SoC01 Pendekezo la mabadiliko ya Mtaala wa Elimu

SoC01 Pendekezo la mabadiliko ya Mtaala wa Elimu

Stories of Change - 2021 Competition

David M Mrope

Senior Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
115
Reaction score
74
Swala la elimu ni pana sana ni kweli kabisa. Pia tunaelewa kuwa mfumo huu wa elimu ndio umetufikisha hapa leo hii. Lakini Serikali kila siku inakubali kuwa teknolojia inazidi kukua,lakini bado kwa ukuaji huu wameshindwa kufumua mfumo huu wa elimu na kuuunda upya ili uendane na soko la ajira.

Elimu tuliyonayo tunafundishwa hasara na faida ya vitu mbalimbali,yaani hata mwanafunzi wa chuo kikuu anaendelea kuulizwa kazi ya jani katika mmea. Hii haiingii akilini hata kidogo,basi ni vyema tukaboresha zaidi mfumo wetu.

Haya ni baadhi ya mapendekezo juu ya mtaala wa elimu.

(i) KUPUNGUZA MIAKA YA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI.
Hii miaka ni kweli ilikuwa bora zaidi kipindi kile ambacho familia nyingi za kitanzania zilikuwa bado hazijaelimika. Kutokana na hasili ya mazingira yale kweli ilimtaka mwanafunzi asome miaka saba msingi na minne sekondari kwa sababu hakupata mchango wowote nje ya mwalimu.

Lakini kwa kipindi hiki,serikali haioni haja ya kuboresha elimu yetu kwa kupunguza miaka kwa sababu familia nyingi sasa zinamuamko mkubwa wa elimu. Asilimia kubwa ya watoto kwa sasa wanasoma masomo ya ziada ambayo huwasaidia kuelewa haraka tofauti na hapo mwanzo.

Pia serikali haioni kama itapunguza gharama za usomeshaji,na pesa hizo ambazo zitaokolewa basi zitumike kufufua na kuendeleza karakana na vyuo mbalimbali vya ufundi nchini.

(ii) WANAFUNZI WA SAYANSI WAPITIE VYUO VYA KATI.
Serikali ingeweka mfumo ambao baada ya kumaliza kidato cha nne,wanafunzi waliofaulu vizuri masomo ya sayansi wapelekwe vyuo vya kati badala ya kwenda kidato cha tano na sita.

Ungewekwa utaratibu ambao,aliyepata ufaulu mzuri masomo ya sayansi na anandoto ya kusomea afya,uhandisi n.k angetakiwa kwanza kupita vyuo vya kati kama vile veta na kupata ujuzi ngazi ya diploma kisha kwenda moja kwa moja chuo kikuu.

Hii itasaidia sana kutatua changamoto ya ajira. Leo hii mtoto anamaliza chuo kikuu shahada ya uhandisi wa maji lakini hata jinsi ya kujiajiri anashindwa,kutokana na mfumo wa elimu.

(iii) SOMO LA BIASHARA LIENDANE NA MAZINGIRA YA KITANZANIA.
Tunatambua wazi masomo ya biashara yanaendelea kufundishwa katika shule zetu. Lakini masomo haya yamekua ni tatizo kutokana na mtaala wetu ulivyo.

Bado tunafundishwa jinsi ya kutunza pesa,kuweka & kutoa pesa,na kuhesabu pesa. Dunia ya leo hakuna mtu anamwajiri mtu ili atunze pesa,ahesabu pesa na kufanya miamala.

Mfumo huu ungeboreshwa na watoto wafundishwe vyanzo vya mtaji,aina za biashara,changamoto za biashara,na mengine mengi. Nafikiri watoto wangekuwa na ubunifu mkubwa na wangeweza kujiajiri.

(iv) SOMO LA KILIMO LIJIKITE KIBIASHARA ZAIDI.
Haiwezekani mtoto ambaye anaenda kuwa mkulima hajui hata namna ya kuendesha kilimo cha umwagiliaji. Alafu elimu ya umwagiliaji anapewa kijana wa chuo kikuu cha kilimo sokoine ambaye naye anakosa ajira na anaamua kuachana na kilimo na kuuza matunda.

Serikali inapaswa kutilia mkazo na kuachana kila wakati kufundishana ili tufaulu mitihani. Kama bado tutaendelea kuulizana maswali ya aina za magurudumu ya trekta nafikiri itatuchukua muda sana kufanikiwa.

(v) ELIMU YA LISHE BORA NI MUHIMU KWA WANAFUNZI WOTE.
Unajua elimu ina mfumo maalumu,ambao unachangamana duniani kote, mfano masomo ya hisabati,baiolojia,kemia n.k. Lakini nchi husika inayouwezo wakuandaa masomo ya ziada kutokana na uhitaji wa nchi hiyo.

Swala la lishe ni muhimu,lakini kila siku tunapata masomo hospitalini tu,tena baada ya kuugua vyakutosha. Kumbe elimu ya lishe bora ingetolewa kwa ubora sana na hata haya magonjwa yanayoongezeka sasahivi yangepungua kama ukosefu wa nguvu za kiume.

(vi) MICHEZO NA BURUDANI.
Mimi nakumbuka shuleni kwetu waliokuwa wakicheza mpira sana niwale waliokuwa vilaza na wachache sana ndio walikuwa na akili darasani. Wale walioshiriki katika maigizo,ngoma na kuimba ni wale ambao walikuwa vilaza na wachache ndio walikuwa vizuri.

Wenye akili walipewa wasome risala, na kumvisha skafu mgeni rasmi. Hali hii inapelekea kuona michezo na burudani kama ni fungu la kukosa. Hata wazazi hufikia hatua ya kukataza watoto wao kujihusisha na michezo.

Serikali ingeipa nafasi michezo na burudani,na wazazi pia wangepata muamko. Tungepata si tu wachezaji hata makocha au maraisi wa vyama vya soka Tanzania na Afrika.

Hivyo serikali iangalie kwa mapana mambo haya na ikiwezekana mfumo wetu wa elimu basi uboreshwe kutokana na nyakati tulizopo.

DAVID M MROPE.
SUA.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom