Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Wasije chapana vibao lakini..... Nani atakuwa mpatanishi? Napendekeza maaskofu na mashehe kupitia taasisi zao wateue. TEC, CCT na wale wapentekoste na waislamu wote wakutane na wagombea watatu wa juu then Lewis Makame awe chairman. Litoke neno hapo..... Nisingependa Kinana au Baregu pale..... Asante
Mwelekeo wa hali ya uchaguzi unasikitisha kidogo. Matukio ya vurugu za hapa na pale unanifanya nitamani kuwa wagombea wa Urais wa kianzia na Kikwete wakutane ili kulipa taifa picha ya umoja katika tofauti. Watoe kauli ya pamoja ya kuwakata wanachama wao na mashabiki kutotumia nguvu na wale wenye vikundi vya ulinzi wawatulize makada wao. Vinginevyo, tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Wafanye mapema
Mzee Mwanakijiji,
Nakushuru kwa pendekezo lako linaloonyesha ukomavu wa siasa zako, uzalendo, mapenzi na huruma kwa nchi yetu na watu wake. Ni jambo muhimu sana kwamba kiongozi aliyeko madarakani sasa, yaani Rais Kikwete aongoze katika tamko hilo. Hata kama, kwa sababu yoyote ile, hatafuata ushauri huu, ingefaa Dk. Willibrod Slaa na Profesa Ibrahim Lipumba wakatoa tamko linalozingatia ushauri huu.
Edwin Mtei. (Mwenyekiti Mstaafu na Muasisi wa CHADEMA)
Ndugu yangu kama huna taarifa basi nikwambie tu kuwa CCM kule Hai mkoani Kilimanjaro wameteka mtu na kupasua vioo vya magari ya CHADEMA. Unataka kusema hawa ni wafuasi wa nani?Kwa mtazamo wa CCM hakuna vurugu yoyote mpaka sasa, ndio maana wanaishia kupiga kelele eti wapinzani wanatoa kauli za kumwaga damu....
Mwelekeo wa hali ya uchaguzi unasikitisha kidogo. Matukio ya vurugu za hapa na pale unanifanya nitamani kuwa wagombea wa Urais wa kianzia na Kikwete wakutane ili kulipa taifa picha ya umoja katika tofauti. Watoe kauli ya pamoja ya kuwakata wanachama wao na mashabiki kutotumia nguvu na wale wenye vikundi vya ulinzi wawatulize makada wao. Vinginevyo, tujiandae kulipa gharama kubwa zaidi. Wafanye mapema
Kikwete hatakubali. Dawa ni maandamano...