Kifurukutu
JF-Expert Member
- Aug 29, 2013
- 4,641
- 6,694
Wakuu nimekua mfuatiliaji wa mchezo wa mpira wa miguu hapa nchi na mdau wa michezo kwa ujumla wake!
Watanzania wengi tumekuwa tukihitaji kuona soka la vilabu vyetu pendwa likikua kufikia level za kutikisa vilabu kimataifa kama tp mazembe na nyingine nyingi barani Africa.
Uhitaji huu wa kukua kwa soka Tanzania, kwa muono wangu ningependekeza itokee muungano wa ligi kuu kwaTanzania nzima ili kuleta ushindani kwa timu zetu zote toka Zanzibar na Bara.
Suala la muungano kimichezo nahisi itakua chachu ya mabadiliko katika soka la tanzania, kukua kwa vilabu na baadae kukua kwa timu ya Taifa ambayo imekua kichwa cha mwendawazimu kila mtu ananyoa tu!
Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar kisiasa, kiuchumi na kijamii ni wa muda sasa,
je ni kitu gani kinakwamisha muungano huu kimichezo licha ya kuonesha unaweza kuleta mabadiliko chanya?
Watanzania tumekwama wapi katika vilabu vyetu bara na zanzibar?
Itapendeza sana wahusika waliangalie hili, siku za usoni tuwe na Tanzania premier league (TPL) kwa ustawi wa soka la Tanzania ndani na nje ya nchi.
Nawasilisha