SoC02 Pendekezo: Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu iwaongezee kiwango cha mkopo wanufaika

SoC02 Pendekezo: Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu iwaongezee kiwango cha mkopo wanufaika

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 2, 2022
Posts
60
Reaction score
75
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ni taasisi iliyoanzishwa chini ya Sheria Na.9 ya 2004 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2007, 2014 na 2016) kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi wa Tanzania wenye uhitaji na stahiki kupata mikopo na ruzuku kwa ajili ya elimu ya juu. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inajukumu la kuwapangia mikopo wanafunzi wenye uhitaji ambao wanapata nafasi ya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu vilivyoidhinishwa, lakini hawana uwezo wa kiuchumi kulipia gharama za masomo yao.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inamchango mkubwa mno kwa Wasomi wengi Nchini kwani Idadi kubwa ya Wasomi Nchi wamesoma kwa kutegemea mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, na kama kusingekuwa na mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi idadi kubwa ya Watanzania tungeshindwa kumudu gharama za malipo ya Ada pamoja na Michango mingine inayohitajika chuoni hivyo tusingeweza kupata Elimu ya Juu.

Kwa kawaida Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu huwapangia wanufaika mikopo ya Ada (Tution Fees) kwa asilimia ambapo mnufaika atalipiwa Ada na Bodi kulingana na asilimia alizozipata, Mikopo ninayoipendekeza iongezwe kwa wanufaika ni mikopo ya pesa za chakula na malazi (meals and accommodations) ambapo wanufaika wote bila kujali asilimia za mikopo waliyopangiwa hupewa kiasi cha shilingi kiasi cha shilingi laki tano na elfu kumi (Tshs 510,000/=) za Kitanzania kila baada ya mienzi miwili kwa ajili ya chakula na malazi. Vilevile Kuna mikopo ya vitabu na maandishi (Books and Stationery) ambayo hutolewa kwa baadhi ya wanufaika ambapo kila mwaka wa masomo unapoanza ambapo mnufaika aliyepangiwa mikopo hii hupewa kiasi cha pesa za Kitanzania shilingi laki mbili (Tshs 200,000/=). Bila kusahau Kuna wanufaika ambao hupangiwa mikopo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (Fieldwork Practice) pamoja na mikopo ya kufanya utafiti (research). Pamoja na mikopo ya mahitaji maalum ambayo hutolewa kwa baadhi ya wanafunzi.

Mikopo wanayopangiwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kwa miaka ya nyuma ilikuwa inajitosheleza lakini kwa sasa hakiwezi kutosheleza mahitaji ya wanafunzi kama inavyotakiwa kwani maisha ya miaka ya nyuma na maisha ya Sasa ni tofauti. Gharama za maisha ya sasa ni ghali kuliko maisha ya nyuma, ambapo hivi karibuni tumeshuhudia mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali kwa mfano bidhaa za chakula pamoja na bidhaa nyingine ambazo zimepanda bei tofauti na miaka ya nyuma. Vilevile upatikanaji wa baadhi ya huduma mbalimbali kama huduma ya usafiri kwa Sasa zimepanda tofauti na miaka ya nyuma. Hivyo basi kiasi cha pesa wanazopangiwa wanufaika na Bodi ya Mikopo kwa Sasa hakiwezi kukizi mahitaji Yao hiyo ni kwa sababu gharama za maisha zimepanda tofauti na ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.

Kupanda kwa gharama za maisha kumewathiri baadhi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya Elimu ya Juu hiyo ni kutokana na kiwango cha pesa na mikopo wanazopangiwa haziwezi kumudu gharama za maisha ya sasa kama ilivyo kuwa miaka ya nyuma, baadhi ya athari wanazozipata wanufaika ni Wanufaika wamekuwa wakishindwa kuendelea na masomo aidha kwa kuhairisha mwaka wa masomo au kukacha kusoma kabisa kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama za maisha ya ambayo yapo juu Sana, Athari nyingine ni baadhi ya wanufaika hujiingiza katika mikopo yenye masharti magumu ambayo inaweza kuwapelekea kupoteza baadhi ya mali zao pale wanakuwa wameshindwa kurudisha mikopo hiyo na athari ya mwisho ni kushuka kwa uwezo wa ufaulu wa mnufaika wa mikopo hii ni kutokana na msongo wa mawazo kutokana na kiwango cha mikopo ya pesa wanachopewa na Bodi ya Mikopo hakiwezi kukizi gharama za maisha.

Hivyo basi ninapendekeza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu iwaongezee wanufaika kiwango cha mikopo hususani mikopo ya chakula na kujikimu, mikopo ya vitabu na viandikwa, mikopo ya mafunzo kwa vitendo na mikopo ya utafiti pamoja na mikopo ya mahitaji maalum ili waweze kumudu gharama za maisha ya sasa kwani maisha ya Sasa hivi yanagharama kubwa tofauti na maisha ya miaka ya nyuma. Kwa mfano hivi karibuni tumeshuhudia mfumuko wa bei bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za chakula pamoja na bidhaa nyingine. Vilevile huduma mbalimbali zimepanda bei mfano huduma za usafiri ambazo zimepanda bei tofauti na miaka ya nyuma. Iwapo Bodi ya Mikopo itawaongezea wanafunzi wanaonufaika mikopo wataweza kumudu gharama za maisha ya sasa.

Kuna faida mbalimbali watakazopata wanafunzi wanaonufaika kama Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu itawaongozea wanufaika kiwango cha pesa za mikopo kwamfano wanufaika wataondokana na maswala ya kuhairisha chuo au kukata tamaa ya kuendelea na chuo, Wanufaika wataepuka kujiingiza kwenye mikopo mingine yenye masharti makali kwa sababu kiasi cha mikopo watakachopangiwa kitakuwa kinajitosheleza kumudu gharama za maisha ya sasa bila kukopa sehemu nyingine, vilevile kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kwa sababu wanufaika hawatakuwa na msongo wa mawazo kwa kuumiza kichwa ni sehemu gani nyingine ya kupata pesa kwa ajili ya kumudu gharama za maisha.

Mwisho, Hivi karibuni Wafanyakazi wameongezewa asilimia za mishahara na serikali ili waweze kumudu gharama za maisha ya sasa hii ni baada ya mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali pamoja na huduma mbalimbali. Kama wafanyakazi wameweza kuongezewa asilimia za mishahara kwa ajili ya kupanda kwa gharama za maisha ya sasa, Hivyo basi ninapendekeza na wanafunzi wa Elimu za Juu wanaonufaika na mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu wa Elimu ya Juu wasiongezewe kiwango cha mikopo hususani katika mikopo ya pesa ya chakula na kujikimu, Vitabu na viandikwa, mikopo ya mafunzo kwa vitendo, mikopo ya kufanya utafiti pamoja na mikopo ya majitaji maalum. Ili na wao waweze kumudu gharama za maisha ya sasa.
 
Upvote 2
Halafu wakimaliza wanaingia mtaani wanakuwa machinga na bodaboda, mkopo hawarejeshi
 
Back
Top Bottom