Pengo la Lissu, Mnyika na Zitto halijazibwa bungeni! Hizi tozo za kizalendo zisingepita bila marekebisho makubwa!

Pengo la Lissu, Mnyika na Zitto halijazibwa bungeni! Hizi tozo za kizalendo zisingepita bila marekebisho makubwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kiukweli kilio cha wananchi huko mitaani kuhusu maumivu ya tozo za kizalendo au mshikamani kimekuwa kikubwa mno.

Wananchi wanawakumbuka Tundu Lissu, J J Mnyika na Zitto Kabwe na kusema hivi " vidume" vingekuwepo bungeni ama tozo hizi zisingepita au zingepita baada ya kufanyiwa marekebisho makubwa sana.

Wewe mdau unasemaje?
 
Tunalipa kodi. 3% ya watanzania ndio waliokuwa wanalipa. Sasa hii ndio dawa yetu
Wengine kazi yao kudai serikali inawepe maendeleo. Hela za maendeleo zitatoka wapi? n
 
Napendekeza 2025
Vyama vyote vya upinzani visiingie kwenye uchaguzi.
Wapite tu bila kupingwa,kwani hata wakiingia wapinzani hoja zao huzuiliwa nakufungiwa ubunge.
Vyama vibaki kutoa elimu kwa wananchi
 
Ndio tatizo la viongozi wasio na maono ,wanashindwa kubuni vyanzo vipya wao wameng'ang'ania kule kule.
 
Tunalipa kodi. 3% ya watanzania ndio waliokuwa wanalipa. Sasa hii ndio dawa yetu
Wengine kazi yao kudai serikali inawepe maendeleo. Hela za maendeleo zitatoka wapi? n
Kuna tofauti kati ya kodi na tozo bwashee!
 
Sifanyi tena ujinga wa Kutuma fedha labda iwe emegency Wazee wangu wanaumwa Kujijini
 
Napendekeza 2025
Vyama vyote vya upinzani visiingie kwenye uchaguzi.
Wapite tu bila kupingwa,kwani hata wakiingia wapinzani hoja zao huzuiliwa nakufungiwa ubunge.
Vyama vibaki kutoa elimu kwa wananchi
Naamini kile kipindi kimepita. Kwa kweli ingawa bunge ni live hamu sina
 
Kujifunga mkanda huleta maumivu....

Dr.Mwigulu Nchemba alitutaka tujiandae KISAIKOLOJIA....

Baada ya miaka takribani 6 Serikali yetu adhimu ilijifunga mikanda kwa kutoajiri kwa upana kinyume na muda huu mfupi wa AWAMU YA 6.....

1)Walimu zaidi ya 6000 wameajiriwa na TAMISEMI...Hawa wanahitaji kulipwa POSHO kabla ya kuwaingiza katika PAYROLL...UNAZIPATAJE HIZO FEDHA BILA YA WANANCHI KUFUNGA MIKANDA?!!!

2)Watumishi wa afya zaidi ya 2000 wameajiriwa na TAMISEMI NA WIZARA YA AFYA.
Hawa unawalipa bila ya kuongezwa kwa vyanzo vya mapato?!!!

3)Miradi ya kimkakati....SGR ,BWAWA LA KUFUA UMEME LA JKN.Fedha tutazitoa wapi bila ya kuikaza mikanda?!!!

HATUWEZI KUYATAKA MAENDELEO BILA YA KUIPITA NJIA NGUMU.....

#KaziIendelee
 
Kilio ni kikubwa kwenye mitandao na siyo mitaani. Wanasiasa wanachochea kilio za kuigiza kwa maslahi yao tu ya kusaka madaraka. Kodi hizi tajiri analipa, mbunge analipa, mkulima analipa, mwanafunzi analipa, mfanyakazi analipa kwa kadri ya matumizi yako tatizo liko wapi. Tulipe kodi. Nchi huendeshwa kwa kodi.

Matajiri waliporwa hakuna aliyewatetea na wakakimbia nchi na mitaji yao. Leo wigo wa kodi umepanuka kelele tusimyumhishe mama na serikali yake.

Akikubali na akashindwa kumaliza miradi na kuleta nafuu ya wananchi kwa kuondoa kero za afya, elimu, miundo mbinu ni lawama kubwa mno kuliko hii ya kulipa kodi ya miamala, mafuta nk.
 
Wapinzani walitengeneza diversion ya hili jambo kwa kujua au kutojua.

Hata kama wapo nje ya Bunge lakini bado wakati haya yakifanyika Bungeni wao waliwekeza nguvu na muda kudai Katiba Mpya.

Huu ni ukosefu wa kujua nini Cha kusimamia na Kwa namna gani.

Tuna upinzani dhaifu Sana na usiokuwa na malengo.
 
Wapinzani walitengeneza diversion ya hili jambo kwa kujua au kutojua.

Hata kama wapo nje ya Bunge lakini bado wakati haya yakifanyika Bungeni wao waliwekeza nguvu na muda kudai Katiba Mpya...
Watu mkiishiwa hoja huwa mnaandika vituko sana. Ndugu si ukubaliane tu kuwa hapa CCM mmevuruga sana na wapinzani hawapo kabisa? Kwani bajeti inasomwa mitaani au Bungeni?
 
Back
Top Bottom