Pengo la kapteni John Komba halijazibwa?

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
317
Reaction score
520
Wadau salaam. Nimekuwa nikisikiliza na kutazama nyimbo za maombolezo kufuatia kifo cha JPM, hakika sijasikia ToT wakitamba kama ilivyokuwa enzi za marehemu John Komba (hata Kama wametunga).

Mtakumbuka alipofariki dunia Baba wa Taifa, hayati Julius K. Nyerere, Komba ndiye alikuwa 'habari ya mjini'. Nyimbo zake za simanzi zilileta taifa katika maombolezo sahihi. Nyimbo za Komba zilianza kusikika saa 12 tu tangu kutangazwa kifo cha Baba wa Taifa.

Safari hii sivyo. Naona Bongo Fleva ndiyo wanatamba. Kidogo na za dini ambazo hata hivyo, siyo lengwa kwa maombolezo husika. Je, ToT hajatokea wa kuziba pengo la Komba au ni mabadiliko ya wakati?
 
Hajatokea wa kuziba pengo. Kwani hukuona hata kwenye kampeni.
 
Alikuwa ni alfa na omega yaani ni hivi, ToT ilikuwa ni Komba ndo maana bila Komba, ToT imejifia bila utaratibu
 
Haituhusu
 
Pengo gani kwani? Kila zama na kitabu chake alijisemea mzee Ruxa
 
TOT ya sasa imejaa waimba taarab tu! Akina Hadija Kopa na akina Abdul Misambano! Mwaka jana ili kuondokana na aibu, miccm ikaona bora iwarubuni Bongo fleva na Bongo muvi kuwavuta watazamaji.
 
Mpaka sasa hajatokea wa kuliziba pengo la Captain Komba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…