SoC04 Pendekezo langu kwa serikali kuhusu Sekta za Elimu na Afya

SoC04 Pendekezo langu kwa serikali kuhusu Sekta za Elimu na Afya

Tanzania Tuitakayo competition threads

Davoo hiclan

New Member
Joined
Jun 29, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Kwa majina naitwa David naishi Arusha ila ni mkazi wa mwanza na nina umri wa miaka 20, wazo na maoni yangu kwa serikali ni kwenye Sekta mbili elimu na sekta ya Afya.

SEKTA YA ELIMU
Katika upande wa elimu ningependa kutoa maoni yangu kwenye uongozi husika kutokana na janga kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana wa kitanzania ningependekeza somo la stadi za kazi lifundishwe hadi sekondari ambapo litasaidia vijana kupata na kujifunza aina mbalimbali za ubuni ili waweze kujiajiri wenyewe na wasitegemee kuajiriwa. ili litakuza pato la nchi na uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

SEKTA YA AFYA
Maoni yangu katika upande wa afya ni kuiomba serikali na sekta husika ya afya kuwa na mkakati maalumu wa kukutanisha madaktari bingwa na wagonjwa angalau wiki moja kila baada ya mieze sita, na kutoa fursa kwa makampuni mbalimbali kufanya udhamini kwenye suala hilo ambapo itasaidia wananchi kupata huduma mbalimbali za kiafya ambazo pengine wasingeweza kukidhi gharama zake na hii itasaidia kuwa na Taifa lenye Afya njema kwa maendeleo zaidi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom