Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Zanzibar ina Rais, ina wimbo wa taifa, ina bendera ya taifa na ya Rais, ina Baraza la Wawakilishi, ina Baraza la Mapinduzi, ina Valantia, Mafunzo na KMKM, ina Serikali Kamili ya Mapinduzi SMZ, ni taifa kamili lililoungana na Tanganyika kutengeneza Tanzania bila kupoteza utaifa wake.
Mojawapo ya sifa za Rais ni kuamuru majeshi yoooote ya Ulinzi na Usalama kwa cheo chake cha Amiri Jeshi Mkuu. Tanzania ina Amiri Jeshi Mkuu mmoja tu anayeamuru majeshi (JWTZ, JKT, Polisi, Magereza, Mgambo, Jeshi Usu la Uhifadhi; Katiba ya JMT Ibara ya147 (2) na (4) ingawa ibara ndogo ya 4 haijataja Jeshi la Mgambo, Jeshi Usu la Uhifadhi, Mafunzo Znz, Valantia na KMKM) ambaye ni Rais wa Muungano (isome Ibara ya 147 pamoja na Ibara ya 148 inayohusu madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu ili upate muktadha mzuri):-
1. Je, vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM vinaamuriwa na Amiri Jeshi Mkuu (Rais wa JMT)? Au vinaamuriwa na Rais wa SMZ (Zanzibar) ambaye siyo Amiri Jeshi Mkuu?
2. Na kama Rais wa JMT hana Mamlaka kuamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM je, vinaamuriwa na nani?
3. Je, ni vibaya kama tukifanya marekebisho ya Katiba ili Rais wa Znz ambaye (naomba nitumie neno huenda) ndiye anayeamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM aitwe Amiri Jeshi wa Vikosi vya SMZ (tumuongezee hiyo title) ili kuweka perspective vizuri kwa vikosi vya SMZ kuamuriwa na Amiri Jeshi pia kama ilivyo itifaki ya majeshi duniani kote? Kwahiyo Rais wa Znz atakuwa na titles za Rais wa SMZ, Mwenyekiti wa BMZ (Baraza la Mapinduzi Zanzibar), Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na AMIRI JESHI WA VIKOSI VYA SMZ (kwa minajili ya itifaki tusimuwekee neno #Mkuu kwenye maneno “Amiri Jeshi Mkuu”).
4. Katiba ya Muungano (ambayo inafanyakazi Znz pia) inazuia mtu, shirika, kikundi isipokuwa serikali kuanzisha majeshi soma Sehemu ya Nane, Sura ya Tisa (Majeshi ya Ulinzi), Ibara ya 147, Ibara ndogo ya (1), uk. 203. Sasa basi, Ibara hii imetaja serikali ndiyo inayoruhusiwa kuunda majeshi lakini haijabainisha ni serikali ipi, ya JMT, ya SMZ au zote?
5. Na kama ni hivyo je, vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM vimeanzishwa na nani? Vinaamuriwa na nani? Anayeviamuru ana wadhifa wa Amiri Jeshi au Amiri Jeshi Mkuu? Je, vikosi hivyo si vinafanyakazi ndani ya mipaka ya JMT? Nani anaamuru ulinzi wa mipaka ya nchi (JMT)?
6. Kama suala la Ulinzi na Usalama ni suala la Muungano je, ni Rais wa JMT ndiye anayeamuru vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM? Au vinaamuriwa na Rais wa SMZ ambaye siye Amiri Jeshi Mkuu na wala siye Rais wa Muungano?
7. Kama tukiruhusu Rais wa Zanzibar awe Amiri Jeshi kwa vikosi vya Mafunzo, Valantia na KMKM je, Zanzibar itakuwa na Waziri wake wa Ulinzi (wa vikosi?)
Mwenye ufahamu na Katiba ya Zanzibar atujuze.
Tuko tayari kujifunza ambayo siyo dhambi hii.