Championship
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 5,500
- 10,616
Wanabodi,
Ni dhahiri kwamba ipo changamoto kubwa sana ya wafanyabiashara hawa wadogo pale Kariakoo. Wamekuwa wengi mno na kusababisha adha kubwa sana kwa wenye maduka na wateja waendapo kupata huduma.
Ninapendekeza eneo lote la jangwani painuliwe, pajengwe vizuri na kuwekewa vibanda modern ambapo machinga wa pale kariakoo wapangishwe kwa malipo nafuu ili waweze kuendelea na kujikimu kimaisha.
Lile eneo ni zuri kwasababu lipo katikati ya mji, ni karibu na mahali watakapopata bidhaa (yaani maduka ya Kariakoo) na ni rahisi kwa wateja kuweza kuwafikia.
Ujenzi wa pale jangwani wala hauwezi kuwa complicated ikiwa ile mito mitatu itachimbwa na kujengewa vizuri ili ipitishe maji.
Muhimu tu ile mito ijengwe vizuri kwa plan ya kuwa njia ya usafirishaji kwa miaka ijayo. Ule mto unaweza kuchimbwa kutoka pale selander mpaka mbezi na kuvuta maji ya bahari ili kuwe na boti za abiria na utalii. Hii teknolojia ipo, nimeiona pale Dubai na Thailand.
Nawasilisha.