Denis Lucas Shio
Member
- Aug 2, 2022
- 60
- 75
1. UTANGULIZI
Viwanda ni moja kati ya shughuli ya kiuchumi ambayo muhimu katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa sababu viwanda husababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma zinazopatikana kwa watu kwa bei nafuu, hupunguza utegemezi kwa nchi zingine na inaboresha uchumi, hupelekea kupanda kwa kiwango cha maisha na kuongeza nafasi mpya za ajira. Kwa upande mwingine viwanda pia vina hasara zake hususani katika uchafuzi wa mazingira. Kwamfano moshi unaotoka viwandani unaposambaa katika hewa unaweza kuwa na adhari kwa binadamu, wanyama na mimea. Kwa sasa viwanda vingi vimewekwa mabomba maalum yanayoelekeza moshi kwenda katika anga lakini bado mfumo huo una athari ndani yake ambazo nitaziorodhesha hapa, na kupendekeza mfumo mpya na faida zake.
2. MFUMO UNAOTUMIKA KWA SASA
Idadi kubwa ya viwanda duniani vimesimikwa mabomba maalum kwa juu yanayoelekeza moshi kuelekea juu katika anga ambapo moshi viwandani umeelekezwa kwenda juu kwa kutumia mabomba maalum.
2.1. ATHARI ZA MFUMO UNAOTUMIKA KWA SASA
Mfumo huu unaathari mbalimbali ikiwemo kuharibika kwa tabaka la ozoni kwa sababu mfumo umeelekeza moshi wa viwandani kwenda kwenye anga. matokeo ya kuharibika kwa Tabaka la Ozoni ni kuruhusu mionzi ya jua (sun radiation) kufikia uso wa ardhi hivyo kutishia afya ya viumbe hai katika ikolojia mbalimbali. Mionzi ya jua ukifika katika uso wa dunia husababisha kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile mtoto wa jicho unaosababisha upofu, upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi, hivyo mtu aweza kuonekana mzee kuliko umri wake. Pia idadi kubwa ya watoto wapo katika hatari zaidi ya kupata madhara haya. Madhara mengine ni pamoja na kuathiri ukuwaji wa aina mbalimbali za mimea.
2.2. NJIA YA KUZIKABILI ATHARI
Njia ya kuzikabili athari za mfumo huu ni kubadili maelekezo wa mabomba ya moshi ambapo mabomba hayo yanapaswa yatokee kiwandani kuelekea chini ya ardhi ambapo kutakuwa na chemba maalum iliyotengenezwa kwa ajili ya kuuhifadhia moshi badala ya kuuelekeza mabomba ya moshi katika anga. Baada ya muda moshi huo unaweza weza kuvunwa kutoka katika ardhi na unaweza kutumia kama malighafi ya kutengenezea bidhaa mbalimbali kama rangi nyeusi ya kiatu (kiwi). Najua wengi mtajiuliza moshi unaweza vipi kuwa malighafi lakini ukienda katika bomba la kutolea moshi la gari au pikipiki ukichunguza utakutana na nta ya masinzi meusi yaliyotengenezwa na moshi kisha utakuwa umepata majibu ya swali uliokuwa unajiuliza.
3. MFUMO MPYA NINAOUPENDEKEZA KUZUIA ATHARI ZA MOSHI WA VIWANDANI
Mfumo mpya ninaoupendekeza utakuwa kama ifuatavyo;
(a) Bomba la moshi lililoelekezwa kwenda chini ya ardhi ambapo kutakuwa na chemba maalumu ya kuhifadhia moshi. Ambapo itakuwa tofuati na mfumo wa awali ambao mabomba ya moshi kutoka viwandani yalikuwa yameelekezwa juu ili moshi uelekee angani.
(b) Uwepo wa chemba maalum ya kuhifadhia moshi iliyotengenezwa chini ya ardhi ambayo itakuwa inatumika kupokea moshi katika mabomba maalum yaliyoelekezwa chini ya ardhi na kuhifadhia moshi. Chemba ya kuhifadhia moshi inatakiwa iwe imesiribwa au kuwekwa saruji katika kuta zake ili kuzuia sumu au kemikali iliyopo kwenye moshi isiingie katika udongo na kuathiri viumbe vinavyoishi chini ya ardhi pamoja na mimea.
(c) Uwepo wa mlango maalum katika chemba utakaokuwa unatumika kupakua malighafi itokanayo na moshi ili ikatumie kutengenezea bidhaa mbalimbali kama rangi nyeusi inayopakwa katika kiatu alimaarufu kama (KIWI).
3.1. FAIDA ZA MFUMO MPYA
Mfumo mpya wa kuelekeza mabomba ya moshi chini ya ardhi ambapo kutakuwa na chemba ya kuhifadhia moshi iliyotengenezwa chini ya ardhi unafaida zifuatazo;
(a) Husaidia kutunza mazingira kwa kuzuia uchafuzi wa hali ya hewa kwani moshi ukitapakaa katika anga hupelekea hali ya hewa kuchafuka.
(b) Kuzuia kuaribika kwa tabaka la ozoni kwa sababu moshi unatoka kiwandani unakuwa umeelekezwa chini ya ardhi katika chemba maalum na sio angani. Kama tabaka la ozoni halitoaribiwa mionzi mikali ya jua itakuwa haifiki kirahisi katika uso wa dunia na hupelekea usalama wa afya ya viumbe hai wa ainambalimbali. Pia huzuia kuongezeka kwa magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile mtoto wa jicho unaosababisha upofu, upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi.
(c) Hurahisisha upatikanaji wa malighafi ambayo inaweza kutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali kama rangi nyeusi inayotumika kung'arisha bidhaa nyeusi za ngozi kama viatu.
4. HITIMISHO
Mwisho ninapendekeza mfumo huu wa kuelekeza mabomba ya kusafirisha moshi chini ya ardhi katika chemba maalumu utumike katika viwanda ili kuhakikishiwa na usafi wa mazingira kwa kuthibiti moshi unaotoka katika viwanda usisambae katika anga na kusababisha uchafuzi wa hali ya hewa au uharibifu wa tabaka la ozoni ili kuepukana na athari mbalimbali zinazoweza kutokea baada ya kuaribika kwa tabaka la ozoni kama magonjwa ya kansa ya ngozi, uharibifu wa macho kama vile mtoto wa jicho unaosababisha upofu, upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi na kujikunja kwa ngozi. Athari hizo zitaepukika kwa sababu kama tabaka la ozoni litakuwa halijaharibika na mionzi mikali ya jua ambayo inaathari haiwezi kufika katika uso wa dunia kiurahisi.
Maana ya maneno yaliyotumika:
Tabaka la ozoni: hili ni tabaka la hewa ambalo liko katika anga la juu la pili lifahamikalo kitaalamu kama stratosphere ambalo linaweka aina ya tabaka ama tambara angani ambalo linazuia mionzi mikali ya jua inayoweza kuleta athari katika afya za binadamu na viumbe hai kuja moja kwa moja duniani.
Uso wa dunia: Maana yake ni ardhi.
MICHORO YA PICHA HAPO CHINI INAONESHA MFUMO UNAOTUMIKA KWA SASA NA PICHA NYINGINE INAONESHA MFUMO NINAOUPENDEKEZA KUZUIA ATHARI ZA MOSHI WA VIWANDANI.

Upvote
6