Pengo: Kauli ya Askofu Niwemugizi (kwamba Katiba Mpya ndiyo kipaumbele cha wananchi) siyo msimamo wa Kanisa Katoliki

Huyu askofu kwanza arudishe pesa za escrow alizobeba kwenye mfuko wa sandarusi
 
Upepo umebadilikaje? Mbona wananchi huku "field" wako na CHADEMA bega kwa bega? Waza tu CHADEMA haifanyi hata mkutano mmoja bado mnahemewa jee na yenyewe ikiwa majukwaani si ndiyo kitakuwa kiyama chenu?
Labda field ya Jukwaa la Siasa la Jamiiforums
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Pengo ni kweli ana kiti Vatican, Pengo ni kweli anaweza kumpigia simu Papa, Pengo ni kweli alishiriki kumpigia kura Papa, Pengo ni kweli anajua mengi juu ya sheria za kanisa. Lakini alikuwa na haja gani ya keenda public kuwa maneno ya askofu mwenzake si msimamo wa kanisa. Hata Forum aliyotumia Niwemugizi wala haikuwa ya kanisa. Naye alitoa maoni yake kama Niwemugizi raia mwema na mwenye uchungu na nchi yetu.
 
Kwa nini huyo Askofu Niwemugiz hamkujadili hapa kama mnavyomjadili Pengo?
 
Naigopa kusema kawa *mnafiki*
[Corol=redmaharageyawapi!?]
 
Tulia na huyo babu wenu huko sisi tunamsikiliza bosi wake ambaye ni Askofu Niwemugizi yeye atabakia kuwa kadinali mpiga kura za upapa tu full stop
 
Wewe unalijua Kanisa Katoliki kuliko Kardinali Pengo ambaye anakaa meza moja na Papa? Pengo ana kiti chake Roma kwenye Meza moja na Papa, Pengo anaweza kuongea na Papa kwa Simu, wewe takataka unaweza kumpigia nani Simu hata akapokea?
Kanisa ni Mali ya Papa, yeye ni binadamu kama wengine, sijui amekula Maharage ya wapi?
 
Huwa hampendi kuambiwa ukweli.....
Mbna hamkumkosoa GWAJIMA kipindi kile yupo upande wenu....
Askofu PENGO yupo sahihi maana kaona mtu sahihi
Kama ambavyo Mbowe anavyosifia mazuri ya MAGUFULI....mbna hausemi ana kiharibu chadema?
Huwa mnasoma lkn au mnacoment tu.Hoja ni Pengo kupinga mabadiliko
 
Kanisa ni Mali ya Papa, yeye ni binadamu kama wengine, sijui amekula Maharage ya wapi?

Siyo kweli, kwa nini wewe siyo Papa wa Kanisa Katoliki kama unafikiri kila mtu anaweza kuwa Papa!
 
Tulia na huyo babu wenu huko sisi tunamsikiliza bosi wake ambaye ni Askofu Niwemugizi yeye atabakia kuwa kadinali mpiga kura za upapa tu full stop

Sasa kama ni hivyo povu lote la nini? Kwa nini mnajaza kurasa hapa hata kumjadili? Kwa nini msiendelee tu na huyo Askofu wenu?
 
Wakuu natanguliza salamu .

Maelekezo makuu ya Mungu kwa wanadamu ni kuishi katika kweli iliyojaa haki tupu , kutenda mema na kukataa maovu , hivyo tunategemea kiongozi yeyote wa dini ya kweli aishi na atende kama Mungu alivyoelekeza .

Kardinali Pengo anatenda kinyume na Maagizo haya ya Mungu , ni wazi ameamua kujipambanua kuukumbatia unafiki , Amejipachika usemaji wa Kanisa kinyume cha utaratibu .

Ni vema sasa Kwa kulinda heshima yake lililojiwekea miaka mingi , kanisa Katoliki linapaswa KUMTIMUA kardinali Pengo ili akaendeleze harakati zake za kupinga katiba mpya ndani ya chama chake cha ccm .

Naomba kuwasilisha .
 
Pengo wenu huyu ni useless kabisa hana msaada kanisani hadi nyumbani/familia na jamii kijijini kwake Mwazye,KALAMBO,Rukwa.Ukifika kwao utashangaa alivyoitelekeza familia/jamii yake.Ibada njema huanzia nyumbani
 
Sasa kama ni hivyo povu lote la nini? Kwa nini mnajaza kurasa hapa hata kumjadili? Kwa nini msiendelee tu na huyo Askofu wenu?
Tunataka na nyinyi muelewe kuwa ukadinali sio cheo yeye anatumia ignorance ya Watanzania wengi kwenye dini kuonyesha kuwa yeye ndiye boss na msemaji wa wakatoliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…