwasababu unaposikiliza ndio utajua watu wanapenda Nini, wanaelewa Nini na utapata mawazo mbalimbali kutokana na kusikiliza kwako.
Kiuhalisia katika mazingira ya kawaida kila mwanadamu anapenda kusikilizwa, lakini Sasa tatizo lina anzia kwa muongeaji anaongea kuhusu mada gani, katika mazingira gani na anazungumza na wakina nani , kwa malengo gani na vitu vingine Kama hivyo.
Wengi katika wazumgumzaji Huwa hawazingatii misingi hii ya mazungumzo kwa mfano kijana anaweza kuwa anaongea na bosi wake lakini anatumia maneno makali na machafu, au vijana wengi wanapoongea na wazazi wao, wengi wao wanatumia lugha za mitaani,utasikia MTU anamuita baba yake "dingi" au anamuita mama yake "mama juma" kwasababu tu yeye anaitwa juma kwahiyo kumuita mama anaweza kuona haijakaa sawaa anamuita mama yake majina Kama hayo, hatimaye anaenda kumuita bosi wake "chibonge" hii inatokana na kutokuzingatia nafasi za watu ambao tunazungimza nao.
Lengo la mazungumzo au kuongea ni jambo lingine la kuzingatia Kama kijana wakitanzania. Ifikie wakati vijana tusiwe tunaongea saana, bila ya kufikisha taarifa ilivyokusudiwa katika mazungumzo hayo, kwasababu maneno mazuri ni Yale machache lakini yawe yenye kueleweka. Na katika Lengo la mazungumzo hakikisha unafikia Lengo la kuongea kwako Kama Lengo ni kuomba msaada hakikisha unaomba msaada na unaeleweka.
Kama Lengo ni kuwapongeza au kuwashukuru watu basi hakikisha unafikia Lengo Hilo, vilevile Kama Lengo ni kuwafundisha watu basi hakikisha unafundisha kwa ufupi na urahisi lakini pia hakikisha unaeleweka, na Kama wewe ni mchekeshaji basi hakikisha watu wanacheka kutokana na maneno hayo uliyo ya zungumza na isiwe kinyume chake.
Mzungumzaji anapozingatia mazingira ya mazungumzo, Lengo la kuongea au mazungumzo na mahusiano baina yake yeye mzungumzaji na wasikilizaji mara nyingi mzungumzaji huyu ataonekana ni MTU mwenye hekima na busara katika maisha yake ya Kila siku, lakini kwasababu ya kuto kuzingatia vipengele hivyo vya msingi baadhi ya vijana wa kitanzania tunakumbwa na kasumba ya kukosa hekima katika nyakati na mazingira mabalimbali.
Ili kuepuka kasumba hii mbaya vijana inatubidi tuzingatie vipengele hivyo vya msingi wakati wa mazungumzo lakini pia ni Bora tukapenda kusikiliza zaidi kuliko kuongea kwa SABABU kusikiliza kutatusaidia kujifunza Mambo mengi na mapya zaidi kuliko kuongea kwa SABABU kuongea ni kurudia Mambo ambayo sisi tunayafahamu.
NDUGU ZANGU WA TANZANIA, kusikiliza kutatusaidia kuepuka ugomvi na migogori, kunasaidia kuelewa Mambo kwa urahisi, kusikiliza kunaongeza uhusiano ya, kifamilia, kindoa,kidini na kadhali. Hapo chini ni picha kutoka katika vitabu vya dini ambapo mungu anahusia kusikiliza kutokana na umuhimu wake, vilevile picha nyingine ni kutoka katika mtandao wa Instagram, mwenye akaunti hiyo anahimiza kusikiliza kwa makini kabla huja amua kujibu.
By: MKAKA WA CHUO.

Upvote
0