Pengo la Lissu, Mnyika na Zitto halijazibwa bungeni! Hizi tozo za kizalendo zisingepita bila marekebisho makubwa!


Vyanzo vya kodi nchi ni vichache kiasi hicho?
 

Haitoshi kulipa mishahara na posho. Haitoshi kujenga barabara na kupeleka maji vijijini. Ndio maana tunafunga mikanda.
Kinachouma sana ni kuona watu wanafuja pesa za walipa kodi na waachwa hivi hivi. Kuna scandals kadhaa na bado wengine wachache wanataka kutengeneza nyingine. Hasa kwenye miradi hewa au kuongeza gharama za miradi. Shoka liko shinani.....
 
Wananchi wengi wanamkumbuka magufuli na sio hao uliowataja
 
tatizo wameyaacha majembe kina mbowe lisu na msigwa, wakawapeleka bungeni warembo wa kutomaswa, kushikwashikwa, kubembelezwa na kulegea eti ndo wakawe wapinzani bungeni.
 
Kuna tofauti kati ya kodi na tozo bwashee!
Mkuu hakuna tofauti hapo, hizo ni mbinu za kutofautisha maneno ili matamshi yaonekane tofauti lakini kitu ni kilekile, MWANACHI KUTOA FEDHA NA KUIPATIA SERIKALI KWA MATUMIZI YAKE.
 
Inawezekana wewe haya makodi na madude mengine yanayotuumiza watanzania hayakuhusu... Kaa kimya
 
Msiache kumfuatilia ex MP Peter msigwa kwny kipindi cha Agenda sa 3:00 usiku muone mlivyopoteza vichwa bungeni kwa ujinga wa kijani tupu
 
Tunalipa kodi. 3% ya watanzania ndio waliokuwa wanalipa. Sasa hii ndio dawa yetu
Wengine kazi yao kudai serikali inawepe maendeleo. Hela za maendeleo zitatoka wapi? n
Hakuna mtanzania asiyelipa kodi,iwe direct au indirect
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…