Pendekezo kwa Tanesco kuhusu kusambaza umeme kwa wahitaji wa eneo husika

Pendekezo kwa Tanesco kuhusu kusambaza umeme kwa wahitaji wa eneo husika

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Kwa vile Tanesco haina fedha za kutosha kusambaza umeme kwa wahitaji wote na kwa muda muafaka napendekeza ifuatavyo:

1. Watu ni wagumu kuchangia kupata huduma ya umeme. Akitokea mtu/watu wakajitolea kuvuta umeme, basi wengine ambao wamegoma kuchangia kuvuta umeme huo, wasiwekewe umeme mpaka watakapo changia kiasi ambacho kitakuwa kimeamuliwa kutokana na gharama walizoingia wale waliovuta umeme.
Nina uhakika hii itawaondoa ugumu watu wasiopenda kuchangia. Hakuna anyeweza kukaa kwenye giza wakati jirani yake anapeta na umeme.

2. Kwa vile kuingiza umeme kama nguzo iko mbali ni gharama, napendekeza mtu apatiwe umeme (kama nguzo iko karibu naye). Bili yake ya LUKU iongezewe kulipia deni la umeme aliowekewa. Nadhani system yenu ya LUKU mnaweza kuiprogramme kuwa lazima afikishe kiasi fulani ndiyo ataweza kununua umeme kupitia mitandao ya simu. Ushirikiano na mitandao ya simu inaweza kufanikisha hili. Na wengi watapenda hii njia ya kupata umeme.

Naomba wengine waongezee alternatives za kuwezesha watu kupata umeme.

(kuna mdau humu amesema utaratibu huu namba 1 hapo juu waliutumia watu wa idara ya maji kuvuta maji, waliokataa kuchangia walinyimwa maji na baada ya kuona mafanikio, wote walilipa na kuunganishwa)
 
Back
Top Bottom