Pendekezo kuanzishwa kwa "East Coast US Tanzanians alliance "

Pendekezo kuanzishwa kwa "East Coast US Tanzanians alliance "

environmental

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Posts
1,054
Reaction score
137
Wakuu kwa mtazamo wangu na nimekuja kuweka huu uzi hapa ili tuwe na positive katika kuleta maendeleo ya nchi yetu Tanzania. Na pia tujifunze au tuwe creative kubuni nini kinatakiwa kifanyike kwa nyakati hizi kiuchumi. Miaka mingi sana serikali ya Tanzania ilikuwa na tabia ya kuwawekea vikwazo watanzania kwenda nje ya nchi kutafuta maisha.

Vikwazo kama upatikanaji wa passport na hata kama ukifika nje[abroad]. Kama mtanzania amepata tatizo la kibinadamu kama kukosa sehemu ya kulala au kumsaidia kupata passport mpya utaona watumishi wa balozi husika wanakuja na kusema kuwa umekuja nje kutafuta nini? mnatutia aibu tu huku. Bila kujua huyu mtu ni hazina ya taifa kama akiwezeshwa kidogo na akaweza kuhimili maisha ya pale alikokwenda.

Nije kwenye point yangu. Kutokana na kuwa na watanzania wachache na wamesambaa mbalimbali katika state za Marekani, nimeona tuanzishe jumuia ambayo itakuwa na uwezo wa kuwaokoteza Watanzania ambao wanaishi mbalimbali na kuwaweka pamoja ili tuweze kuleta maendeleo yetu hapa USA na muhimu zaidi kule Nyumbani Tanzania. Hii itakuwa jumuia kubwa zaidi ambayo sijui kama wezentu wameshaanzisha kama hii.Itakuwa wasiliana kwa karibu sana kwa kila mtanzania kwa kutumia vifaa vya kisasa vya mawasiliano,na pia ili kumpata rais wa jumuia itakuwa rais huna sababu ya kuja kupiga kura, system tayari itakuwa inakujua utaweza kupiga kura online[ kwa kutumia simu, computer, ipad na hata ukitaka uje mwenyewe kituoni kupiga kura.Tunataka kuwa wazi kwa kila kitu, website itaelezea kila kitu,na kila saa kutakuwa na habari mpya na hasa kuhusu kazi na mambo mengine ya maisha.

Kati ya vitu muhimu hii jumuia inatakiwa kufanya ni kuweza kuwaleta vijana wengi kuja nje kisheria, au kuwapa information kuhusu scholarships ili waje kusoma na pia kujitafutia riziki na hatimaye kuweza kutuma pesa nyumbani (Remittances) na kuweza kuifanya nchi kuwa imara kwenye account yake ya pesa za kigeni.

Mfano kwa wenzetu wa Mexico utumwaji wa pesa (remittances) kutoka abroad umekuwa NO.2 As source of income after oil exports, ambayo wamexico walio nje waliweza kutuma pesa Mexico 21.2 billion in 2009 ukilinganisha na 25.1 billion 2008(source world bank). Lakini pato hilo lilishuka zaidi kuanzia 2010 -2012, hii ni kutokana na Hali ya uchumi kuwa ngumu duniani na hasa USA, ambako wamexico wapo zaidi ya millioni 11.8.

Kutokana na maelezo ya Rais wa bank kuu ya Mexico Bwana Augustin Carstens alielezea kushuka kwa pato lao limetokana pia na wamexico kukosa kazi na wengine kurudishwa mexico (illegal immigration). Lakini amefurahishwa na kuona uchumi wa USA unaonyesha dalili nzuri katika kukua.

Tuje kwa majirani zetu Kenya, wenzetu wanatuma pesa nyumbani zaidi ya billioni 3. Nchi ya kwanza ambayo wananchi wake utuma pesa zaidi nyumbani kwao ni INDIA.
REMITTANCES VS MAJOR EXPORTS

Philippines[2013] 25 billion"Remittances", 22 billion [electronics]


Vietnam[2013] 11 billion"Remittances" , 12 billion [petroleum]


Pakistan[2013] 14 billion"Remittances", 5 billion[cotton exports]


Lesotho[2012] 500 million"Remittances", 300 million[diamonds and precious stones]



source of data worldbank.

Kwa hiyo kwa mawazo yangu ningeomba serikali ya Tanzania iangalie zaidi interest kama nchi zingine wanavyofanya.Tuwe na system ya kurahisisha vijana kuondoka nchini kwa kasi.Kwani baadae kuna makundi yatakuwa yanarudi ili kuwekeza katika fani mbalimbali,huku wengine wanaondoka ili ku balance pato la pesa za kigeni serikali inapata.vile vile kama watanzania waishio nje wakifikia kwa mfano one million,serikali inaweza kufungua mfuko maalum.Kila mtanzania aliyeko nje atoe 50 dollar kila baada ya miezi 6.Inatosha hizo pesa kusaidia kwenye miundo mbinu na mambo mengine ya maendeleo.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
 
Back
Top Bottom