Pendekezo; Muungano wa ligi Tanzania bara na Tanzania Zanzibar

Kifurukutu

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
4,641
Reaction score
6,694
Wakuu nimekua mfuatiliaji wa mchezo wa mpira wa miguu hapa nchi na mdau wa michezo kwa ujumla wake!

Watanzania wengi tumekuwa tukihitaji kuona soka la vilabu vyetu pendwa likikua kufikia level za kutikisa vilabu kimataifa kama tp mazembe na nyingine nyingi barani Africa.

Uhitaji huu wa kukua kwa soka Tanzania, kwa muono wangu ningependekeza itokee muungano wa ligi kuu kwaTanzania nzima ili kuleta ushindani kwa timu zetu zote toka Zanzibar na Bara.

Suala la muungano kimichezo nahisi itakua chachu ya mabadiliko katika soka la tanzania, kukua kwa vilabu na baadae kukua kwa timu ya Taifa ambayo imekua kichwa cha mwendawazimu kila mtu ananyoa tu!

Muungano wa Tanzania bara na Zanzibar kisiasa, kiuchumi na kijamii ni wa muda sasa,
je ni kitu gani kinakwamisha muungano huu kimichezo licha ya kuonesha unaweza kuleta mabadiliko chanya?

Watanzania tumekwama wapi katika vilabu vyetu bara na zanzibar?

Itapendeza sana wahusika waliangalie hili, siku za usoni tuwe na Tanzania premier league (TPL) kwa ustawi wa soka la Tanzania ndani na nje ya nchi.

Nawasilisha
 
Ni jambo zuri.
Eleza kidogo jinsi ya kufanikisha haya katika muktadha wa;
1. Udhamini ~ visiwani hatutaki.mdhamini anayeuza kilevi
2. Uchumi wa timu ~gharama za kutoka Gombani Pemba mpaka Kaitaba Kagera

3. Idadi ya timu ~ ukijumlisha timu za Zanzibar na Tanganyika utakuwa na ligi.yenye.timu nyingi sana tena zisizo na kiwango.
4. Namna ya kuunganisha TFF na ZFA~kumbuka visiwani.wanapigania uanachama FIFA baada ya kufanikiwa CECAFA na CAF.

Kwa kifupi ni ngumu kwa sasa kuwa na.ligi moja.
 
yaani hayo mliyokoloni hayajawatosha bado mwataka mengine,duh kweli mtu akizoea kula nyama ya mtu haachi,wao hayo mlionayo katika muungano wanataka watoke ilhali nyinyi mnafikiria kuendelea kuwatawala zaidi,kweli kuna tafauti kubwa ya khanithi na shoga.
 
Neno....
 
Unaongea hivyo alafu una kaduka kako kariakoo..tutawafanya watumwa mara ngapi leteni fyoko tukizamishe kijisiwa
 
Mkuu, bila shaka ni CAF siyo CUF
 
Nisivyoipenda Zanzibar yaani natamanigi hata tupigane nao vita wajitenge nasi
 
Tukiamua inawezekana tu swala kama udhamini,
Mkuu yote hii inawezekana tukiwa na nia moja ya kuendeleza michezo nchini!
watanzania waelimishwe namna muungano kimichezo utakavyoleta tija kwa taifa.

Suala la mdhamini asiehusika na kilevi, nchini tunamakampuni mengi sana kama ya mitandao ya simu, benk bima nk yanaweza kufanya udhamini, pia isue ya hali ya kiuchumi za timu nafikiri hii ndio mana ya kuwa na mdhamini katika ligi so litatatuliwa tu


Upande wa timu kuwa nying zisizo na ubora hii sidhani, kwani lazima tusimamie ligi daraja la kwanza iwe imara ili timu zinazopanda ziwe za ushindani na imara.
Timu 20 zinatosha sana kwa Tanzania nzima, zaidi mkanganyiko unaweza jitokeza mwanzo ni kwa namna gani tunaweza kuanzisha na kuunganisha timu hizi kwa pamoja.

TFF na ZFA ni kama nilivyosema hapo awali, tukae tuungane tuanzishe shirikisho la Tanzani nzima.
 
Mkuu hamna cha ukoloni hapa, muungano uwe kwa maslahi ya umma wa watanzania
 
Unaongea hivyo alafu una kaduka kako kariakoo..tutawafanya watumwa mara ngapi leteni fyoko tukizamishe kijisiwa
Kweli kabsa mkuu wamejaa huku bara halafu wanalia na mkoloni
 
Hilo swala wa Matopeni hawatakubali sababu kabla Ligi ya Mungano haijakufa Timu ya Wananchi ndio Bingwa wa Kihistoria wa hilo kombe hadi leo hii.
 
Unalisemea vp hili swala kwa sasa

Bado hamuhitaji ligi ya muungano?
 
Turudishe kombe LA muungano bingwa ndo atakayecheza club bingwa afrika. Sema bahati mbaya hili kombe wenzetu yeboyebo hawaliwezi wamezoea mizunguko ya timu 16 wahonge huko ndo wachukue kombe
 
Tanzania bara na Zanzibar ndio nini? Kama kuna Zanzibar kuna Tanganyika pia na kama kuna Tanzania bara basi kuna Tanzania visiwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…