Pengo la Lissu, Mnyika na Zitto halijazibwa bungeni! Hizi tozo za kizalendo zisingepita bila marekebisho makubwa!

Tunalipa kodi. 3% ya watanzania ndio waliokuwa wanalipa. Sasa hii ndio dawa yetu
Wengine kazi yao kudai serikali inawepe maendeleo. Hela za maendeleo zitatoka wapi? n
Sio asilimia 3% Watu approx 500 ndo big tax payer. Hawa wengine huwezi wategemea maana ni unstable mpaka wakuzwe. Tunataka kodi ikusanywe kwa watu wachache mpaka wafungiwe account zao bank yaani au wakimbie tuhamie kwa hawa wafanyabiashara unstable tufunge accont zao wakishindwa halafu mwishoni tubaki bila walipa kodi?

Ukisikia makusanya yapo juu ujue kuna mtu amechangia, safari hii ni wote kidogo kidogo.
 
Walipo kuwa bungeni mkuliwa mnawatukana
 
Iko wazi na inajulikana kbs ✔️✔️ Ila sasa ngoja waje vijana wako MATAGANIST hapa uone moto wake 😂😂😂
 
Ukiacha unafiki unaongea ukweli
 
Tunalipa kodi. 3% ya watanzania ndio waliokuwa wanalipa. Sasa hii ndio dawa yetu
Wengine kazi yao kudai serikali inawepe maendeleo. Hela za maendeleo zitatoka wapi? n
3% ndio walipa kodi? Ile VAT iliyopo kny kila muamala unaofanya sio kodi? Kila mtu analipa kodi iwe directly au indirect. Ukiweka vocha tu kuna kodi hapo umelipia. Kitendo tu cha kununua kitu kwa mangi ambacho sio exempted with tax na wewe umelipia kodi. Huu mpango ulioletwa ni mpango tofauti na kodi walichofanya ni utapeli
 
Kwa hiyo wewe hutaki kulipa tozo? Sasa hao uliowataja endapo wangepinga kama ambavyo walikuwa wanapiga siku zote lakini zinapita ndio ingesaidia kupeleka maendeleo majimboni kwao?
 
Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake 😂😂😂. Yaan pamoja na kuwatoa kweny ubunge mpaka huko mtaani bado mnawashutumu tu kweny hili? Uko nje ya bunge huna ushawishi wa kimageuzi wa kupinga hoja flan. Ila upinzani nchi hii unatupiwa kila baya, mara utasikia wapinzan wametuchelewesha sana 🤣🤣🤣🤣👆
 
Sasa kama unajua hilo kodi ikiongezwa kidogo kuna shida gani? Kwani mahitaji yanapungua au kuongeza?

Wabunge wamepitisha kwa sababu wao ndio wanajua shida za barabara majimboni kwao,maji,afya na elimu .. unadhani hizo pesa zisingeelekezwa huko wangekubali?

Nyie mijitu ya Mjini hamjui kwamba Vijijini wamama wanakufa kwa uzazi Kisa barabara mbovu na kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya ,wanashinda kutwa nzima kutafuta maji wanayogombea na wanyama.,Kama kwamba haitoshi watoto wanasafiri umbali mrefu kufuata shule tena kwenye makorongo,hujamsikia Mtaka juzi?

Kwa hiyo unataka usitozwe hizo tozo Ili Hali iendelee, kwenye madini mnakopiga kelele Mwaka mzima mapato yake hayafiki hata bil.600 kwa aina zote za Madini .

Kazi imeshaanza👇







 
Kwani na Mzee Mgaya analipa Tozo?😅😅
 
Mijitu ya mjini ndio hio hio kina mwigulu, raisi wako na wenzie. Wewe unasema habari za vijijini hiyo ni kazi yangu au ya serikali. Si kila siku tunaimbiwa nchi ni tajiri kwanini mje kuumiza wananchi. Wabunge kwanini wasingesema wakatwe wao pesa zitumike huko vijijini? Hizi tozo kwani wanakatwa wa mjini peke yake au unajitoa UFAHAMU TU??
 
Serikali inakunya pesa za kutekeleza wajibu au lazima wewe ulipe ndio itekeleze? Lipa kodi acha kulia Lia hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…