Cicero
JF-Expert Member
- Jan 20, 2016
- 2,924
- 3,074
Habari zenu wadau.
- Kwa wale mnaofuatilia shughuli za Jumuiya ya Afrika Mashariki mtagundua kwamba Bunge la Afrika Mashariki limeshindwa kufanya kikao hata kimoja tangu kuchaguliwa kwa wabunge wapya, sababu kuu ikiwa ni Kenya na South Sudan kushindwa kuchagua wawakilishi wao kwenye bunge hilo. Kenya wanasingizia eti wako busy na uchaguzi wao mkuu na South Sudan walikosea kufuata procedure za kuchagua wabunge wa Afrika Mashariki kama ilivyo kwenye mkataba (wanawake hawakutimia idadi stahiki).
- Sheria na kanuni za bunge hilo zinasema kwamba akidi itatimia pale ambapo kutakuwa na wawakilishi walau watatu kutoka katika kila nchi mwanachama (I stand to be corrected on this).
- Hivyo basi kuna pendekezo limeletwa na wadau kwamba ili kuepuka deadlock kama hii inayosababishwa na system iliyopo ya uchaguzi, wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wawe wanachaguliwa na wananchi moja kwa moja sawa na wabunge wenzao wa kitaifa yaani kwenye uchaguzi mkuu unakuwa unamchagua Rais, mbunge wa Afrika Mashariki na mbunge wa Jamhuri kama ilivyo kwenye Umoja wa Ulaya na ECOWAS.
- Hili limekaaje? Ni zipi faida na hasara za hili pendekezo hususan kuelekea hatua ya mwisho ya mtangamano ambayo ni kuundwa kwa Serikali ya Shirikisho la Afrika Mashariki? Mimi kila siku I always say mnaopinga kuundwa kwa serikali ya EAC mmechelewa sana mtakuja shtuka kitu tayari kishasimama. Serikali haiundwi mara moja ila ni gradual process. Sasa hivi imeanzishwa passport ya pamoja ya EAC....mara inakuja sarafu moja ya Afrika Mashariki, bunge nalo ndo hilo liko mbioni kupewa more power and legitimacy. Yote haya ndio serikali ya EAC inavyoumbwa kama mtoto tumboni mwa mama yake!