Pendekezo la documentary kutoka kwa AliKiba: Wasanii wa Bongomovie ‘watawezana’?

Pendekezo la documentary kutoka kwa AliKiba: Wasanii wa Bongomovie ‘watawezana’?

akilindefu

Member
Joined
Sep 5, 2020
Posts
69
Reaction score
63
Habari wanajukwaa,

Leo katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndugu John Joseph Pombe Magufuli kulikuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa bongo fleva akiwemo ndgu Ali Swalehe Kiba almaarufu kama Ali Kiba.

Wakati akiendelea na utumbuizaji katika jukwaa ameomba Serikali kutenga bajeti kwa ajili ya bongo movie ili watengeneze documentary ya mwalimu JK Nyerere ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo sasa

Swali langu kwenu wanajukwaa hawa wasanii wetu wataweza kweli?

Naomba kuwasilisha.
 
Habari wanajukwaa,

Leo katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ndugu John Joseph Pombe Magufuli kulikuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa bongo fleva akiwemo ndgu Ali Swalehe Kiba almaarufu kama Ali Kiba...
Bora wasitoe hela maana watatia kichefuchefu pale Steve nyerere atakapoigiza nafasi ya Mwl. Nyerere na kutuharibia lengo.
 
Back
Top Bottom