Peniela (Story ya kijasusi)

Mkuu huu mzigo ni balaaaa
Usikawie sana kutupia episode zinazofuatia
 
SEASON 2
SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA SEHEMU ILIPOISHIA
“ Flaviana ninakuhakikishia kwamba nitatumia vyombo vyote vya usalama unavyovifahamu kumtafuta mumeo kuwatafuta watu waliofanya kitendo kile.Nakuhakikishia kwamba hakuna ambaye ameshiriki katika shambulio lile atabaki huru.Lazima wote wapitiwe na mkono wa sheria.” Akasema Dr Joshua na kidogo Flaviana akapata faraja .
“ Dr Kigomba amefanya uzembemkubwa sana.Suala lile halikuwa la kuchukulia kirahisi rahisi kama alivyolichukulia.Kwa sasa amesababisha tatizo jingine kubwa.Ametupa tena kazi ya kumsaka Elibariki na kufahamu mahala aliko.Elibariki anaufahamu ukweli wa nini kilimuua Flora na tukio la leo litamfanya aamini kabisa kwamba anatafutwa auawe kutokana na kuufahamu ukweli. Kigomba ndiye aliyesababisha haya yote.” Akawaza Dr Joshua akiwa amekasirika sana
“ lakini inawezekanaje Elibarik i asiwemo ndani ya hilo gari ? Kuna mtu alimpa taarifa? Na huyo mtu ambaye alikuwa akipambana na vijana wetu ni nani? Akajuliza Dr Joshua
“ hapa lazima kuna jambo linaloendelea.Lazima ufanyike uchunguzi wa kina kubaini ni kitu gani ambacho kinaendelea.hainiingii akilini kwamba Elibariki asiwemo ndani ya gari wakati vijana wamemfuatilia toka alipotoka hapa.Kama hakuwemo ndani ya gari yuko wapi? Uchunguzi wa kina unahitajika katika jambo hili.” Akawaza Dr Joshua

ENDELEA…………………
Dr Joshua aliitisha kikao cha dharura na washirika wake wakubwa Dr Kigomba na Captain Amos lengo likiwa ni kujadili kile kilichotokea usiku ule..
“ Jamani nimewaiteni hapa kwa dharura ili tujadili jambo lililotokea usiku huu.Kama mnavyofahamu mambo yameanza kwenda tofauti na matarajio.Mpango wetu haukuenda kama tulivyokusudia na hii ni kwa sababu ya kukosekana kwa umakini na usimamizi madhubuti .Makosa mengi yamefanyika ambayo sasa yanatulazimisha kufanya kazi ya ziada kuyarekebisha.Niliwataarifu toka awali kwamba Elibariki ni mtu hatari sana kwetu kwa sababu tayari amekwisha nusa harufu ya kinachoendelea hapa.Amekwisha fahamu sababu ya kifo cha Flora kiyu ambachohakutakiwa mtu yeyote kukifahamu .Japokuwa tumefanikiwa kuonyesha kwamba taarifa yake haikuwa na ukweli wowote ndani yake lakini bado ni mtu hatari sana kwetu.Suluhisho peke e lilikuwa ni kuwahi kummaliza lakini kumefanyika uzembe mkubwa katika mpango huo na kushindwa kufanikiwa.” Akasema Dr Joshua
“ Shambulio limefanyika lakini amekufa mtu mwingine kabisa tofauti na mtu tuliyekuwa tunamtaka.Sijawaita hapa ili kulaumiana kwa kilichotokea lakini nimewaita hapa ili kutafuta namna ya kusahihisha makosa yaliyofanyika.Elibariki bado yuko hai na amejificha mahala.Tunatakiwa tumtafute kwa kila njia hadi apatikane.Lakini kabla ya hapo kuna maswali kadhaa ambayo lazima tuyatafutie majibu.Kwanza ni kwa nini Elibariki hakuwemo ndani ya gari lake? Ni nani aliyekuwa akishambuliana na vijana wetu ? Je ni Elibariki mwenyewe au kuna mtu wingine? Kama ni mtu mwingine ni nani? Amewafahamuje vijana wetu? Haya nimaswali ambayo Lazima tupate majibu yake..Nina wasi wasi sana yawezekana kukawa na kuvuja kwa siri na ndiyo maana Elibariki akaponyoka kwa sababu hainiingii akilini ni kwanini hakuwemo ndani ya gari lake wakati vijana walikuwa na uhakika kabisa kwamba ameingia ndani ya gari lake.” Akasema Dr Joshua
“ Mzee ninaweza kukubaliana nawe kwa sababu nimezungumza na mtu ambaye alikuwa akimfuatilia toka ameingia hapa usiku huu alisema kwamba alifika hapa na kuonana na mkewe wakaelekea bustanini wakaongea halafu akaelekea katika gari lake na kabla ya kupanda katika gari aliongea kwanza na simu na baada ya muda akaingia katika gari lake na kuondoka.Kwa mujibu kijaa huyo ni kwamba elibariki si aliyekuwa akiendesha hilo gari.Kulikuwa na mtu aliyekuwa anaendesha na ninadhani ndiye aliyekutwa amekufa.Ina shangaza sana namna alivyonusurika .Nina wasiwasi yawezekana kweli kuna uvujaji wa siri zetu.” Akasema Dr Kigomba
“ Kigomba lifanyie kazi hilo suala haraka iwezekanavyo.Tunatakiwa tufahamu kama kuna uvujaji wowote wa taarifa zetu.Vijana wetu wanatakiwa wachunguzwe kama kuna mmoja kati yao ambaye anatoa siri zetu nje.Hili ni jambo la haraka sana kulifanya vinginevyo mipango yetu yote itakawama na juhudi zote za miaka mingi zitakuwa kazi bure.Hatutaweza kuupata utajiri ule ambao tunatarajia kuupata endapo hakutakuwa na juhudi za makusudi za kuhakikisha suala hili linafika mwisho.Ndugu zangu tumeshughulika na suala hili kwa miaka mingi na tunaelekea ukingoni kwa hiyo tukifanya mchezo tunaweza kushindwa kulimaliza salama na mkumbuke kwamba endapo tukishindiwa kulimaliza salama basi ndio utakuwa mwisho wetu.” Akasema Dr Joshua
“ Ni kweli Dr Joshua kumeanza kuonekana vizingiti hasa katika hatua hizi za mwishoni.Mwanzo tulianza vizuri sana lakini baada tu ya Dr Flora kuingia na kifahamu suala lile mambo yalianza kwenda ndivyo sivyo.”akasema Captan amos.Dr Joshua akadakia
“ Usiwe na shaka kuhusu Flora .Nina hakika hakumweleza mtu yeyote.lakini alitaka kuwaeleza watoto wake ndipo tukamuwahi.Nina hakika ulimi wake haukuwahi kutamka chochote kuhusiana na jambo hili.”
“ Dr Joshua nitalisimamia suala hili la uchunguzi na nitahakikisha kila kitu kinakwenda kama ulivyoagiza.Pamoja na hayo kuna kitu Fulani ambacho ninataka kukushauri”
“ Ni kitu gani hicho Kigomba? Akauliza Dr Joshua
“ Njia nyepesi ya kumpata Elibariki kwa haraka ni kuelekeza macho yetu kwa mke wake .Nina hakika lazima atawasiliana naye na atamuelekeza mahala alipo .Flaviana ni njia rahisi sana kwetu ya kumpata Elibariki”
“ Kigomba ,tayari mmekwisha unganisha simu ya Flaviana na mnaweza mkafuatilia kila atakachoongea simuni inatosha sana lakini kama unaona kuna ulazima wa kumfuatilia basi fanya hivyo kwani kwa sasa chochote kinachoweza kutusaidia hatutakiwi kukipuuza.” Akasema Dr Joshua.
“ Sawa nimekuelewa mzee.”
“ Nataka mpaka kesho jioni nitakaporejea toka katika mazishi tayari muwe na majibu ya mambo haya niliyowaelekeza.Sitaki tena majibu ya kisisa.Ninataka matokeo mazuri” akasema Dr Joshua
“ Tumekuelewa mzee.Tutajitahidi kufanya kama ulivyotuelekeza” akasema Dr Kigomba
“ Sijui ni kwa nini kumeanza kutokea vizingiti katika hatua za mwishoni kabisa za mpango wetu.Lakini hakuna kitakachoharibika ,lazima kila kitu kitakwenda kama kinavyotakiwa.Tukishampata Elibariki roho yangu itakuwa imetulia lakini vinginevyo sintakuwa na amani kabisa.Bado naendelea kujiuliza ameponaje katika shambulio lile? Nina hakika asilimia mia moja kwamba lazima kuna mtu ambaye alimpa taarifa za kuwepo kwa shambulio .Lakini hata kama alipewa taarifa mbona vijana wetu hawakumuona akishuka sehemu yoyote toka alipotoka hapa? Alitowekaje ndani ya gari? Akajiuliza Dr Joshua baada ya akina Kigomba na Amos kuondoka

*******

Osmund alitoka ofisi kuu ya Team SC 41 akachoma mafuta hadi nyumbani kwa John Mwaulaya.Akafululiza hadi chumbani kwa John ambaye hali yake kidogo ilikuwa umeimarika
“ Hallo John” akasema Osmund
“ habari yako Ossy. Sijakuona toka asubuhi ya leo.Ulikuwa wapi?
“ John nilikuwa na mizunguko mingi sana siku ya leo.Unaendeleaje?
“Ninaendelea vizuri sana.Nyie mnaendelaje?
“ Tunaendelea vizuri .Nimeongeana mkuu toka Marekani na anakupa pole sana ila amesema kwamba anasubiri taarifa ya Dr Burke ili aweze kujua ni namna gani ya kuutibu ugonjwa wako” akasema Osmund
“ Hakusema kitu kingine? Akauliza John
“ Alikupa pole nyingi.Vile vile nimeongea na Peniela na amesema kwamba anahitaji kukuona” akasema Osmund
“ Ana matatizo gani? akauliza John
“ Hakuniambia ana matatizo gani ila alisema kwamba ni suala binafsi”
Kimya kikapita Osmund akimtazama John mwaulaya.
“ Mtaarifu kwamba nitaonana naye kesho jioni”akasema John
“ Sawa mzee” akasema Osmund akiendelea kumkodolea macho John
“ Mbona unanitazama hivyo Osmund ? Kuna kitu unataka kuniambia? Unataka kuniambia kuhusu vifo vya vijana wetu sita ? Akauliza John na kumstua sana Osmund.Hakuwa ametegemea kama John tayari anafahamu kuhusiana na vifo vile.
“ Osmund kwa nini ukanificha kuhusiana na tukio hilo? Akauliza John
“ Ulipaswa kuja kwangu na kunieleza kila kitu kuhusiana na kilichotokea .Kwa nini hukutaka ushauri wangu ? Ulifikiri kwamba sintajua kilichotokea ? Osmund usidhani kwamba kwa vile niko kitandani sijiwezi basi sina nafasi tena katika Team Sc41.Mimi bado ni mkuu wa Team SC41.Nimeianzisha mimi na ninaifahamu vizuri kuliko yeyote kati yenu kwa hiyo kabla ya kufanya jambo lolote unapaswa kwanza kuja kwangu na kunitaarifu ili nikupe ushauri.Mwili wangu hauna nguvu lakini kichwa change bado kina uwezo mkubwa wa kuongoza” Akasema John
“ John sikukueleza kutokana na haliyako lakini hupaswi kunilaumu John kwa kilichotokea kwa sababu nilifanya kila kitu kwa sababu yako.Kama isingekuwa ni kwa sababu ya ugonjwa wako nisingemteka mke wa yule daktari,”
“ Hukupaswa kufanya vile.Team SC 41 si kikundi cha watekaji.Si kikundi cha mapigano.Ungejua athari ya kitu ulichokifanya usingesimama hapa ndani na kusema kwamba ulifanya kwa ajili yangu.” Akasema John.Osmund akakaa kimya kwa muda kisha akasema
“ Dr Burke anakuja kesho kujakuona afya yako na ndiye atakayetoa mapendekezo ya namna ya kukutibu” akasema Osmund.
“ Thank you” akasema John
“ Anything you need John?
“ Nothing.Just leave me alone” akasema John.Osmund akamuangalia na na kutoka
“ Peniela ana matatizo gani? Kwa nini anataka kuniona? Akajiuliza John baada ya Osmund kutoka
“ Inawezekana kuna jambo linamsumbua hadi akataka kuja kuniona? Ninajua ana hamu sana ya kukaa name na kuongea name.Ana mambo mengi ambayo anataka kuyafahamu toka kwangu na mimi pia nina mambo mengi sana ambayo ninatamani kumweleza lakini ninashindwa namna ya kumwambia. Natamani afahamu kuhusu wazazi wake lakini sijui atanielewaje endapo nitamwambia kwamba ni mimi ndiye niliyewaua wazazi wake.Kuna mambo mengi ambayo anatakiwa ayafahamu Peniela lakini ninashindwa namna ya kumfahamisha.” Akawaza John baada ya Osmund kutoka mle chumbani
“ Laiti kama ningekuwa nina uhakika wa kuishi kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa huu unaonisumbua ningemfanyia Peniela mambo makubwa kufidia maumivu mengi niliyomsababishia katika maisha yake,kufidia maisha yake niliyoyaharibu kwa kumuingiza katika team SC41.Ingawa bado sijachelewa sana lakini kuna mambo ambayo nikiyakumbuka kuhusu Peniela huwa yananiumza sana.Kubwa ambalo nina hakika endapo atalifahamu atakasirika sana ni kitendo cha kumuua mvulana wake wa kwanza Peter mtoto wa tajiri mmoja mkubwa hapa nchini.Mahusiano yao yalianza wakati Peniela akiwa kidato cha pili .Sikutaka Peniela awe na mahusiano ya kimapenzi kwa sababu nilikuwa na mipango tayari ya kuja kumtumia katika shughuli muhimu za Team SC41.Peniela aliumia sana kwa kifo cha Peter .Japokuwa ni muda mrefu umepita lakini bado naikumbuka siku ile .” akawaza John na kufumba macho akavuta kumbu kumbu
Ni siku ya jumamosi wanafunzi sita wa shule ya sekondari ya Hope Secondary ,shule ambayo wengi wa watoto wanaosoma hapa ni wenye uwezo mkubwa kifedha, wakiwa katika magari matatu waliamua kutoka na kwenda matembezini nje kidogo ya jiji.Kila mmoja alikuwa na mpenzi wake na walionekana kuifurahia sana safari yao.Hawakujua kama nyuma yao kulikuwa na gari inawafuatilia kila sehemu waliyokwenda.
Wanafunzi wale walifika mahala kulikokuwa na uwanda mpana wa majani mazuri wakatoa vitu walivyokuwa wamebebea kama vile vinywaji na kuanza kuburudika kila mmoja na mpenzi wake.Wakati wakiendelea na burudani yao wakiwa hawana wasi wasi wowote ghafla wakavamiwa na mtu aliyekuwa amejificha uso wake na akawalazimisha wote walale chini.Mtu yule aliyekuwa na akamuamuru Peter asimame na kumpigisha magoti mbele ya wenzake na kisha akaanza kumiminia risasi yule kijana alifariki pale pale.Yalikuwa ni mauaji ya kutisha ambayo Peniela aliyashuhudia kwa mara ya kwanza katika maisha yake.
Kumbu kumbu ile limfanya John Mwaulaya ahisi kama kuna kitu kikali kinaukata moyowake.
“ kwa nini nlikuwa mkatili namna hii ? Nilitoa uhai wa watu wengi wasio na hatia na sikujua kama siku moja na mimi nitakinusa kifo.Death is so scary “ akawaza John
*****
Mathew na Eva walisimamisha gari katika baa moja maarufu ijulikanayo kama mkombozi.
“ kwa mujibu wa Sabina ni kwamba nyuma ya baa hii kuna nyumba ya bibi yake ina vyumba vinne na kuna kilabu cha pombe za kienyeji.Alisema nimuulizie bibi Mariana.” Akasema Eva wakashuka ndani ya gari na kuzunguka nyuma ya ile baa ya mkombozi ni kweli kulikuwa na kilabu cha pombe za kienyeji na kulikuwa na idadi kubwa ya watu.Eva akamfuata mama mmoja na kumuuliza kama anaweza kumpata bibi Mariana akaelekezwa kwamba ni yule aliyekuwa akiuza pombe.Akamfuata na kumsalimu akamuomba waongee pembeni.
“ Bibi samahani kwa kukusumbua katika biashara “ akasema Eva
“ Bila samahani mwanangu.” Akasema Bibi Mariana
“ Nimekuja hapa nimeagizwa na Sabina”
“ Sabina? Bi Mariana akastuka
“ Ndiyo bibi”
“ Yuko wapi huyu mjukuu wangu? Ni muda mrefu sijamuona na hajafika hapa kwangu.”
“Bibi Sabina yuko safari .Ni rafiki yangu tulikuwa wote safari nje ya mkoa .Kuna biashara Fulani tunafanya wote na mimi nimerudi mara moja kuja kuchukua mzigo na ninaondoka kesho asubuhi sana na ndiyo maana imenilazimu kuja hapa kwako usiku huu” akasema Eva
“ Wala usijali mwanangu.Haka kajukuu kangu hakajambo?
“Sabina mzima kabisa bibi,anaendelea vizuri”akasema Eva
“ Nashukuru kama anaendelea vizuri” akasema bibi Mariana
“ Bibi Sabina amenituma nikuletee mzigo huu hapa” akasema Eva na kufungua pochi yake akatoa bunda la noti na kumpatia.
“ ouh Mungu wangu ahsante sana.Mungu awabariki sana na awazidishie mafanikio” akasema Bi Mariana
“ Amina bibi.Halafu pia amenituma kwamba unipe ule mzigo wake niende nao”
“ Sawa mwanangu ngoja nikakuletee sasa hivi .” akasema Bi Marina na kuingia ndani .Alikuwa nafuraha ya ajabu kwa kupewa bunda lile la noti.Mathew alikuwa amesimama mbali kidogo na hakutaka kuwasogelea
Baada ya kama dakika kumi hivi Bi Mariana na kurejea akiwa na mfuko wa nailon
“ Samahani kwa kuchelewa unajua mzigo wenyewe nilikuwa nimeuficha mbali kwa sababu alisema kwamba niufiche mbali “
“ Ahsante sana bibi nashukuru”
“ Hata mimi nashukuru mjukuu wangu.Msalimu sana Sabina mwambie mzigo nimeupokea na ninashukuru sana” akasema Bi Mariana akaagana na Eva akaondoka ,
“Mzigo huu hapa “ akasema Eva akimkabidhi Mathew mzigo ule.Walipofika garini Mathew akaufungua .Kulikuwa na kiboksi chenye ukubwa wa karatasi ya barua lakini kilikuwa cha chuma na kilikuwa kimefungwa kwa ufunguo .
“ hakukupa ufunguo wa kiboksi hiki?akauliza Mathew
“ Hapana hakunipa”akajibu Eva
“ Ok nitakwenda kukifungulia nyumbani.Ahsante sana Eva Umenisaidia sana” akasema Mathew na kuwasha gari wakaondoka
“Mathew wewe ni rafiki yangu na umenisaidia mambo mengi sana lakini naomba nikueleze ukweli kwamba sijafurahishwa hata kidogo na kitendo ulichokifanya leo kwa Sabina.Ule si ubinadamu hata kidogo” akasema Eva huku akionekana bado amekasirika
“ Eva,kama nilivyokwamba awali kwamba kazi yangu wakati mwingine inahitaji kufanya maamuzi magumu ili kufanikisha baadhi ya mambo.Maamuzi magumu niliyoyafanya yametusaidia tumeweza kukipata kitu ambacho ni cha muhimu sana.Jifunze kufanya maamuzi magumu katika kazi zako” akasema Mathew
“ Mathew achana na maneno hayo ya wanasiasa .Maamuzi magumu katika kuhatarisha uhai wa mtu? Unajua ni kiasi gani umehatarisha uhai wa Sabina kwa ajili ya hiki kiboksi tu? Akasema Eva.Mathew akamtazama na kusema
“ Unajua ni watu wangapi wamepoteza uhai wao kwa sababu tu ya hiki unachokidharau? Akauliza Mathew na hawakuendelea tena na maongezi .Wakati safari ikiendelea kimya kimya Anitha akapiga simu
“ Hallow anitha “ akasema Mathew
“ Mathew nimefankiwa kupata taarifa za Habid soud.Huyu ni mtoto wa tajiri mmoja mkubwa nchini Saudi Arabia anayemiliki visima vya mafuta.Habib soud anatajwa kama mmoja wa vijana wenye mafanikio makubwa sana nchini mwao.Hizo ndizo taarifa zake ambazo nimezipata lakini ninaendelea kumchimba zaidi ili niweze kuzipata taarifa zake za kina”
“ Good Job anitha.Niko njiani ninakuja .Noah amekwisha rejea?
“Hapana bado hajarejea. Umefanikiwa kuupata ule mzigo?
“ Ndiyo nimefanikiwa kuupata” akasema Mathew
“ Good job Mathew” akasema Anitha na kukata simu
Eva bado aliendelea kuonyesha kukasirika na hakutaka maongezi tena na Mathew
“ Eva najua umekasirika sana lakini nakuomba usifanye hivyo.Kazi yangu inanilizimu kufanya vile nilivyofanya” akasema Mathew
“ Nikifika sasa hivi kama Sabina yuko bado hai basi nitaondoka naye.Sitaki aendelee tena kukaa pale kwako” akasema Eva
“ Usijalie Eva.kwa sasa sina haja naye tena.Unaweza ukamchukua” akasema Mathew
Walifika nyumbani kwa Mathew na kuingia ndani.
“ Vipi hali ya mgonjwa? Mathew akauliza
“ Amepoteza fahamu tena” akasema Daktari.Eva akamuangalia Mathew kwa jicho la ukali.
“ Vipimo vinaonyeshaje?
“ Mapigo ya moyo yako juu sana isivyo kawaida na hii ni hatari sana” akasema daktari
“ Dr Evarist can we save her” akauliza eva
“ yes we stili have a chance lakini si hapa inabidi tumkimbize hospitali” akasema Dr Evarist
“ Lets go,we’re getting gher out of here” akasema Eva.Daktari akamgeukia Mathew akamtazama kana kwamba alikuwa anataka asike naye anasema nini
“ yah you can get her out of here” akasema Mathew na kusaidiana na Daktari wakambeba Sabina wakamuingiza katika gari ,Mathew akamuamuru yule msichana mwingine aliyekuwa mtumishi wa ndani aongozane na akina Eva kwani hakuwa akimuhitaji tena
“ Noah karudi ? akauliza Mathew
“ Hapana bado.Inawezekana kuna mahala wamepita” akasema Anitha
“ Ok good muache asafishe macho na yule jamaa mwingine anaendeleaje?
“ Amepewa dawa amelala”
“ Ok good.Kuna taarifa nyingine umezipata kuhusia na Habib?
“ bado ninaendelea kutafuta taarifa zake lakini hakuna taarifa zozote mbaya za kumuhusu yeye.Taarifa zake nyingi ni za utumiaji mbaya wa fedha ” Akasema Anitha
“ Ok keep searching.”akasema mathew
“Mmefanikiwa kupata kitu gani huko mlikotoka? Akauliza Anitha.Mathew akakitoa kile kiboksi katika ule mfuko akakiweka mezani
“A box? Anitha naye akashangaa
“Ndiyo ni huu mzigo ambao Sabina aliuficha kwa bibi yake
“ Watu wote hawa wamekufa kwa sababu ya hiki kiboksi? Akauliza Anitha
“ Hata mimi nilistuka kidogo lakini ngoja kwanza tukifungue tujue ndani yake kuna nini” akasema Mathew na kutoka ,halafu akarejea na kifaa cha kukatia chuma na kuanza kukikata kile kiboksi kwa kuwa hawakuwa na funguo.

KIBOKSI AMBACHO KIMESABABISHA UHAI WA WATU ZAIDI YA WATANO KUPOTEA KIMETUA MIKONONI MWA MATHEW.KUNA NINI NDANI YAKE? JAJI ELIBARIKI YUKO WAPI?
 
SEASON 2


SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

“ Noah karudi ? akauliza Mathew

“ Hapana bado.Inawezekana kuna mahala wamepita” akasema Anitha

“ Ok good muache asafishe macho na yule jamaa mwingine anaendeleaje?

“ Amepewa dawa amelala”

“ Ok good.Kuna taarifa nyingine umezipata kuhusia na Habib?

“ bado ninaendelea kutafuta taarifa zake lakini hakuna taarifa zozote mbaya za kumuhusu yeye.Taarifa zake nyingi ni za utumiaji mbaya wa fedha ” Akasema Anitha
“ Ok keep searching.”akasema mathew
“Mmefanikiwa kupata kitu gani huko mlikotoka? Akauliza Anitha.Mathew akakitoa kile kiboksi katika ule mfuko akakiweka mezani
“A box? Anitha naye akashangaa
“Ndiyo ni huu mzigo ambao Sabina aliuficha kwa bibi yake

“ Watu wote hawa wamekufa kwa sababu ya hiki kiboksi? Akauliza Anitha

“ Hata mimi nilistuka kidogo lakini ngoja kwanza tukifungue tujue ndani yake kuna nini” akasema Mathew na kutoka ,halafu akarejea na kifaa cha kukatia chuma na kuanza kukikata kile kiboksi kwa kuwa hawakuwa na funguo.


ENDELEA……………………………….

Mahew na Anitha wote walionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kufahamu ndani ya kile kiboksi kulikuwa na kitu gani.Alikikata kiungalifu sana ili asije haribu kilichokuwamo mle ndani.Baada ya kufanikiwa kukifungua wote wakapigwa na mshangao kwa walichokikuta ndani.Kulikuwa na bahasha.Akaitoa bahasha ile na kufungua ndani yake kulikuwa na karatasi nne ambazo zilionekana kuchorwa chorwa vitu kama vya kisayansi .Mathew na Anitha wakabaki wanaangaliana.

“ So what’s this? Akauliza Anitha baada ya kuziangalia karatasi zile na kushindwa kufahamu kilichokuwa kimeandikwa
“ Hata mimi sifahamu ni kitu gani hiki” akasema Mathew halafu akachukua tena zile karatasi akaanza kuziangalia

“ Zinaonekana ni kama formula za kisayansi lakini sina uhakika.” Akasema Mathew
“ Kwa hiyo listi yote ile ya watu wamekufa kwa sababu ya karatasi hizi? Akauliza Anitha
“Inashangaza sana lakini nina hakika lazima kuna kitu ndani ya karatasi hizi ambacho hatukifahamu na ndiyo maana kukawa na mlolongo wa vifo” akasema Mathew

“ Mathew nataka kukubaliana na wewe lakini ninasita.Ninahisi kuna kitu kingine walichokuwa wanahitaji kukiuza na si hizi karatasi.Hainiingii akilini kabisa kwamba karatasi hizi zisababishe idadi ile watu kuuawa.Edson,mpenzi wake brigita,mzee Matiku,mzee KItwana wote hawa wamekufa kwa sababu ya hizi karatasi? Ninahisi bado kuna kitu kingine kimefichwa ambacho tunatakiwa tukipate.” Akasema Anitha

“ Anitha mzigo huu tumeutoa kwa bibi yake Sabina ambao alikuwa ameuficha mbali.Sabina alipewa mzigo huu na mzee Kitwana kwamba aufiche.Nina hakika kuna kitu ndani ya karatasi hizi ambacho tunatakiwa tukifahamu.Usikate tama mapema” akasema Mathew
“Mathew una hakika kwamba hakuna kitu kingine tofauti na hizi karatasi? Unajua hainiingii akilini eti watu wote wale wafe kwa sababu tu ya hizi karatasi.Na ukumbuke kwamba hii ilikuwa ni biashara ambayo ilitakiwa kuwapatia watu hawa wote mamilioni ya fedha sasa ninashindwa kuamini kama karatasi hizi ndizo zingewaingizia watu wale millions of money.I think there is something else” akasema Anitha

“ Anitha Karatasi hizi ziliibwa toka ikulu na Edson na walipanga waziuze kwa mamilioni ya fedha kwa Habib Soud ambaye nilikwambia utafute taarifa zake .Kama ni hivyo lazima karatasi hizi zina kitu kizito ndani yake.Karatasi kama hivi kuuzwa kwa mamilioni ya fedha si kitu rahisi ,kwa hiyo basi tunachitakiwa kukifanya kwa sasa ni kujaribu kufahamu karatasi hizi ni za nini na umuhimu wake.” Akasema Mathew
“ Nani ambaye atatueleza kuhusiana na karatasi hizi? Mbona maandishi yake ni ya ajabu ajabu tu? Akauliza Anitha
“ Karatasi hizi zimeibwa toka ikulu na ili kufahamu ni za nini tunatakiwa kumpata mtu toka ndani ya Ikulu ambaye anaweza akatueleza kuhusu nini kilichomo ndani ya karatasi hizi.Zimeandikwa kisayansi sana na sisi si wanasayansi.Hakuna chochote tunachoweza kuambua ndani ya karatasi hizi” Akasema Mathew
“ Ni nani ndani ya ikulu ambaye anaweza akatusaidia Mathew? Huoni kwa kufanya hivyo tunaweza kuwa tunajitafutia matatizo mengine kwa sababu karatasi hizi zimeibwa toka ikulu?” Akasema Anitha.Mathew akafikiri kwa muda halafu akasema

“ Mr President”
“ President? Anitha akashangaa

“ Ndiyo ,tukimfuata na karatasi hizi anaweza akatusaidia kufahamu kilichomo ndani yake na umuhimu wake na kwa nini ziliibwa na kutaka kuuzwa kwa mamilioni ya fedha.Kama zimetoka ndaniya ikulu basi lazima atakuwa anafahamu ni za nini.Hakuna mwingine tunayeweza kumuanini zaidi yake” akasema Mathew

“ Kwa hiyo tutamueleza ukweli sisi ni akina nani ? akaulzia Anitha
“ Kama tubna nyaraka kama hii lazima tumueleze ukweli ili atuamini”
“ How can we meet with President? Akauliza Anitha
“ Through Elibariki.Yeye ni mkwe wake na atatusaidia sisi kuweza kuonana naye kwa urahisi.Jambo hili si la kuchelewa tunatakiwa tulifahamu vizuri na kwa haraka “ akasema Mathew na kuchukua simu yake akazitafuta namba za jaji Elibariki akapiga lakini simu ya jaji Elibariki haikuwa ikipatikana

“ Elibariki yuko wapi? Kwa nini ameizima simu yake? Akauliza Mathew

“ Nilikwambia yawezekana Noah akawa amemshawishi wakapitia sehemu Fulani kupooza koo si unajua tena Noah anavyopenda starehe” akasema Anitha

“ Ok ngoja tuwasubiri lakini ingekuwa vyema kama angewahi kuja ili tuweze kuongea naye kuhusiana na suala hili na atusadie kuweza kulipatia ufumbuzi ” Akasema Mathew na kuzishika tena zile karatasi akaanza kuziangalia

“ Dah ! pamoja na ufahamu wangu wa vitu vingi lakini kwa hili nimegonga mwamba.Nimeshindwa kuambua kitu chochote hapa.Namna vitu vilivyoandikwa andikwa inachanganya sana.” Akasema Mathew
“ Mathew unadhani labda inawezekana kuna kitu kinafichwa ndani ya maandishi haya ili kisijulikane? Yawezekana ni siri Fulani?
“ Kwa namna nilivyoziona hizi ni formula za kisayansi.Kuna mahesabu mengi ya kisayansi humu ndani kwa hiyo inatakiwa tumpate mtu ambaye anaweza akatufafanulia kuhusiana na formula hizi.Usijali Anitha tutafahamu tu ni kitu gani lakini lazima tujue kwamba kilichomo ndani ya karatasi hizi ni kitu kikubwa na ndiyo maana kimegharimu uhai wa watu.Na hata hivyo tunatak…………….” Mathew akakatishwa na simu yake ya mkononi iliyokuwa ikiita.Alikuwa ni Jason

“ Hallo Jason” akasema Mathew
“Mathew samahani kwa kuwasumbua mida hii lakini nataka kuwahamisha kuhusiana na shambulio lililotokea usiku huu”

“ Shambulio ? Mathew akastuka

“ Shambulio gani Jason?

“ Ina maana hamjapata taarifa zozote za kuhusiana na shambulio lililotokea? Akauliza Jason

“ Hapana hatuna taarifa zozote.Ni shambulio gani? akauliza Mathew kwa mshangao

“ Gari la jaji Elibariki limeshambuliwa na watu wasiojulikana usiku huu na inasemekana kuna tu ameuawa” akasema Jason.Taarifa zile zikamstua mno Mathew

“ Shambulio hilo limetokea saa ngapi?
“ Usiku huu Mathew na inasemekana kuna mtu mmoja ameuawa katika shambulio hilo”
“ Ouh my God ! “ akasema Mathew na kushindwa la kusema .Midomo yake ilikuwa inamcheza.

“ What happened Mathew? Akauliza Anitha.Mathew akashinda kuongea
“ C’mon Mathew tell me what happened? Akauliza Anitha

“ Elibariki ameshambuliwa na watu wasiojulikana” akasema Mathew huku sauti ikimtetemeka

“ Don’t tell me he’s dead” akasema Anitha na macho yake yalishindwa kuonyesha mstuko aliokuwa ameupata
“ Jason ! akaita Mathew
“ Mtu aliyekutwa amekufa ndani ya gari ni jaji Elibariki au ni nani ? Kwa sababu Elibariki alikuwa ameongozana na Noah usiku huu” Akauliza Mathew

“ Alikuwa na Noah? Akauliza Jason
“ Ndiyo alikuwa na Noah “ akajibu Mathew

“Mpaka sasa hakuna taarifa kamili kwamba aliyekutwa amekufa ndani ya gari hilo ni nani lakini taarifa zinadai kwamba ni mtu mmojandiye aliyekutwa amekufa.Hivi sasa ninaelekea katika hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kwenda kumtambua kama ni Elibariki ama vipi.” Akasema Mathew
“Jason ahsante sana hata sisi tunaelekea huko sasa hivi” akasema Mathew na kukata simu.Alihisi mwili wake kukosa nguvu
“ Jason anasemaje? Akauliza Anitha

“ Hakuna mpaka sasa taarifa kamili iliyotoka kama aliyekufa ni jaji Elibariki ama si yeye.Kwa sasa Jason anaelekea hospitali kuu ya Taifa ili kwenda kuutambua mwili wa mtu huyo aliyekutwa amekufa ndani ya gari la jaji Elibariki” akasema Mathew

“ Mathew I’m so scared.Elibariki alikuwa na Noah ndani ya gari.Una hakika Noah yuko salama? Akauliza Anitha

“ Siwezi kuwa na uhakika kama aliyefariki takuwa nani lakini lazima tujiandae kwa lolote.Tunaelekea hospitali tukathibitishe.” Akasema Mathew na kuingia chumbani kwake akabadili mavazi halafu wakaingia garini na kuanza safari ya kuelekea hospitali kuu ya taifa kwa ajili ya kwenda kuutambua mwili wa mtu aliyeuaa kwa risasi ndani ya gari la jaji Elibariki.
“ Mathew unadhani ni nani ambaye anaweza kuwa amefanya shambulio hili ? Akauliza Anitha kwa sauti yenye kitetemeshi.

“ hapana siwezi kujua kwa sasa.Ni vigumu kufahamu kwa sababu majaji huwa ni watu wenye maadui wengi.Inawezekana wakawa ni watu ambao hawakuridhishwa na mojawapo ya maamuzi yake kwa hiyo wakaamua kulipiza kisasi.”akasema Mathew ambaye alionekana kuwa na mawazo mengi sana.Anitha alikuwa ameifunga mikono yake na kuiweka kifuani akiomba kimoyo moyo.
“Mungu wangu ninaomba Noah awe mzima kwa sababu naye alikuwamo ndani ya gari la jaji Elibariki.”
Waliwasili katika hospitali kuu ya taifa na kuelekea moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti .Nje ya jengo lile wakakutana na Jason ambaye tayari alikwisha fika
“ Jason tupe taarifa.Umefanikiwa kumtambua mtu huyo? Akauliza Mathew

“ Nimefanikiwa kumuona lakini si jaji Elibariki..” akasema Jason na huku akionekana kuogopa .Anitha alikuwa ameiweka mikono kichwani aliogopa sana.Mathew Anitha na Jason wakaingia ndani ya chumba cha maiti kwa ajili ya kuitambua maiti ya mtu Yule.Anitha akaanguka na kupoteza fahamu baada ya kugunudua kwamba mtu Yule aliyekuwa amefariki ni Noah.Mathew na Jason wakisaidiana na watu wengine waliokuwapo pale wakambeba na kumtoa nje kwa ajili ya kumsadia ili aweze kurejewa na fahamu zake.Alipatwa na mstuko mkubwa sana.Wakati Anitha akiendelea kupatiwa huduma ya kwanza Mathew alisogea pembeni akatoa kitambaa na kujifuta machozi.Aliumizwa sana na tukio lile.

“ Ni nani lakini aliyefanya jambo kama hili? Ni nani aliyemuua Noah? Akajiuliza huku machozi yakiendelea kumtoka

“ Masikini Noah amekufa bado kijana mdogo tu.Nitawaeleza nini familia yake? Bado Mathew aliendelea kuangusha machozi na mara akashikwa bega na Jason

“ Mathew ,Anitha ameamka” akasema Jason

“Jason I’m deeply hurt.Sijawahi kuumia namna hii kwa miaka mingi.Machozi ya mwisho niliyatoa wakati familia yangu ilipoteketea kwa moto lakini leo nimeshindwa kujizuia na kuangusha machozi.Nimeumia sana Jason kwa kifo hiki cha Noah.Nimemfahamu Noah kwa muda mrefu na ni mimi niliyemjenga hadi hapa alipofika.Nilimuita aje anisaidie katika kazi mliyotukabnidhiya kumtafuta muuaji wa Edson na sikjua kama nilikuwa namuita aje kufa.Laiti kama ningejua kijana Yule anakuja kufa wala nisingemuita aje anisaidie kazi” akasema Mathew na kushindwa kujizuia kudondosha chozi

“ Pole sana Mathew.Pole sana” akasema Jason

“ Ahsante sana Jason.Japokuwa kifo tumeumbiwa wanadamu lakini kwa kweli nimeumizwa mno na mauaji haya ya kikatili ya Noah.Sikutegenmea hata siku moja kama Noah angeweza kuawa kikatili namna hii” akasema Mathew kwa ucungu

“ Ilikuwaje Noah akawa katika gari la jaji Elibariki? Akauliza Jason.Mathew akafuta machozi na kusema
“ Noah alikuwa anajeraha katika mguu wake kwa hiyo tulimuacha nyumbani wakati sisi tukielekea katika kazi Fulani usiku huu.Wakati hatupo alifika Elibariki kwa kuwa nilihitaji kuonana naye usiku wa leo.Aliponikosa aliamua kuondoka na kwenda kuonana na mke wake halafu arejee.Alinipiga simu na kunitaarifu kwamba atarejea baada ya muda na anaongozana na Noah ambaye alisema kwamba anataka kwenda kuufanyisha mazoezi mguu wake na alikuwa ameboreka pale ndani peke yake.Ningejua kama anakwenda kufa wala nisingemruhusu aondoke pale nyumbani” akasema Mathew na kufuta machozi.Kikapita kimya cha sekunde kadhaa Jason akauliza

“ Jaji Elibariki yuko wapi? Si umesema kwamba walikuwa wote ndani ya gari? Akauliza Jason
“ Ni kweli walikuwa wote ndani ya gari lakini hata mimi sifahamu Elibariki yuko wapi “ akasema Mathew

“ Hili ni jambo la kushangaza sana kama walikua wote garini yeye yuko wapi? Kwa nini afariki Noah peke yake? Ina maana wakati shambulio hilo linafanyika Elibariki hakuwamo garini? Akauliza Jason

“ Jason jambo hili linashangaza sana.Hata mimi nashindwa kuelewa kwamba ndani ya hilo gari alikuwepo Noah peke yake? Kuna maswali mengi ya kujiuliza hapa lakini kwa sasa inatubidi tuachane kwanza na hayo ili tushughulikie suala la msiba wa Noah.Siwezi kufanya jambo lolote kwa sasa hadi kwanza akili yangu itakapotulia .Elibariki yuko wapi ,amekufa ama hajafa ni suala ambalo nitalishughulikia baadae.” Akasema Mathew ambaye ni wazi alionekana kuchanganyikiwa
“Sawa Mathew ,basi tuanze taratibu zinazotakiwa ili tuweze kukabidhiwa mwili wa Noah.Niachie mimi nitalishughulikia suala hili .Kwani Noah ni mtu wa wapi? Ndugu zake wako wapi?

“Kwa sasa familia yake inaishi jijini Harare Zimbabwe.Mama yake ni mtanzania na baba yake ni raia wa Zimbabwe.Nitafanya utaratibu wa kuwasiliana na familia yake na kuwataarifu kuhusiana na msiba huu na kwa pamoja tujadiliane namna ya kufanya kama Noah azikwe hapa Tanzania au asafiriswe kwenda Zimbabwe.” akasema Mathew

“ Sawa Mathew mimi nitalishughulikia suala hilo .Kwa sasa unaweza kwenda kupumzika mimi nitalishuhulikia jambo hili kwa sababu lina taratibu zake na nitakupa majibu kesho asubuhi.” Akasema Jason .
Tayari Anitha alikwisha rejewa na fahamu zake lakini hakuwa na nguvu kabisa.Machozi mengi yalikuwa yanamtoka.Jason akamshika mkono akamsaidia kutembea hadi katika gari akiwa ameongozana na Mathew
“ Mathew are you sure you can drive? Akauliza Jason
“ Yes I can.Shughulikia suala hilo na nitakufahamisha baada ya kuwasiliana na familia ya Noah” akasema Mathew na kuwasha gari kisha wakaondoka.Anitha alikuwa ameinama akilia.Mathew naye alikuwa akiendesha gari huku machozi yakimtiririka.Kifo cha Noah kilimuumiza sana.
Walifika numbani na Anitha akajitupa sofani akaendelea kulia

“ Anitha najua ni kwa namna gani kifo cha Noah kimekuumiza,hata mimi nimeumia sana na siwezi kueleza ni kwa namna gani ninaumia moyoni lakini pamoja na maumivu yote tuliyonayo kwa sasa tunatakiwa tusimame imara katika suala hili hadi hapo tutakapo hakikisha kwamba Noah amepumzishwa.Sisi ndiyo ndugu zake wa karibu na tunatakiwa tuwe na nguvu na ujasiri tuubebe msiba huu hadi mwisho .Tafadhali Anitha nakuhitaji sana katika hili.Nahitaji sana ushirikiano wako” akasema Mathew

“ Mathew I’m sorry I cant…Ninashindwa kabisa kujizuia kulia.NImeumia sana..Ouh Noah !..Anitha akashindwa kujiuzia na kuangua kilio.Mathew akamfuata akamkumbatia na kumfuta machozi.

“ We need to be strong for him” akasema Mathew halafu akainuka na kwenda chumbani kwake akakaa kitandani nz kuanza kulia.Baada ya kama dakika kumi hivi za kulia akainuka na kujifuta machozi halafu akafungua kabati lake na kutoa kitabu Fulani ambacho huwa anaandika kumbu kumbu kadhaa.Akazitafuta namba Fulani akaziandika katika simu yake na kupiga lakini namba zile hazikuwa zikipatikana.Akaandika tena namba nyingine na kupiga.Simu ikaanza kuita.Mathew alikuwa anampigia simu dada wa Noah anayefanya kazi katika benki moja nchini Zimbabwe.Baada ya kuzipata taarifa zile dada wa Noah akaumuunganisha Mathew na wazazi wake akawataarifu kuhusiana na kilichotokea.Kila aliyeipata taarifa ile alipatwa na mstuko mkubwa sana.Baba wa Noah akamuahidi Mathew kumpigia simu asubuhi ili kumtaarifu ni kitu gani watakuwa wameamua kuhusiana na mazishi ya mtoto wao
Mathew alikaa tena kitandani an kukumbuka mbali sana toka alipokutana na Noah na kujenga urafiki na hatimaye akamtoa katika kazi aliyokuwa anaifanya na kumuingiza katika kufanya kazi binafsi na ambazo zilimletea mafanikio makubwa .

“ Alikuwa ni kijana mchapa kazi na ambaye alikuwa uwezo ajabu.Nimekwisha fanya naye kazi nyingi na kila kazi niliyofanya naye ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Yeye na Anitha hawakuwa tu ni marafiki zangu bali ndugu zangu” akawaza Mathew
“ Yeyote aliyefanya kitendo hiki nitamtafuta hadi nimpate.Kila risasi iliyoingia mwilini mwa Noah haitakwenda bure lazima itaondoka na mtu. I swear in heaven and earth yeyote aliyefanya ukatili huu hawezi kujificha sehemu yoyote nisimtambua.Nitawasaka kila mahala na nitawapata.” Akawaza Mathew akiwa na hasira kali

*******


Mwili wa jaji Elibariki ulikuwa umeloa damu na alikuwa na jeraha katika mkono wake wa kulia lililokua linatoa damu.Alikuwa amekaa ndani ya gari huku pembeni yake kukiwa na mwanamke aliyekuwa anaendesha gari kwa umahiri mkubwa sana.Mwili wote bado ulikuwa unamteteteka.Alikumbuka kilichotokea muda mfupi uliopita akaogopa sana.

“ Wamemuua Noah !! akawaza huku machzi yakimtoka
“ Ni akina nani wale waliofanya kitendo kile cha kinyama? Nilifanya kosa kubwa sana kulipuuza onyo lile nililopewa na Yule mwanamke aliyenipigia simu na kunitaka nisiingie katika gari.Inaonekana kuna mpango ulikuwa umekwisha pangwa ili niuawe.Lakini kwa nini watake kuniua? Ni nani wanaotaka kuniua? Mwanamke Yule aliyenipigia simu na kunipa onyo ni nani? Ni huyu pembeni yangu ama ni nani? Huyu mwanamke naye ni nani? Amenifahamuje? Mbona mimi simfahamu? Ananipeleka wapi? Akajiuliza Jaji Elibariki maswali mfululizo bila kupata majibu
“Mpaka sasa hivi sifahamu nimeponaje katika lile shambulio.Dah ! Toka nimezaliwa sijawahi kushuhudia shambulio baya kama lile.Risasi zilikuwa zinavuma kama vitani.Nimeponyoka toka mdomoni mwa kifo.” Akawaza Jaji Elibariki na kuvuta kumbu kumbu kuhusiana na namna tukio lile llilivyotokea.Alikumbuka namna Noah alivyoruka na kumkinga na risasi akaumia sana na machozi yakamtoka
“ Noah aliniokoa.Bila yeye hivi sasa ningekuwa tayari marehemu.Shambulio lile lilinilenga mimi na amekufa kifo nilichostahili kufa mimi.Ninaamini haikuwa ni mipango ya Mungu nifariki leo.Nadhani Mungu ana makusudi yake kwa nini nimepona leo hii.” Akawaza Jaji Elibariki halafu akajaribu kunyoosha mkono akagugumia kwa maumvu makali

“ Elibariki ! akaita Yule mwanamke ambaye alikuwa makini sana katika usukani.Elibariki akageuza shingo na kumtazama.Hakuwa na kumbu kumbu kama amewahi kumuona sehemu mwanamke sehemu yoyote.
“Unajisikiaje? Akauliza Yule mwanamke

“ Sijielewi elewi bado.I feel like I’m dead” akasema Elibariki na Yule mwanamke akatabsamu na kusema

“ You are not dead Elibarki .You are alive.Kuna sehemu yoyote umeumia? Akauliza

“ Ninasikia maumivu makali hapa katika mkono wa kulia na chini ya mguu wa kushoto” akasema Elibariki

“ Pole sana.” Akasema Yule mwanamke

“ Wewe ni nani? Akauliza Elibariki.Yule mwanamke akatabasamu na kusema

“ Mtu ambaye hupaswi kumfahamu”

“ Mtu ambaye sipaswi kukufahamu? Una maana gani kusema hivyo? Wewe ndiye uliyenipigia simu? Akauliza Elibariki
“ Elibariki kitu cha msingi cha kushukuru kwa sasa ni kwamba uko salama.”

“ Nani waliotaka kuniua? Unawafahamu? Akauliza jaji Elibariki

“ Elibariki huu si muda wa maswali mengi” akasema Yule mwanamama.Elibariki akakaa kimya kidogo halafu akauliza

“ Unanipeleka wapi?
“ Somewhere safe.Kuna sehemu yoyote ambayo unahisi inaweza kuwa salama kwa sasa kwa wewe kwenda kujificha? Kwa sababu hutakiwi kabisa kuonekana.”Akauliza Yule mwanamama.Jaji Elibariki akafikiri kwa muda halafu akasema

“ Ndiyo”

“ Ni wapi nikupeleke ? Akauliza Yule mwanamke

“ Kwa rafiki yangu”
“ Unafahamu anakokaa? Akauliza
“ Ndiyo ninapafahamu”

“ Unazifahamu namba zake za simu kwa kichwa ? kwa sababu sitaki uwashe simu yako” Akauliza

“ Ninazikumbuka “ akasema jaji Elibariki na kumtajia Yule mwanamke akaziandika katika simu yake akapiga na simu ikaanza kuita
“ Hallow” akasema Yule mwanamke baada ya simu kupokelewa

“ Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili

“ Samahani ninaongea na nani?
“ Unaongea na Peniela” ikasema sauti ya upande wa pili.Yule mwanamke akamgeukia jaji Elibariki
“ Anasema anaitwa Peniela ndiye rafiki yako? Akauliza

“ Ndiyo”

“ Do you trust her? Akauliza tena
“ Ndiyo ninamuamini sana” akasema jaji Elibariki

“ Ok ongea naye” akasema Yule mwanamke na kumpatia Elibariki simu
“ Hallow Peniela Elibariki hapa ninaongea”
“Elibariki?

“Ndiyo ni mimi?

“ Mbona unanishangaza Elibariki? Mbona unanipigia kwa kutumia simu nyingine? Uko wapi ? Uko na nani?
“ Niko katika gari na ….” Elibariki akasita.Yule mwanamke aliyekuwa akiendesha gari akaachia usukani wa gari na kumnyang’anya Elibariki simu
“ Hallow Peniela.Una gari? Akauliza
“ Ndiyo ninalo”

“ Ok vizuri basi washa gari lako sasa hivi na uje pale Kisulo restaurant uje umchukue rafiki yako .He’s in trouble na anahitaji sehemu salama.Tafadhali usimwambie mtu yeyote kuhusiana na jambo hilina uwe na uhakika hakuna mtu anayekufuatilia” Akasema Yule mwanamke na kukata simu.



KARATASI WALIZOZPATA AKINA MATHEW ZIMEANDIKWA KITU GANI? MWANAMKE ALIYEMUOKOA JAJI ELIBARIKI NI NANi? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
EASO 2
SEHEMU YA 13
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Unaongea na Peniela” ikasema sauti ya upande wa pili.Yule mwanamke akamgeukia jaji Elibariki
“ Anasema anaitwa Peniela ndiye rafiki yako? Akauliza
“ Ndiyo”
“ Do you trust her? Akauliza tena
“ Ndiyo ninamuamini sana” akasema jaji Elibariki
“ Ok ongea naye” akasema Yule mwanamke na kumpatia Elibariki simu
“ Hallow Peniela Elibariki hapa ninaongea”
“Elibariki?
“Ndiyo ni mimi?
“ Mbona unanishangaza Elibariki? Mbona unanipigia kwa kutumia simu nyingine? Uko wapi ? Uko na nani?
“ Niko katika gari na ….” Elibariki akasita.Yule mwanamke aliyekuwa akiendesha gari akaachia usukani wa gari na kumnyang’anya Elibariki simu
“ Hallow Peniela.Una gari? Akauliza
“ Ndiyo ninalo”
“ Ok vizuri basi washa gari lako sasa hivi na uje pale Kisulo restaurant uje umchukue rafiki yako .He’s in trouble na anahitaji sehemu salama.Tafadhali usimwambie mtu yeyote kuhusiana na jambo hilina uwe na uhakika hakuna mtu anayekufuatilia” Akasema Yule mwanamke na kukata simu.

ENDELEA…………………
Kisulo Restaurant ni moja ya hoteli kubwa na nzuri jijini Dar es salaam ambayo kwa masaa yote huwa imejaa watu kutokana na huduma nzuri wanazozitoa pamoja na chakula kizuri kinachopika hapa.Kila aina ya chakula unachokihitaji basi unaweza ukakipata hapa.Eneo la maegesho la hoteli hii ni kubwa kutokana na idadi kubwa ya watu wanaofika hapa.Gari alilokuwa amepanda jaji Elibariki lililokuwa linaendehshwa na mwanamke ambaye hakumfahamu lilivuka hoteli kidogo na kwenda kusimama mbele yake,yule mwanamke akalizima akatoa bastora yake na kuiweka tayari.Alikuwa na wasiwasi sana yawezekana walikuwa wakifuatiliwa.
“Peniela ! do you trust her? Akarudia tena kuuliza yule mwanamke
“ Yes I do “ akasema Jaji Elibariki
“ kwa nini unaniuliza hivyo? Akaulizia
‘ Ninakuuliza hivyo kwa sababu maisha yako ya sasa hivi yanategemea sana watu unaowaamini.” Akasema yule mwanamke
“ kwani wewe ni nani? Umenifahamuje? Kwa nini umeniokoa? Unawafahamu waliotaka kuniua? Akauliza jaji Elibariki
“ Eliariki nimekwisha kwambia kwamba usitake kunifahamu.Kukuweka sehemu salama ni jukumu langu la kwanza .Nitakutafuta tena baadae.Ila ninachokuonya ni kwamba hutakiwi kabisa kuonekana kwa sasa.Hutakiwi kutoka hadi hapo nitakapokuamuru.” Akasema yule mwanamke.Jaji Elibariki akamtazama na kusema
“ Ninashukuru sana kwa kuniokoa lakini bado ninashauku kubwa ya kutaka kukufahamu wewe ni nani ,na kwa nini umeniokoa? Akauliza .Yule mwanamke hakujibu kitu akatoa simu yake na kuzitafuta namba za simu za Peniela akampigia
“ Hallow Peniela umefika wapi?
“ Nimekaribia sana kufika.” Akajibu Peniela
“ Ok good.Ukifika utalifuata gari Fulani limeegeshwa mbele ya kibanda kile cha kuuza vocha za simu .” akasema Yule mwanamke na kukata simu
“ Elibariki are you sure you’ll be in safe hands? Akauliza yule mwanamke
“ Yes I’m sure” akasema Elibariki
“ Kitu kingine usithubutu kumpigia simu mtu yeyote yule na kumweleza kwamba uko hai na mahala uliko.Si mke wako wala yeyote unayemfahamu mpaka hapo nitakapokuruhusu kufanya hivyo.Tumeelewana Elibariki?
“ Tumeelewana”akajibu jaji Elibariki ambaye bado kila kitu kilichotokea kwake ilikuwa ni kama sinema
“ This woman Peniela ,who is she to you? Akauliza yule mwanamke
“ What ? akauliza jaji Elibariki ambaye alionekana kuwa mbali sana kimawazo
“ nakuuliza huyu Peniela ni nani wako?Ndugu yako,rafiki yako au ni nani wako?
“ Ni rafiki yangu.” Akajibu Jaji Elibariki
“ Unamfahamu? Akauliza jaji Elibariki
“ Hapana simfahamu ila ninahitaji kumfahamu ili nihakikishe kwamba niko katika mikono salama”akasema yule mwanamama
“ Kwa nini umeniokoa? Kwa nini unataka kuhakikisha kwamba niko katika mikono salama? Akauliza jaji Elibariki na mara gari moja ndogo nyeusi ikawapita na kwenda kusimama mbele yao akashuka msichana mmoja ambaye jaji Elibariki akamtambua
“ Thats Peniela” akasema
“ wow she’s so beautiful” akasema yule mwanamke huku akitabasamu na kufungua mlango wa gari akashuka
“ Peniela ! akaita yule mwanamke na Peniela akamsogelea.Alikuwa na wasi wasi mwingi
“ Habari yako” yule mwanamke akamsalimu Peniela
“Nzuri .Elibariki yuko wapi? Is he ok? Akauliza Peniela akiwa na hamu ya kutaka kujua hali ya Elibariki
“ Usihofu Elbariki ni mzima na anaendelea vizuri .Kumefanyika shambulio usiku huu kuna watu waliotaka kumuua lakini nimefanikiwa kumuokoa. Elibariki anatafutwa auawe kwa hiyo anatakiwa apate sehemu ya kujificha hadi hapo mambo yatakapokaa vizuri Kwa sasa wewe pekee ndiye mtu ambaye anakuamini na anaamini katika mikono yako atakuwa salama.”akasema yule mwanamke
“ Ni akina nani wanaotaka kumuua? Akauliza Peniela akiwa na wasi wasi mwingi
“ Ni mapema mno kusema ni akina nani lakini naomba tu ufahamu hilo kwamba roho ya Elibariki inatafutwa kwa gharama yoyote ile kwa hiyo basi hakikisha kwa kila namna utakavyoweza Elibariki anakuwa salama.Muda wowote ule ukihisi hatari yoyote ile utanipigia simu yangu na kunifahamisha na nitakusaidia.”akasema yule mwanamke
“ kwani wewe ni nani? Akauliza Peniela lakini yule mwanamama hakujibu akaufungua mlango wa gari na kumtoa Jaji Elibariki kwa haraka haraka akaingia katika gari la Peniela kisha yule mwanamke akaondoa gari lake kwa kasi.Kwa muda wa sekunde kadhaa jaji Elibariki na Peniela walibaki wanaangaliana.Peniela aliogopa sana kwa namna Elibariki alivyokuwa ameloa damu
“ Pole sana Elibariki” akasema Penny
“ Ahsante sana Penny”
“ Umeumia mahala kokote?akauliza Peniela
“ Nina jereha hapa katika mkono wa kulia nahisi nimekwaruzwa na risasi na katika mguu ninahisi kuna maumivu makali”
“ Pole sana Elibariki.Nani lakini waliofanya kitu hiki? Unaweza kuwafahamu? Akauliza Peniela
“ Hapana Penny siwezi kuwafahamu ni akina nani lakini nia yao ilikuwa ni kuniua” akasema Elibariki.Penny akawasah gari wakaondoka
“ Nani ametaka kumuua Elibariki? Yawezekana akawa ni Jason akitaka kulipiza kisasi ? Ninaanza kuwa na wasi wasi sana yawezekana kabisa akawa ni Jason huyu ndiye aliyepanga njama hizi.Jason alichukia sana siku ile na nilimuona kabisa kwamba alikuwa na dhamira ya kuua na ndiyo maana alimpiga Elibariki na chupa kichwani.Sioni mwingine anayeweza kufanya jambo kama hili zaidi yake.” Akawaza Peniela
“ Kwa mujibu wa yule mwanamke Elibariki yuko katika hatari kubwa sana ya kuuawa.Lazima nitafute sehemu salama ya kwenda kumuweka.Sehemu ipi ni salama zaidi kumuweka kwa sasa?akajiuliza Peny
“Nyumbani kwangu sina hakika kama ni salama na nina ogopa anaweza akajulikana .Katika ile nyumba mpya niliyohamia leo ni sehemu salama na anaweza akaishi pale muda mrefu bila ya mtu yeyote kufahamu lakini tataizo ni kwamba lengo la rais kunitaka nikaishi pale ni ili awe na uwezo wa kufika muda wowote anaotaka .Itakuwaje iwapo atakuja na kumkuta Elibariki yuko pale? Hapana sehemu ile si muafaka kumuweka Elibariki.Itanibidi nimpeleke nyumbani kwangu halafu kesho nitaangalia namna nzuri ya kufanya. Lazima nipate sehemu salama kabisa ya Elibariki kuishi kwa muda wowote anaoutaka” akawaza Peniela
“ Nimefurahi kwa Elibariki kutua tena katika mikono yangu.Nilikuwa naitafuta sana nafasi hii ya kuweza kuutengeneza upya uhusiano wangu na Elibariki.Ni mtu ambaye amenisaida sana katika kuniweka huru .Lazima na mimi nimsaidie katika kipinid hiki ambacho anahitaji sana msaada ” akawaza Peniela na hawakuongea kitu chochote hadi walipofika nyumbani kwake akashuka na kufungua geti akaingiza gari ndani halafu akaufungua mlango wa gereji na kuliingiza gari katika gereji na ndipo alipomruhusu Jaji Elibariki kushuka.Akamsaidia kutembea hadi sebuleni akamkalisha sofani.Bado jeraha alilokuwa amelipata jaji Elibariki katika mkono wake liliendelea kutoa damu.Peniela akaenda chumbani kwake na kurejea na kiboksi chenye vifaa vya huduma ya kwanza na kulisafisha jeraha lile na kisha kupata dawa na kulifunga ili lisiendelee kutoa damu.
“ Pole sana Elibariki,usijali hapa uko sehemu salama na nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba unakuwa salama.Kwa sasa ngoja nizuie hii damu halafu nitamuita daktari atakuja kukuangalia “ akasema Peniela na Elibariki akaonyesha wasi wasi Fulani
“usiogope Elibariki.Daktari huyo ni rafiki yangu mkubwa tumesoma wote toka shule ya msingi “ akasema Peniela.Baada ya kumfunga jeraha lile akamshika mkono na kumuongoza hadi bafuni ambako alimsaidia kuoga halafu akampeleka kitandani .
“ Peniela nashukuru sana “ akasema Jaji Elibariki
“ Usijali Elibariki.Wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu kwa hiyo nitafanya kila linalotakiwa kufanywa kuhakikisha kwamba uko salama.” Akasema Peniela wakatazamana kwa muda halafu Peniela akasema
“ Elibariki ninaomba samahani sana kwa jambo lililotokea siku ile.Ni jambo la aibu sana lakini naomba tusahau yote yaliyotokea.Najua ulikasirika sana kwa tukio lile lakini nina hakika tutakaa na kuliongelea “ akasema Peniela .Jaji Elibariki akatabasamu kidogo na kusema
“Peniela naomba kwa sasa usiwaze kuhusiana na mambo hayo.Yamekwisha pita na kwa sasa tuko katika mambo mengine kabisa.Tushughulike na lili liko mbele yetu yaliyopita yamekwisha pita tusihangaike nayo.Tell me anything and I believe you”akasema jaji Elibariki na kumfanya Peniela atabasamu
“ Nashukuru sana Elibariki.Ngoja kwanza niwasiliane na daktari” akasema Penny na kumpigia daktari rafiki yake waliongea kwa dakika kama mbili hivi halafu akamfuata Elibariki
“ Daktari anakuja muda si mrefu” akasema
“ nashukuru sana Penny.Ahsante sana kwa kunijali ” akasema Elibariki na Penny akatabasamu na kusema
“ Elibariki nilistuka sana uliponipigia simu.Baada ya tuko lile la siku ile nilikuwa naogopa hata kukupigia simu na kukujulia hali yako.Kila nilipotaka kukupigia nilijikuta nikishindwa.Uliponipigia leo nilistuka sana na kujiuliza ni kwa nini mimi? Kwa nini katika watu wote hawa waliokuzunguka ukanichagua mimi? Am I that important to you?akauliza Peniela .Jaji Elibariki akamtazama na kusema
“ Peniela ,jina lako lilikuwa la kwanza kulifikiria mara tu nilipofikiria kama kuna sehemu salama ninaweza kwenda kukaa kwa usiku huu.Sikuwaza mtu mwingine yeyote zaidi yako kwa hiyo nina amini kwamba hapa niko sehemu sahihi “ akasema jaji Elibariki.
“ Mkeo ana taarifa ya kilichotokea? Akauliza Peniela
“ Nina hakika lazima atakuwa na taarifa mpaka hivi sasa.Siku hizi taarifa hazichelewi kusambaa.Nina hakika baada ya kuzipata taarifa hizi atakuwa katika wakati mgumu sana ”
“ Elibariki najua bado uko katika mstuko lakini unaweza ukanieleza hasa nini kilitokea? Akaulizia Peniela
Jaji Elibariki akafumba macho na kuvuta picha ya tukio lile kisha akasema
“ Usiku huu mke wangu alinipigia simu na kunitaka niende nikaonane naye kuna suala ambalo alitaka kunieleza.Siwezi kukuficha Peny kwa siku za hivi karibuni mimi na mke wangu tumekuwa katika mikwaruzano kidogo.Hata usiku huu tulipoonana tulishindwa kuelewana ikanilazimu kuondoka kwani nilikuwa na miadi ya kuonana na rafiki yangu mmoja anaitwa Mathew.Kabla sijafungua mlango wa gari langu nilipigiwa simu na mtu ambaye simfahamu.Alikuwa ni mwanamke na akaniambia kwamba nisiingie katika gari.Nikamuuliza yeye ni Nani na kwa nini nisiingie katika gari langu akaniambia kwamba kuna mpango wa kuniua.Nikampuuza na kuingia garini.Nilikuwa na mtu mmoja anaitwa Noah ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari langu usiku huu.Tuliendelea na safari hadi tulipofika katika makutano ya barabara za Mkwavinyika na Kilimanjaro pale kwenye taa za kuongozea magari tukakuta kuna msururu mrefu wa magari.Wakati tukisubiri taa ziwake ghafla zilitokea piki piki mbili na kuanza kutuvurumishia risasi.Yule jamaa niliyekuwa naye garini Noah aliniwahi na kunikinga na zile risasi zikampata yeye na kumuua pale pale.Bila Noah hivi sasa tayari ningekuwa nimekufa.Alijitolea hai wake kwa ajili yangu” akasema jaji Elibariki
“ Pole sana Elibariki.Pole sana” akasema Peniela na kumfuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.
“ Ahsante sana Peniela.”
“ Lakini ni akina nani waliotaka kufanya jambo hili? Ni kwa nini walitaka kukuua? Akauliza Peniela huku naye machozi yakimtoka
“ Sifahamu Peniela.Sifahamu ni akina nani wanaoitafuta roho yangu .Kwa sasa baada ya kunusurika inanibidi nichukue tahadhari kubwa sana kwani watu hawa wakijua wamenikosa hawatalala usingizi wataendelea kunisaka usiku na mchana hadi wahakikishe wametimiza lengo lao.lakini nakuhkikishia Peniela kwamba lazima watu hawa watapatikana tu” ” akasema jaji Elibariki na Kengele ya getini ikalia kuashiria kwamba kuna mtu.
“Huyo atakuwa ni daktari wangu” akasema Peniela na kuinuka akaelekea getini.Ni kweli alikuwa ni daktari aliyemuita Dr Jonesia.Peniela akampokea na kumpeleka moja kwa moja hadi chumbani kwake ambako alikuwepo jaji Elibariki.Dr Jonesia akasalimiana na jaji Elibariki halafu akaanza kumuangalia mahala alikoumia.Alimchunguza kwa muda wa kama nusu saa hivi kila sehemu ya mwili ambayo kulionekana kuwa na damu halafu akasema
“ Mungu ni mkubwa majeraha haya yote ni ya michubuko tu na hakuna risasi hata moja iliyoingia mwilini mwake” akasema Dr Jonesia na kuyatibu majeraha yote ya jaji Elibariki halafu akamchoma sindano na kumtaka apumzike.Peniela akamshukuru na kumsindikiza akaondoka
“ Peniela nashukuru tena kwa mara nyingine kwa msaada wako .Kama nilivyosema awali kwamba sikukosea kabisa kuja hapa.Ninaamini nimefika sehemu sahihi ninakotakiwa kuwapo kwa sasa”akasema jaji Elibariki na Penny akatabasamu kidogo
“Usijali Elibariki nitafanya kila linalowezekana kwa ajili yako “ akasema Peniela na mara simu ambayo huwa anaitumia kuwasiliana na Dr Joshua ikaita
“ Sorry Elibariki I need to take this call in Private .Its important’akasema Peniela na kuichukua simu ile akatoka mle chumbani
“hallow Dr Joshua’akasemaPeniela
“hallow Peniela,hujambo? habari za makazi mapya? Kareem aliniambia kwamba ila kitu kimekwenda vizuri kama ulivyotaka”
“Ndiyo Dr Joshua kila kitu kimekwenda vizuri na ninashukuru sana.Vipi wewe unaendeleaje? Akauliza Penny
“Hata mimi ninaendlea vizuri sana Penielea.Leo tulikuwa na zoezi la kuuaga mwili wa Flora na kesho tunalekea kijijini alikozaliwa kwa ajili ya mazishi.”
“ Pole sana Dr Joshua.” Akasema Peniela
‘ Ahsante sana Peniela.lakini yote hii ni mipango ya Mungu .Yeye ndiye mwenye kupanga mambo yote yatokee na hata kwa hili ana makusudi yake kwa nini litokee sasa.Nadhani ana mpango mkubwa wa nchi kumpata first lady mpya” akasema Dr Joshua huku akicheka kidogo
“Dr Joshua achana na mawazo hayo kwanza.Subiri kwanza hadi mkeo atakapozikwa”
“ Hahaha Peniela unanifurahisha sana,Flora is gone and she’ll never come back.Maisha lazima yaendelee “akasema Dr Joshua akatulia kidogo halafu akaendelea
“ Peniela nimekupiga simu kukutakia tu usiku mwema na kukumbusha ni namna gani ninavyokupenda.Endapo kama kusingekuwa na watu wengi hapa msibani nigekuja sasa hivi kujaku kuangalia na kupata faraja.Wewe ndiye furaha yangu”
“ Dr Joshua kwa sasa siko katika ile nyumba mpya .Nimerejea kwanza nyumbani kwangu kwa muda.” Akasema Penny na kumstua Dr Joshua
“kwa nini penny? Kuna tatizo lolote?akauliza Dr Joshua
“hapana Dr Joshua hakuna tatizo lolote ila kuna mambo ambayo nataka niyaweke sawa kwanza kabla ya kuanza kuishi katika nyumba mpya.” Akasema Peniela
“ Sawa Peniela tutaongea vizuri nikisharudi kesho.Endapo kuna kitu chochote unakihitaji utawasiliana na Kareem moja kwa moja” akasema Dr Joshua
“ Usiku mwema Dr Joshua”
“ Usiku mwema Peniela.I love you”akasema Dr Joshua na kukata simu
“ Huyu mzee hana akili nzuri.Yaani hata mke wake bado hajazikwa tayari amekwisha anza kuwaza mambo mengine kabisa.Laiti angenifahamu wala asingethubutu kunitamkia maneno yale ya kipuuzi.” Akawaza peniela na kurejea tena chumbani.
“ Peniela kuna jambo nataka nikuombe”
“ Omba chochote Elibariki”akasema Peniela
“Kuna mtu wa muhimu sana ambaye nataka niwasiliane naye”
“ Mke wako? Akauliza Peniela
“hapa sitaki kuwasiliana na mke wangu.Ni rafiki yangu tu ila ni wa muhimu mno ” akasema jaji Elibariki.Peniela akachukua simu yake na kuziandika namba alizotajiwa na Elibariki halafu akapiga.
“ Simu inaita”akasema Penny na kumpatia Elibariki simu
‘ Hallow” ikasema sauti ya upande wa pili
“ Hallow Mathew.Elibariki hapa ninaongea” akasema
“ Elibariki ? ! ..Mathew akastuka
“Ndiyo Mathew ni mimi”
“ Uko wapi Elibariki ? akauliza Mathew
“ Niko sehemu salama kwa sasa.Tayari mmepata taarifa za kilichotokea?
“ Ndiyo Elibariki.Tayari tumekwisha zipata taarifa na muda si mrefu tumetoka hospitali kuutambua mwili wa Noah.Pole sana kwa kilichotokea.”
“ Ahsante sana Mathew.Kwa kweli lilikuwa ni tukio baya sana na sikuwahi kutegemea kama siku moja tukio kama lile linaweza kunitokea.Ilikuwa nife lakini Noah ameniokoa .Amekufa kishujaa .He saved me.He saved my life” akasema Jaji Elibariki huku akilengwa na machozi
“ Kifo cha Noah kimeniumiza sana Elibariki.Lakini hatuna namna ya kufanya imeshatokea imetokea.Kwa sasa uko wapi? Akauliza Mathew
“ Kuna sehemu nimejificha”
“ Is it a safe place? Are you sure you are safe? Akauliza Mathew
“ Yes I’m sure.I’m safe”
“ Ok good.Endelea kujificha hapo hapo .Kwa sasa tunashughulikia msiba wa Noah.Nimewasiliana na wazazi wake tayari nchini Zimbabwe na wamesema kwamba tutawasiliana tena asubuhi ili wanitaarifu kuhusiana na walichokipanga.Noah alikuwa ni kama mdogo wangu kwa hiyo nitaweka kila kitu pembeni kwa sasa na baada tu ya kumzika ndipo nitaanza tena kazi.Ninakuahidi kwamba yeyote aliyehusika katika tukio hili hatabaki salama.Nitakaporejea utashuhudia nitakachokifanya.Kila risasi iliyoingia mwilini mwa Noah italipwa.Kwa sasa endelea kukaa hapo hapo hadi nitakaporejea.Endapokukiwa na tatizo lolote unitaarifu mara moja.Lakini mpaka hapo tutakapoonana tena please stay safe” akasema Mathew na kukata simu

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
SEASON 2

SEHEMU YA 14


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Kifo cha Noah kimeniumiza sana Elibariki.Lakini hatuna namna ya kufanya imeshatokea imetokea.Kwa sasa uko wapi? Akauliza Mathew
“ Kuna sehemu nimejificha”

“ Is it a safe place? Are you sure you are safe? Akauliza Mathew
“ Yes I’m sure.I’m safe”
“ Ok good.Endelea kujificha hapo hapo .Kwa sasa tunashughulikia msiba wa Noah.Nimewasiliana na wazazi wake tayari nchini Zimbabwe na wamesema kwamba tutawasiliana tena asubuhi ili wanitaarifu kuhusiana na walichokipanga.Noah alikuwa ni kama mdogo wangu kwa hiyo nitaweka kila kitu pembeni kwa sasa na baada tu ya kumzika ndipo nitaanza tena kazi.Ninakuahidi kwamba yeyote aliyehusika katika tukio hili hatabaki salama.Nitakaporejea utashuhudia nitakachokifanya.Kila risasi iliyoingia mwilini mwa Noah italipwa.Kwa sasa endelea kukaa hapo hapo hadi nitakaporejea.Endapokukiwa na tatizo lolote unitaarifu mara moja.Lakini mpaka hapo tutakapoonana tena please stay safe” akasema Mathew na kukata simu



ENDELEA………………………..


“ Mathew ameumizwa sana na kifo cha Noah .Nimeisikia sauti yake na anaonekana wazi kwamba ana nia ya dhati ya kulipiza kisasi.Hata mimi ninamuunga mkono kwa hilo.Lazima watu wote waliofanya kitendo kile wapatikane .Watu wale walikuwa na lengo la kuniua lazima niwafahamu ni akina nani kwa nini wanataka kuniua? Akawaza jaji Elibariki.Mawazo mengi yakamjia kichwani kutafakari kuhusiana na tukio lile .

“ Ama kweli maisha ya mwanadamu ni mafupi sana.Dakika chache zilizopita nilikuwa naongea na kucheka na Noah lakini ghafla tu watu wameukatili uhai wake.Tukio lile litaendelea kukaa katika kumbukumbu zangu kwa miaka mingi sana .Ni tukio baya sana kuwahi kunitokea lakini kwa msaada wa Mathew nina hakika nitawafahamu waliofanya tukio lile.” Akawaza na kukumbuka toka alipopigiwa simu na Yule mwanamke na kumzuia asiingie katika gari

“ Mawazo yananijia kwamba yawezekana kabisa sababu ya kutaka kuniua chanzo chake kikawa ni kifo cha Dr Flora ambaye akifo chake kimetawaliwa na utata mwingi. Nilifanikiwa kuufahamu ukweli wa kilichomuua Dr Flora lakini nilishangaa baadaya taarifa yangu kutupwa mbali kwamba ni taarifa ya uongo na ya kuunga unga.Ninamuamini Mathew na hawezi kunipa taarifa ya uongo.Ninahisi kitendo changu cha kuufahamu ukweli wa kifo cha Dr Flora kimewapa mashaka sana watu waliomuua na hivyo ili kuendelea kuificha siri hii wakaona njia bora ni kuniua na mimi pia.Ni akina nani watu hawa? Kwa nni walimuua Dr Flora? Kuna mambo mengi hapa ya kujiuliza na kuyatafutia majibu “ akawaza na taratibu kijiusingizi kikaanza kumpitia kutokana na dawa alizokuwa amepewa .Peniela akamfunika vizuri na kulala pembeni yake.
“ Lini na mimi nitampata mwanaume wa kulala naye kitandani kama hivi ambaye nitakuwa na uhakika kwamba ni mwanaume wangu? Nitakuwa nikilala na wanaume wa wenzangu hadi lini? Nimekwisha anza kuchoshwa na maisha haya.Sitaki tena kuwa sehemu ya Team SC41.Nataka niishi maisha ya kawaida kama wanawake wenzangu.Lakini yote haya mwisho wake umekaribia sana.Nikishaikamilisha operesheni 26B lazima nirejee katika maisha ya kawaida.” akawaza Peniela akiwa ameuweka mkono wake kifuani kwa jaji Elibariki


********

Kumepambazuka na nchi ikia imeamshwa na taarifa kubwa ya kushambuliwa kwa jai wa mahakama kuu.Vyombo vyote vya habari hii ndiyo ilikuwa habari yao kubwa siku hii.Hakuna aliyeweza kufahamu mahal aliko jaji Elibariki japokua kulikuwa na juhudi kubwa za jeshi la polisi katikakumtafuta mahala aliko.Flaviana Hakuweza kabisa kupata usingizi kutokana na hofu aliyokuwa nayo.Mpaka kunapambazuka hakuwa amepata taarifa zzote kuhusiana na wapi alipo mume wake.Akampigia smu baba yake na kumuuliza kama kuna taarifa zzote za kuhsu mahala aliko mume wake lakini mheshimiwa rais akamuhakikishia kwamba vypmbo vya uslama vinaendelea kmtafuta kila mahala .
“Nakuomba baba tafadhali fanya kila linalowezekana ili mume wangu aweze kupatikana.” Kasema Flaviana
“ Flaviana nimekwisha kuahidfi kwamba nitafanay akila linalowezekana ilikuhakkisha kwamba Elibariki anapatikana tena akiwa hai” akasema DrJoshua na kuwaomba wajiandae kwa ajiliya safari ya kueleka mazishini kijijini alikozaliwa mama yao


*******


Mlio wa simu ukamstua Mathew aliyekuwa amejilaza sofani.Akainuka na kuichukua simu yake.Alikuwa ni baba yake Noah ambaye alimfahamisha kwamba wamekaa kikao cha familia na wameafikiana kwamba Noah azikwe jijini Dar es salaam kwa hiyo familia nzima itakuja jijini Dar kwa mazishi.Baada ya kuongea na baba yake Noah Mathew akampigia simu Jason na kumfahamisha mambo aliyoongea na baba yake Noah.Hakumueleza chochote kuhusiana na Ebariki.Kisha ongea na Jason akaenda kumgongea Anitha ambaye macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia akamfahamisha kilichokuwa kinaendelea

“ Anitha there is one more thing” akasema Mathew
“ Kitu gani Mathew?

“ Nimeongea na Elibariki jana usiku”
“ Elibariki?! Anitha akastuka

“ Ndiyo nimeongea naye jana usiku “

“ Kwa nini hukuniambia usiku ule kama uliongea na Elibariki ili nisiwe na mawazo kama amekufa?

“ Usingeweza kunisikia kwa namna ulivyokuwa na uchungu ” akasema Mathew
“ Yuko wapi ? Is he ok? Is he safe? Akauliza Anitha

“ Hakuniambia kama yuko wapi lakini alinihakikishia kwamba yuko salama.”

“ Are you sure he’s safe? Akauliza Anitha

“ Sina hakika sana kama yuko salama lakini yeye mweyewe alinihakikishia kwamba yuko salama”

“ Nina wasi wasi asije kuwa ametekwa na watu na wakamlazimisha apige simu ili kuwaondoa watu wasi wasi” akasema Anitha

“ Hilo linawezekana kabisa .Unajua kwa wakati ule hata mimi kichwa changu hakikuwa sawa.Nilikuwa na mambo mengi sana” akasema Mathew
“ Namba alizokupigia unazo? Akauliza
“ Ndiyo ninazo “ akasema Mathew

“ Tunatakiwa tuzifuatilie namba hizo tuzifahamu ni za nani ili tujue ni wapi tunaweza kuanza kumtafutia jaji Elibariki.We need to find him Mathew.We need to bring him here.This is the only place we can be sure he’s safe” akasema Anitha. Mathew akamtajia namba alizotumia jaji Elibarki kumpigia simu usiku ,Anitha akainuka na kuchukua kompyuta yake ndogo akafungua program Fulani na kuziandika zile namba alizotumia Elibariki kumpigia Mathew.Baada ya kama sekunde ishirini hivi akamgeukia Mathew

“ What ! Umegundua nini? Akauliza Mathew

“ Peniela !..

“ Peniela? Akauliza Mathew

“ Ndiyo.Namba aliyoitumia Elibariki jana kukupigia ni namba ya simu ya Peniela”

“ Are you sure? Akauliza Mathew

“ Yes I’m sure.Ni namba ya Peniela.Are you sure he’s safe there?
“ I think he’s safe.” Akasema Mathew

“ Amefikaje kwa Peniela? Akauliza Anitha

“ Hata mimi sifahamu bado amefikaje lakini nina hakika ni sehemu ambayo amechagua kuwepo kwa sasa.Ukumbuke niliwaambia mapema kwamba Elibariki na Peniela wana mahusiano kwa hiyo atakuwa ameamua kwenda kujificha kule”
“ What about Team SC41? Akauliza Anitha

“ Anitha kwa sasa kilichopo mbele yetu ni kwanza kushughulika na msiba wa Noah na baada ya hapo tutarejea tena kazini na safari hii tutakuwa na kazi kubwa ya kuweza kuwatafuta wale wote waliomuua Noah ,vile vile tuna kazi kubwa ya kufahamu kuhusiana na zile karatasi,na mwisho tuna kazi kubwa ya …” Mathew akasita
“ Kazi kubwa ya nini? Akauliza Anitha

“ Ouh sorry forget about that.Inuka ujiandae leo tuna siku ndefu sana” akasema Mathew na kutoka.
“ Kazi yangu ya mwisho ni kupambana na Team SC41.Sikutaka Anitha afahamu hili kwa sababu hiki ni kisasi changu peke yangu na sitaki yeyote ahatarishe maisha yake kwa sababu ya kazi hii.Nitapambana peke yangu” akawaza Mathew na kuingia chumbani kwake.


********


Miale ya jua ilipenya ndani ya chumba cha Peniela.Sauti za mbwa wa jirani waliokuwa wakibweka ndizo zilizomstua jaji libariki akafumbua macho.
“ Kumekucha” akasema na macho yake yakatua katika saa kubwa ya ukutani ambayo ilionyesha ni saa mbili kasoro za asubuhi.Kitandani alikuwa mwenyewe Peniela hakuwepo

“ Pamoja na matatizo niliyonayo lakini nimelala usingizi mzuri sana japokuwa ulitawaliwa na ndoto mbaya za tukio la jana.Nilisikia raha ya ajabu kulala nikiwa nimekumbatiwa na Peniela.” Akawaza jaji Elibariki na kujitazama majeraha yake akajaribu kusimama hakuwa akisikia maumivu makali kama aliyokuwa akiyasikia usiku
“Ninaendelea vizuri sana.Sisikii maumivu kama yale ya jana usiku” akawaza jaji Elibariki akijaribu kuunyoosha mguu wake ambao ulikuwa na maumivu makali jana na mara mlango ukafunguliwa akaingia Peniela akiwa na sinia lililokuwa na mlo wa asubuhi

“ Elibariki umekwisha amka? Unajisikiaje? Akauliza penny
“ Ninajisikia vizuri sana na sisikii maumivu kama yale niliyokuwa nikiyasikia jana .Nashukuru sana usiku wangu ulikuwa mzuri mno zaidi ya nilivyotegemea japokuwa picha ya tukio lile la jana bado inaendelea kunijia kila mara” akasema Elibariki
“ Ok ni muda wa kupata kifungua kinywa.Leo utapata kifungua kinywa kitandani kwa sababu sitaki utoke kabisa chumbani.Unatakiwa upate mapumziko ya kutosha.Daktari atakuja baadae kuja kukuangalia unaendeleaje pamoja na kukuchoma sindano” akasema Peniela na jaji Elibariki hakusema kitu alibaki anatabasamu akapanda kitandani .
“ Peniela nashukuru sana.” Akasema jaji Elibariki
“ Unashukuru kwa lipi? Akauliza Peniela

“ Kwa kila kitu kwa namna ulivyonipokea na kwa namna unavyonijali.Nashukuru sana na ndiyo maana nilisema kwamba niko sehemu sahihi ninakotakiwa kuwepo” akasema jaji Elibariki .Peniela akatoa tabasamu pana sana na kusema

“ Wewe ni mtu wangu wa muhimu sana na lazima nikuhudumie.Bila wewe hivi sasa ningekuwa nimekwisha anza kuyazoea maisha ya jela.Mimi ndiye ninayepaswa kukushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia” akasema Peniela na kumnywesha Elibariki uji halafu akauliza
“Nina hakika mkeo atakuwa katika wakati mgumu sana hivi sasa baada ya kupata taarifa za kilichotokea jana na hajui uko wapi.Kwa nini usimtaarifu kwamba uko sehemu salama ili asiwe na wasi wasi?
“ Usihofu kuhusu hilo Peniela na wala sihitaji ajue niko wapi.”

“ Kwa nini Elibariki? Yeye ni mke wako na anapaswa kufahamu kila kinachokutokea”
“ Sitaki tu afahamu chochote kuhusiana na mahala nilipo.Kubwa ni kwa sababu za kiusalama.Unajua sifahamu ni nani aliyefanya shambulio lile kwa hiyo nahitaji kukaa mafichoni kwa muda .Katika jambo hili ninakuamini wewe tu” akasema jaji Elibariki na mara simu ya Peniela ikaita.Akainuka na kwenda kuipokea

“ Hallow Osmund habari yako? Akasema Penny
“ Habari yangu nzuri.Peniela niliongea na John nikamtaarifu kuhusiana na ombi lako la kutaka kumuona akakubali na akasema kwamba uonane naye jioni ya leo lakini kwa jioni ya leo sina hakika kama itawezekana kwa sababu hivi sasa naelekea uwanja wa ndege kumpokea Dr Burke anatoka Marekani kuja kuangalia afya ya John kwa hiyo basi nitamtuma kijana aje akuchukue asubuhi hii ukaonane na John ili jioni ya leo awe na daktari akifanyiwa uchunguzi.Uko tayari kwenda kuonana naye asubuhi hii? Akauliza Osmund.Peniela akafikiri kidogo na kusema
“ Ndiyo niko tayari Osmund.Nitakwenda kuonana naye” akajibu Penny

“ Ok vizuri basi kuna kijana nimemuelekeza atakuja kukuchukua hapo nyumbani na atakupeleka kwa John “

“ Ahsante sana Osmund kwa msaada wako huo” akasema Peniela
“Peniela kabla sijakata simu nataka kesho tukutane kwa ajili ya kuongelea kuhusu operesheni 26B “

“ Nitaangalia kama nikipata nafasi nitakueleza Osmund” akasema Peniela na kukata simu akamgeukia jaji Elibariki

“ Are you going somewhere? Akauliza jaji Elibariki

“ Utanisamehe Elibariki kuna mtu ninahitaji kuonana naye asubuhi ya leo lakini sintakawia sana.Sipendi kuondoka na kukuacha peke yako lakini ni mtu wa muhimu sana kuonana naye leo hii” akasema peniela

“ Usijali Peniela.Hata hivyo ninajisikia vizuri na hupaswi kuacha shughuli zako nyingine na kunihudumia mimi” akasema jaji Elibariki
“ Usiseme hivyo Elibarki.Wewe ni mtu muhimu sana kwangu na niko tayari kuahirisha kila kitu isipokuwa mtu huyu ni muhimu sana kuonana naye “ akasema Penny

“ Ni mchumba wako? Akauliza Elibariki.Penny akatabasamu na kusema

“ Sina mchumba ..”
“ Usinidanganye Penny.Usione aibu kuniambia kama una mchumba kwa sababu hata mimi ni mume wa mtu na kisheria sitakiwi kuwepo hapa lakini niko hapa kwa sababu mbili kubwa .kwanza kwa usalama na pili ni kwa furaha ya moyo wangu . I feel so happy around you kwa hiyo basi kama una mchumba ni vizuri ukaniambia ili yasije yakatokea kama yaliyotokea siku ile” akasema jaji Elibariki

“ Elibariki naomba naomba unisamehe sana kwa kilichotokea siku ile lakini nitakaueleza kwa undani baade kuhusiana na suala lile “ akasema Peniela

“ Foregt about what happened Penny.Huna haja ya kutoa maelezo yoyote yale.Hata kama ulikuwa na mahusiano yoyote na Jason mimi hayanihusu kwa sababu mwenye uamuzi na maisha yako na nani uwe naye maishani ni wewe mwenyewe lakini ni vizuri kuwa wazi kama uko katika mahusiano na mtu Fulani ili niweze kufahamu na hasa katika kipindi hiki ambacho niko mafichoni” akasema jaji Elibariki.Peniela akasogelea akambusu na kusema

“ Elibariki naomba uniamini sina mahusiano na mtu yeyote Yule.Jason sina mahusiano naye alikuwa akinitaka siku nyingi lakini sikuwa tayari kumkubalia.Unajua nimepitia kipindi kigumu sana baada ya Edson kuuawa kwa hiyo moyo wangu ulikuwa mzito kufunguka kwa mtu mwingine yeyote lakini nashangaa kwa namna ulivyofunguka kwako kiurahisi.Elibariki you are safe here na utakaa hapa kwa muda wowote utakaotaka hata maisha yako yote kama utahitaji” akasema Peniela na wote wakacheka

“ Ninatamani sana kama ningepata nafasi ya kukaa hapa kwa maisha yangu yote lakini tayari niko katika kiapo cha ndoa kwa hiyo siwezi kuishi hapa maisha yangu yote japokuwa ninatamani sana kama ingekuwa hivyo” akasema jaji Elibariki.Penny akanyoosha mkono wake na kuigusa midomo ya jaji Elibariki halafu akasema

“ Marriage is in hearts and not papers.” Akasema Peniela na kumuacha jaji Elibariki na mawazo mengi


*******


Saa nne za asubuhi tayari Peniela alikwisha jiandaa kwa ajili ya kwenda kuonana na John mwaulaya.Dr Jonesia tayari alikwisha fika na kumuona Elibariki na kuridhika kwamba alikuwa anaendelea vizuri akamchoma sindano na kuondoka.
Gari iliyotumwa kuja kumchukua Peniela na kumpeleka kwa John Mwaulaya iliwasili na akamuaga jaji Elibarki.
“ Elibariki nasikitika kukuacha mwenyewe kwa muda lakini sintachukua muda mrefu sana nitarejea baada ya muda mfupi.Usihofu chochote uko salama.Ili kuongeza usalama zaidi nitafunga mitambo ya usalama na kuweka kamera za ulinzi kila kona ili kuweza kuimarisha ulinzi “ akasema Peniela
“ Nashukuru sana Peniela.Usihofu chochote kuhusu mimi niko salama sana.Hakuna yeyote anayweza kufikiri kwamba ninaweza kuwa hapa” akasema Jaji Elibariki na Peniela akambusu akatoka.
“Sielewi ni kwa nini sehemu ya kwanza kufikiria kujificha nilichagua kwa Peniela ? Ningeweza kwenda kwa Mathew ambako ni salama zaidi lakini sielewi ni kwa nini niliacha sehemu hizo zote na kuchagua kuja kwa Peniela.Nilikuwa sahihi kabisa kuchagua kuja hapa kwa sababu pamoja na matatizo niliyonayo lakini ninapata furaha ya ajabu nikiwa na Peniela na kuna wakati ninasahau kabisa kwamba nina matatizo.Moyo wangu haujawahi kujisikia furaha ya namna hii nikiwa na Flaviana.Ninahisi Flaviana hakuwa mtu sahihi kwangu na ndiyo maana ndoa yetu haina furaha hata kidogo.Kila siku mikwaruzano haiishi.Penny ananijali sana na ananifanya nijsikie furaha ya ajabu” akawaza Elibariki akainuka na kwenda dirishani akachungulia nje
“ Ama kweli maisha ni kitu cha ajabu sana.Leo hii nimekuwa mtu wa kujificha ndani na sitakiwi kuonekana nje.Ni akina nani hawa wanaoitafuta roho yangu? Nimewafanya kitu gani hadi watake kunitoa roho yangu? Lakini bado nina uhakika mkubwa sana kwamba kilichotaka kunipotezea uhai ni taarifa ile ya kifo cha Dr Flora.Ninaufahamu ukweli kwa hiyo wanahofu kwamba siri yao haiko salama.Ni nani walimuua Dr Flora na kwa nini? Hiki ni kitendawili ambacho lazima kiteguliwe na ndipo tutakapoweza kupata majibu ni nani anayetaka kuniua,kwani jambio hili limetokea baada tu ya kuufahamu ukweli ” akawaza jaji Elibariki na kurejea kitandani akakaa

“ Yule mwanamke aliyeniokoa ni nani? Sijawahi kumuona hata mara moja na hakutaka hata kujitambulisha kwangu yeye ni nani na kwa nini aliniokoa.Ninahisi ndiye Yule aliyenipigia simu na kunionya kwamba nisipande gari langu.Laiti kama ningemsikiliza ningeweza hata kuokoa maishaya Noah .Endapo nikifanikiwa kumpata mwanamke Yule yeye ndiye anayefahamu kila kitu kuhusiana na mpango wa kuniua na nina hakika lazima atakuwa akiwafahamu watu waliopanga njama ile. Kazi hii nitakabidhi Mathew yeye ndiye mwenye uwezo wa kulichunguza jambo hili.” Akawaza Elibariki halafu akajilaza kitandani
Peniela aliwasili katika makazi ya John.Lilikuwa ni jumba kubwa sana na la kupendeza.Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Penny kufika mahala hapa.Geti likafunguka wakaingia ndani na gari likaenda kusimama mbele ya jumba kubwa lenye rangi nyeupe.Dereva akashuka haraka haraka na kumfungulia Peniela mlango na kumuongoza kuelekea ndani

“ Nilipokuja siku ya kwanza ilikuwa usiku na sikuushuhudia uzuri wa jumba hili.Dah ni nyumba nzuri sana.” Akawaza Penny huku wakiingia ndani na kupanda ngazi kuelekea ghorofani kilipo chumba cha John Mwaulaya.Yule kijana akagonga mlango wa chumba cha John halafu ukafunguliwa na mtu mwingine aliyekuwa amevaa koti jeupe la kitabibu.Huyu ni kijana mwenye taaluma ya ukadktari naye akiwa ndani ya Team SC41.Alipomuona Peniela akamsalimu kwa heshima kisha akamruhusu aingie ndani na kumuogoza moja kwa moja hadi chumbani kwa John.Uso wa John siku hii ulionekana kuwa na nuru tofauti na siku zilizotangulia

“ Ouh my queen is here” akasema John kwa sauti ndogo na kumfanya Peniela atabasamu

“ Come here.Hug me my queen” akasema John Mwaulaya.Peniela akamsogelea na kumkumbatia pale kitandani
“ Nilikuwa nikihitaji siku nyingi sana kuipata nafasi hii ya kukuona siku moja na kukukumbatia kwani umenifanyia mambo mengi mazuri” akawaza Peniela na kisha akainuka na kuchukua kitambaa.Macho yake yalikuwa yamejaa machozi

“ Unalia nini Peniela? Akauliza John ambaye naye macho yake yalionekana kuwa na machozi

“ Ni miaka mingi nimekuwa nikikuomba nionane nawe nikufahamu lakini umeniruhusu nikuone katika kipindi hiki unachoumwa.Umenihudumia toka nikiwa mtoto mdogo hadi leo hii .Japokuwa sikuwahi kukuona lakini wewe ni zaidi ya baba yangu.” Akasema Penny

“ Peniela usilie tafadhali.Huu ni wakati wa kufurahi na si kutoa machozi” akasema John

“ Ninashindwa kujizuia kutoa machozi kupata nafasi ya kukuona wakati ukiwa katika hali hii.Ninaumia sana kukuona hivi” akasema Penny na mara mlango wa chumba cha John ukafunguliwa akaingia Josh

“ Josh ! naomba unipishe kwanza nina maongezi muhimu na binti yangu Peniela” akasema

“ John ni jambo la muhimu” akasema Josh.John akamfanyia ishara Peniela atoke nje kidogo ili aongee na Josh

“ Mzee ile kazi yako nimeimaliza” akasema Josh

“ Dr Burke is dead? Akauliza John
“ Ndiyo tayari amekwisha fariki.Lakini ilinilazimu kumuua vile vile na Osmund”
“ Good Job.How it happened? Akauliza John

“ Asubuhi ya leo nilimfuatilia Osmund hadi uwanja wa ndege bila ya yeye kufahamu.Alimpokea Dr Burke na kumpeleka katika hoteli aliyompangishia na baada tu ya kuingia katika hoteli hiyo niliwatokea ghafla na bila kupoteza hata sekunde moja niliwamiminia risasi kupitia bastora yenye kiwambo cha sauti kwa hiyo hakuna mtu yeyote aliyeweza kusikia kitu chochote kilichotokea.Dr Burke na Osmund wote wamekufa.Kwa hiyo mzee uko salama.You are safe now” akasema Josh
“ Josh nakushukuru sana kijana wangu.Umeyaokoa maisha yangu.Nina deni kubwa kwako” akasema John Mwaulaya

“ sijali mzee.Siku zote nitakuwa mtiifu kwako “ akasema Josh na kutoka.Peniela akaingia na kumkuta John akiwa na uso wenye furaha sana

“ Nina furaha sana Peniela kwanza kwa kutembelewa na wewe na vile vile kwa kuletewa habari njema na Josh” akasema John
“ Hata mmi ninafuraha sana ya kukutana nawe japokuwa ni kwa muda mfupi kwani Osmund aliniambia kwamba leo kuna daktari anakuja kukufanyia uchunguzi wa afya yako kwa hiyo sitakiwi kuchukua muda mrefu sana.Ninatamani sana kupata muda mrefu wa kukaa nawe ninatamani kukuhudumia hasa katika kipindi hiki unachoumwa na nina mambo mengi ambayo ninahitaji kuongea nawe” akasema Penny

“ Penny usijali kuhusu alichokwambia Osmund.Hakutakuwa na huo uchunguzi wa daktari kama alivyodai.Tafadhali naomba ushinde nami leo hii.Hata mimi nina hamu sana ya kukaa na wewe kuna mambo mengi ambayo nahitaji kukueleza” akasema John

“ Hakutakuwa na uchunguzi wa daktari? Aliniambia kwamba anaelekea uwanja wa ndege kwenda kumpokea Dr Burke.” Akauliza Penny
“ Ugonjwa wangu si wa kutibiwa na Dr Burke.Nahitaji daktari mtaalamu sana wa mishipa ya fahamu.”

“ Kwani unasumbuliwa na nini baba ? akauliza
“ Nina tatizo katika mishipa ya fahamu ya kichwa na ndiyo maana kuna baadhi ya viungo Fulani vya mwili havifanyi kazi sawasawa,”

“ Umepata matibabu gani mpaka sasa hivi? Akauliza Penny

“ Bado sijapata matibabu ya maana mpaka sasa.” Akajibu John

“ Wewe ni kiongozi wa Team SC41 ambayo inafanya kazi ya kulinda maslahi ya marekani kwa nini basi wasikutibu? Marekani kuna hospitali kubwa na nzuri na zenye wataalamu wakubwa sana wanaoweza kuutibu ugonjwa huu.Kwa nini wanakuacha uteseke? Hivi ndivyo team SC41 ilivyo kwamba ukiumwa wanakuacha bila huduma? Akauliza Penny
“Si hivyo Peniela.Jambo hili ni gumu tofauti na unavyofikiri.” Akasema John na kumpa namba Peniela afungue kasiki lililokuwa ukutani na achukue albamu la picha amletee.Peniela akachukua albamu lile kubwa la picha akamletea.Ukurasa wa tatu kulikuwa na picha ya kijana mmoja mtanashati aliyevaa suti nzuri yenye kupendeza akiwa amekaa juu ya jiwe ukingoni mwa bahari

“ Unaiona picha hii? Akauliza John

“ Ndiyo ninaiona” akajibu Penny

“ Huyu kijana unayemuona hapa katika hii picha ni mimi” akasema John.Penny akapatwa na mshangao mkubwa.Kijana Yule aliyeko katika picha ile na John Mwaulaya ni watu wawili tofauti kabisa.

“ This is you? Akauliza Paniela
“ Ndiyo “
“ Mbona hamfanani kabisa “ akauliza Penny

“ Hapa ilikuwa ni kabla ya kujiunga na Team SC41.Wakati huu nilikuwa katika chuo cha kijeshi nchini Marekani nikijifunza masuala ya urubani wa ndege vita.”

“ Wewe ni mwanajeshi? Akauliza Penny
“ Yah nilikuwa mwanajeshi.Wakati nilipopiga picha hii sikuwa na wazo kama siku moja nitakuwa kiongozi wa Team SC41.” Akasema John
“Nilikuwa kijana mtanashati sana nyie vijana mnasema Handsome boy “ akasema John na kumfanya Penny atabasamu

“ IIinilazimu kuibadili sura yangu mara mbili na ndiyo maana unaniona nikiwa katika sura hii ya tofauti kabisa na ile iliyoko katika hiyo picha.” Akasema John
“ Kitu gani kilisabababisha ukabadilisha sura yako? Akauliza Penny

“ Penny ni mambo mengi sana makubwa yametokea ndani ya Team SC41 na ndiyo maana nkalazimika kuibadili sura yangu mara mbili .Nilianza kusumbuliwa na ugonjwa huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa pili wa kuibadili sura.”

“ Kitu gani kilipeleka ukabadili sura yako ? akauliza Peniela

“ Penny kuna mambo mengi sana ambayo huyafahamu na ninatamani sana kukueleza lakini ninashindwa kwa sababu Team SC41 si sehemu sahihi unayostahili kuwepo.”
Peniela akamtazama John na kusema

“ Bado hujanieleza ni kwa nini team Sc41 wameshindwa kukupatia matibabu?akauliza tena Penny
“ Its because I’m dead “
“ You are dead? Akauliza Penny kwa mshangao
“ Yes I’m dead” akasema
“ Ninashindwa kuelewa baba John umekufa vipi?
“ Ngoja niliweke hivi ili unielewe.Ni kwamba kwa miaka kadhaa sasa hivi ninajulikana kwamba nimekwisha fariki.Mimi ni mtu niliyekuwa nikitafutwa sana na serikali mbalimbali duniani kwa hiyo nililazimika kutumia njia hii ya kutengeneza kifo changu ili nisiendelee kutafutwa na ndiyo maana kuna ugumu mkubwa kwa mimi kutibiwa hapa nchini na nje ya nchi”akasema John
“ Kitu gani kilisababisha utafutwe? Akauliza Peniela
“ Nilifanya jambo kubwa sana ambalo sintaweza kukueleza” akasema John


JOHN MWAULAYA ALIFANYA JAMBO GANI KIASI CHA KUTAFUTWA NA SERIKALI MBALI MBALI DUNIANI? ENDELEA KUIFUATILIA SIMULIZI HII…
 
SEASON 2
SEHEMU YA 15
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Kitu gani kilipeleka ukabadili sura yako ? akauliza Peniela
“ Penny kuna mambo mengi sana ambayo huyafahamu na ninatamani sana kukueleza lakini ninashindwa kwa sababu Team SC41 si sehemu sahihi unayostahili kuwepo.”
Peniela akamtazama John na kusema
“ Bado hujanieleza ni kwa nini team Sc41 wameshindwa kukupatia matibabu?akauliza tena Penny
“ Its because I’m dead “
“ You are dead? Akauliza Penny kwa mshangao
“ Yes I’m dead” akasema
“ Ninashindwa kuelewa baba John umekufa vipi?
“ Ngoja niliweke hivi ili unielewe.Ni kwamba kwa miaka kadhaa sasa hivi ninajulikana kwamba nimekwisha fariki.Mimi ni mtu niliyekuwa nikitafutwa sana na serikali mbalimbali duniani kwa hiyo nililazimika kutumia njia hii ya kutengeneza kifo changu ili nisiendelee kutafutwa na ndiyo maana kuna ugumu mkubwa kwa mimi kutibiwa hapa nchini na nje ya nchi”akasema John
“ Kitu gani kilisababisha utafutwe? Akauliza Peniela
“ Nilifanya jambo kubwa sana ambalo sintaweza kukueleza” akasema John

ENDELEA…………………..

Peniela alimuangalia John Mwaulaya na kusema
“ Ni jambo gani baba ambalo huwezi kunieleza? Akauliza Peniela
“ Peniela kuna mambo mengi sana ambayo siwezi kukueleza.Itakuwa vyema endapo hutayafahamu” akasema John na kufumba macho akakumbuka tukio moja kubwa alilowahi kulifanya na ambalo lilisababisha abadilishe sura yake kwa mara ya pili.
Ni siku ya jumanne asubuhi John akiwa ofisini kwake ukaingia ujumbe katika anuani yake ya barua pepe.Ujumbe ule ulitoka katika makao makuu ya Team SC41 Marekani.Katika ujumbe ule alitaarifiwa kwamba kuna kiongozi mmoja wa kidini kutoka nchini Uingereza anakuja Tanzania kwa ziara ya kidini.Ziara ya kiongozi huyo wa kidini imebeba ajenda kubwa nyuma yake kwani anakuja kuzungumza na serikali ya Tanzania kuhusiana na kutoruhusu uwekezaji wowote wa marekani katika madini ya Uranium.Kwani kwa siku za karibuni Marekani imeonyesha kutaka kufanya uwekezaji mkubwa sana katika uchimbaji wa madini ya Uranium nchini Tanzania.Taarifa ile ilimtaka John na Team SC41 wahakikishe kwamba kiongozi yule wa kidini anauawa kabla hajaonana na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mazungumzo ya faragha.
John mwaulaya aliusoma tena ujumbe ule kwa makini,akaurudia tena na tena na kuuelewa.
“ Ninatakiwa kumuua kiongozi wa kidini ! akasema kwa sauti ndogo
“ Hii si kazi rahisi hata kidogo.Ni jambo zito ambalo sikuwahi kulifanya toka kujiunga na Team SC41.” Akawaza John na kuegemea kiti chake akafikiri sana na baada ya kama nusu saa hivi akawaita vijana wake katika chumba cha mikutano
“ Nimepokea maelekezo toka makao makuu kwamba kuna kiongozi mmoja wa kidini anatoka nchini Uingereza atafanya ziara ya kichungaji nchini Tanzania.Ziara hiyo imebeba ajenda kubwa nyuma yake.Katika ziara hiyo kiongozi huyo mkuu wa kidini anataka kuja kuishawishi serikali ya Tanzania kutoruhusu uwekezaji wowote wa madini ya Uranium unataka kufanywa na Marekani.Kwa kuwekeza katika kuchimba madini ya Uranium Marekani itakuwa imekiuka makualiano yaliyofikiwa kati ya mataifa yenye nguvu za kinyuklia duniani kwamba waendelee kupunguza matumizi ya nishati hii ya nyuklia lakini Marekani imeonekana kutaka kuongeza idadi ya vinu vya nyuklia katika kuzalisha nishati ya umeme.Makao makuu wanahitaji kiogozi huyu wa kidini auawe kabla hajaonana na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Akasema John na kuwatazama vijana wake.
“ Jambo hili ni kubwa na kumuua kiongozi mkubwa kama huyu si kazi rahisi lakini kwa kuwa tnfanya kazi kwa maslahi ya Marekani lazima tuifanye.Ilitufanikiwe lazima tubuni mkakati mzito sana utakaotuwezesha kumuua kiongozi huyo.Mkakati nilioubuni nikwamba itaabidi mmoja wetu ajifanye ni mchungaji na ajumuike pamoja na wachugaji wengine katika kumpokea kiongozi huyo toka Uingereza.Hili ni jambo zito na linalohitaji umakini mkubwa kwa hiyo nitasimama mimi mwenyewe katika kuifanya shughuli hii kwani hakutakiwi kosa lolote hapa.Nitakachokifanya ni kwamba nitakuwa na pete mkononi ambayo itakuwa imepakwa sumu na katika pete hiyo kuna kisindano kidogo sana ambacho si rahisi kusikia kama kimekuchoma.Nikishikana mkono tu na kiogozi huyo na kisindano kile kikifanikiwa kumchoma basi sumu ile kali husambaa haraka sana mwilini atakufa ndani ya dakika kumi na tano tu.Kuhusu changamoto ya ulinzi ni kweli ulinzi utakuwepo lakini hautakuwa ni ulinzi mkubwa sana kwani huyu si kiongozi wa kiserikali japokuwa ni kiongozi mwenye heshima kubwa sana nchini mwao.” John Mwaulaya akawaambia vijana wake na kisha wakaanza mikakati kabambe ya maandalizi ya mpango ule .
Siku ya siku ikawadia ambapo askofu Wilbert young Jr akitokea nchini Uingereza akawasili nchini na kupokewa na viongozi kadhaa wa dhehebu lake na kisha msafara wake ukaelekea katika kanisa kuu la dhehebu lake .Katika njia ya kuelekea ofisi kuu viongozi zaidi ya ishirini toka katika madhehebu mbali mbali walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kuonyesha mshikamano wao kwa kiongozi huyu mkubwa ambaye alikuwa akisalimiana na mmoja mmoja.Miongoni mwa watu waliokuwemo katika mstari ule wa kusalimiana na kiongozi yule alikuwepo mtu mmoja aliyevalia mavazi nadhfu ya kichungani na alionekana kama mchungaji kijana sana.Hakuna aliyeweza kudhani kwamba mtu yule aliyekuwa miongoni mwao akiwa na sura yenye tabasamu la kichungaji alikuwa ni mtu hatari sana.Huyu alikuwa John Mwaulaya kiongozi wa team SC41.Kiongozi yule wa kidini alishikana mkono na John Mwaulaya wakasalimiana na alionyesha kufurahi sana kukutana na mchungaji kijana kama John na kumtaka azidi kumtumaini Mungu nasiku moja atafika mbali katika kazi yake ya utumishi.Katika viongozi wote waliokuwe popale ,ni John peke yake ambaye alionekana kuchukua muda kidogo kuzungumza na Askofu Wilbert.Zoezi la kusalimiana na wachungaji wengine na maaskofu liliendelea halafu askofu Wilbert akakaribishwa kuingia ofisi kuu ambako kulikuwa na kikao kifupi cha ukaribisho kabla ya kuendelea na ratiba nyingne alizopangiwa .Wakati askofu mkuu wa Tanzania akitoa maeneno ya kumkaribisha askofu Wilbert alianza kujisikia vibaya akaomba apatiwe maji ya akanywa lakini akazidi kujisikia vibaya na ghafla akajikuta akiishiwa ngucvu na kuanguka chini.Kizaa zaa kikaibuka na gari la wagonjwa likaitwa haraka sana wakampakia askofu Wilbert wakamkimbiza hospitali lakini hawakufanikiwa kufika askofu Wilbert akafariki.
Taarifa za kifo cha askofu Wilbert ziliistua sana serikali ya Uingereza na raia wake kwani askofu yule ni mtu aliyekuwa anaheshima kubwa ndani ya nchi ya Uingereza.Mstuko haukuwa kwa serikali ya Uingereza peke bali kwa serikali nyingi duniani zilistuswa sana na tuko lile ikiwemo serikali ya Tanzania.
Kufuatia tukio lile serikali ya Tanzania ikishirkiana na seriakali ya Uingereza walianzisha uchunguzi mkubwa ili kufahamu ni nani hasa waliofanya kitendo kile kwani ilithibitika kwamba Askofu Wilbert aliuawa kwa sumu.Ilimlazimu John mwaulaya kufanyiwa upasuaji wa kuibadili sura yake ili kupoteza kila aina ya ushahidi kwani taarifa kulikuwa na kila dalili za kugundulika kwamba ndiye aliyefanya mauaji yale.Pamoja na kumbadili John Mwaulaya sura lakini iliwalazimu pia kutengeneza kifo chake na baada ya miezi sita kupita ya uchunguzi wa kifo cha askofu Wilbert taarifa ilitoka na kubainisha kwamba aliyemuua ni mtu mwenye uraia wa Tanzania na marekani lakini taarifa ikaonyesha kwamba mtu yule ambaye alifahamika kwa jina la bandia la Moses Lupakise na taarifa zake zote zikasambazwa kila mahala duniani ili atakapoonekana akamatwe lakini baadae tayari ikatolewa kwamba Moses alikwisha fariki dunia.Hiyo ni sababu kubwa iliyowafanya team SC 41 kushindwa kumpeleka John nchini marekani kwa matibabu.
“ John ! ..Peniela akamstua John aliyekuwa amefumba macho akikumbuka mbali sana.
“Peniela samahani nilikuwa mbali sana kimawazo.Umenifanya nikumbuke mambo mengi sana makubwa” akasema John .Peniela akamtazama na kusema
“ Samahani kwa kukukumbusha mambo ambayo umekwisha yasahau”
“ Usijali Peniela.Kichwa changu kimejaa kumbukumbu nyingi mbaya ambazo najaribu sana kuzisahau lakini ninashindwa.”
“ Usiwaze sana kuhusiana na mambo yaliyopita.Kitu kikubwa kwa sasa ni kushughulika na afya yako ,utibiwe na upone uendelee na maisha yako ya kawaida.Niambie ni kitu gani ninachoweza kukifanya ili kukutibu?
“ Peniela ahsante kwa kunijali lakini kwa sasa sina hakika kama nitapona tena.Hali yangu japokuwa inaimarika lakini ninajua kwamba sina muda mrefu wa kuishi kwa hiyo hakuna haja ya kupoteza nguvu kunihudumia.Its my time to face death”
“usiseme hivyo John,ninakuhitaji sana katika maisha yangu.Wewe bado ni mtumuhimu sana katika maisha yangu.Umenihudumia angali nikiwa mdogo na ni wakati wangu sasa kukuhudumia na kuhakikisha kwamba unapona .Wewe ndiye baba ninayekufahamu ,kwa hiyo naomba uniruhusu nikuhudumie upone.I need to spend much time with you.I don’t want you to die” akasema Peniela huku machozi yakimtoka.John akamuonea huruma sana binti yule akamfanyia ishara amsogelee.Penny akaketi katka kitanda cha John
“ kwa mara ya kwanza leo hii umenifanya nibadili msimamo wangu.Ninataka kuendelea kuishi tena kwa sababu yako.Nataka niyatengeneze maisha yako upya kwani ni mimi niliyeyaharibu kwa kukuingiza huku Team SC41.” Akasema John.
“ Nashukuru sana John kwa kuendelea kunithamini .Nashukuru sana kwa kukubali kutibiwa” akasema Peniela.John Mwaulaya akafumba macho akafikri kidogo na kusema
“ Kuna daktari mmoja ambaye nitakupa mawasiliano yake anaitwa ni rafiki yangu sana utawasiliana naye na utamfahamisha hali yangu na halafu tatakupa jibu nini anaweza akafanya.Huyu ni daktari ambaye nina hakika anaweza akanitibu”
“ Kama ulikuwa na daktari mtaalamu kama huyu kwa nini hukumtafuta mapema toka awali na ukasubiri hadi hali yako imefikia hapa ? Akauliza Peniela
“ Sikuwa nikihitaji kuishi .Nilikata tamaa na maisha yangu kwani sikuona tena thamani ya kuendelea kuishi kutokana na mambo mengi mabaya niliyoyafanya “
“ Ndiyo maana ninataka utibiwe upone .You deserve a second chance.”
“ Second chance? Akauliza
“ Yes you deserve a second chance .Pengine ni mpango wa Mungu ili uweze kuyabadili maisha yako” akasema Peniela.John akamtazama na kusema
“ Do you believe in God? Peniela Akakaa kimya
“ Una fikiri Mungu anaweza akanisamehe makosa yote niliyoyatenda? Akauliza John.
“ John kwa sasa tunachotaka kushughulika nacho ni afya yako na baada ya hapo haya mambo mengine ya kiimani kama unahitaji ushauri wao utawaona viongozi wa dini lakini kwa sasa unatakiwa kwanza upone” akasema Peniela.John akamuelekeza amletee kitabu alichoandika namba mbalimbali za simu akampatia mawasilano ya daktari rafiki yake.
Baada ya kupewa namba zile Peniela hakutaka kuendelea kupoteza wakati akamuaga John na kuondoka.Hakutaka kupoteza muda mwingi pale kwa John kwani alimuacha jaji Elibariki peke yake nyumbani

*******

Ilikuwa ni siku ndefu sana iliyoambatana na matukio mengi.Wakati bado watu wakiendelea kutafakari mahala alipo jaji Elibariki na sababu ya gari lake kushambuliwa ,watu wawili walikutwa wamekufa kwa kupigwa risasi katika chumba cha hoteli ambao mmoja alikuwa raia wa Marekani na mwingine raia wa Tanzania.
Saa kumi na mbili za jioni Dr Joshua alirejea nyumbani akitokea kijijini alikozaliwa mke wake Dr Flora walikoenda kumzika.Mara tu baada ya kuwasili nyumbani Flaviana akamfuata baba yake na kumuuliza kama kuna taarifa zozote amezipata kuhusiana na uchunguzi unaoendelea ili kuwabaini walioshambulia gari la mumewe na mahala aliko Elibariki.
“Mpaka sasa hivi sijapokea taarifa zozote za kuhusiana na tukio lile.Naomba unipe muda kidogo ili niwasiliane na watu wangu nijue wamefikia wapi” akasema Dr Joshua.
Bila kupoteza muda Dr Joshua akawaita Dr Kigomba na captain Amos ambao ni washirika wake wa karibu na kutaka kupata ripoti ya kinachoendelea kuhusiana na kumtafuta Elibariki
“ Mpaka jioni hii Elibariki hajaonekana na hajulikani yuko wapi.Hakuna uhakika kama alitoka hai katika shambulio lile ama alikuwa mzima.Na hata kama alikuwa mzima basi nina uhakika mkubwa sana kwamba lazima atakuwa amejeruhiwa.Vijana wamekuwa wakizungukia hospitali zote kubwa na zahanati ili kutaka kufahamu kama kuna mgonjwa alifika kutibiwa akiwa na majeraha ya risasi lakini hakuna hata hospitali moja iliyothibitisha kumtibu mgonjwa mwenye jeraha la risasi.”akasema Dr Kigomba
“ Kwa hiyo unataka tuamini vipi? Kwamba Elibariki amefariki dunia ? akauliza Dr Joshua
“ Sina hakika sana kama alikufa ama bado yuko hai.Ili kufahamu kama Elibariki mzima au alikufa inatubidi kwanza tumfahamu mtu ambaye alikuwa akipambana na vijana wetu.Bado mpaka sasa hivi hatujafanikiwa kumfahamu mtu huyo ni nani .Lakini ni wazi kwamba mtu yule alikuwa akipambana kumsaidia Elibariki na nina hakika ni huyu ndiye aliyemtoa alibariki pale na kumpeleka mafichoni kwa hiyo kama tunataka kufahamu mahala alipo Elibariki na kama ni mzima ama alikufa basi tunatakiwa kumfahamu huyu mtu ni nani” akasema Dr Kigomba
“ Kuna ugumu gani wa kumfahamu mtu huyo? Sisi ndio tulioishika nchi hii na kila kitu kiko chini yetu kwa hiyo tunatakiwa tutumie kila aina ya mbinu ili kuweza kumpata huyo mtu ambaye nina hakika kabisa kwamba tayari anafahamu kila kitu kuhusiana na sisi na amekuwa akitufuatilia.Nina uhakika kabisa kwamba siri yetu tayari imekwisha julikana .Lakini kuna jambo ambalo nimelifikiria sana siku ya leo” akasema Dr Joshua
“ Jambo gani hilo? Akauliza Captain Amos
“ Tulianza vizuri mpango wetu na tumekwenda viuri sana lakini hapa karibu na kufika mwisho kumeanza kutokea mambo ambayo yanahatarisha kuharibika kabisa kwa mpango wote.Na kama tusipokuwa makini basi tunaweza kujikuta tukipoteza kila kitu na kushindwa kufikia malengo yetu.Mtu wa kwanza ambaye aliapa kuharibu kila kitu alikuwa ni Frola ambaye tayari tumekwisha muondoa.Baada ya Flora kumeibuka tena kikwazo kingine ambacho ni Elibariki na huyo mtu aliyemsaidia jana.Elibariki amefahamu kilichomuua Flora na kama atakuwa amenusurika katika ajali basi lazima atataka kulichimba kwa undani suala hili .Tusimpe nafasi ya kufanya hivyo.Kwa ajili hiyo basi nimefikiria sana na kuona kwamba kuna umuhimu wa kumaliza kila kitu haraka sana,kwa sababu endapo tukiendelea kuvuta muda tutajikuta tukishindwa kabisa kufikia mwisho kwa hiyo basi ninataka kuanza mawasiliano na wale jamaa zetu ili ndani ya wiki mbili wawe wamejikamilisha na kutupatia fedha zetu ili tuwape mzigo wao.Hakuna haja ya kuendelea kuogopa na hatuwezi kuziachia trilioni hizi nyingi za fedha ambazo watatumia hadi vitukuu vyetu kwa maana hiyo basi kwa sasa endeleeni kuhakikisha kwamba hakuna jambo lolote litakalojitokeza kuharibu mpango wetu na tukifanikiwa kumaliza salama hatutakuwa na wasi wasi tena na Elibariki wala huyo mwenzake” akasema Dr Joshua
“ Hilo ni wazo zuri sana Dr Joshua.Ni kweli hakuna haja ya kuendelea kulivuta sana suala hili kwa hiyo kuimaliza biashara hii ndani ya muda mfupi ujao itakuwa vizuri sana kwani kadiri siku zinavyozidi kwenda yanazidi kuibuka mambo mapya kila siku” akasema Captain Amos
“ Ok jamani shughulikieni suala hilo la kuwatafuta Elibariki na huyo mwenzake na mimi nitawasiliana na watu wetu na kuwafahamisha kwamba tumeamua kufanya biashara hii haraka iwezekanavyo”akasema Dr Joshua kisha wakaondoka.
“nadhani kulimaliza suala hili kwa haraka ndilo jambola msingi kwa sasa.Nimeanza kuingiwa na wasiwasi kwamba kuna hatari ya kuyakosa yale matrilioni ya fedha.Karibu nitamaliza muda wangu wa uongozi na kwa hiyo ninataka baada ya kumaliza muda wangu wa kuongoza nimchukue Peniela niondoke naye nikaishi naye mbali kabisa maisha ya kifalme nikifurahia uzee wangu.Nimemkumbuka sana huyu binti ngoja nimpigie simu.Peniela ni mwanamke ambaye ananifanya nijione kama kijana wa miaka thelathini nikiwa naye.Ningefanya kosa kubwa sana kama ningekubali peniela akafungwa gerezani.Nitamfanyia mambo makubwa binti yule na hatawafikiria tena vijana ambao hawawezi kumpa chochote.” Akawaza Dr Joshua na kuchuk ua simu yake akampiga simu Peniela
“ Hallow Peniela” akasema Dr Joshua baada ya Peniela kupokea simu
“ hallow Dr Joshua habari yako?Umeshindaje leo? Tayari umekwisha rejea?akauliza Peniela ambaye alikuwa ametoka nje kuongea na Dr Joshua akiogopa jaji Elibariki kusikia maongezi yale
“ Nimerudi salama na tumemaliza salama kumzika Flora.Umeshinda salama?
“Mimi nimeshinda salama Dr Joshua.Niliyekuwa nakuhofia ni wewe tu”
“ Hata mimi nilikuwa nakuwaza sana Peniela.Natamani hata muda huu ningekuja nikuone kama ungekuwa katika ile nyumba niliyokupa.” Akasema dr Joshua
“ usijali Dr Joshua nikishamaliza shughuli yangu huku nitahamia katika ile nyumba.Hata mimi sipendi kukaa mbali nawe.”
“ Nashukuru sana Peniela kusikia hata wewe unaniwaza.Ninakupenda zaidi ya unavvoweza kufikiri na nitakufanyia mambo makubwa sana ambayo sijawahi kumfanyia mtu yeyote.Utaishi maisha zaidi ya malkia yote haya yatawezekana tu kama ukiniahidi kitu kimoja”
“Kitu gani Dr Joshua?
“Nataka uniahidi kwamba hautaingia katika mahusiano yoyote na hawa vijana na kwamba utakuwa na mimi tu”
“ Dr Joshua kwa sasa kwa vile uko huru basi siwezi kuwa na mahusiano na kijana mwingine yeyote” akasema Peniela na kumfurahisha Dr Joshua
“ Umenifurahisha sana Peniela na ninapenda kukumbusha kwamba ahadi yangu iko pale pale”
“ ahadi gani Dr Joshua?
“ kukuoa” akasema Dr Joshua na kumfanya Peniela atabasamu
“NI mapema sana Dr Joshua kuzungumza kuhusiana na masuala hayo ya kuoana.Bado tuna mambo mengi sana ya ufanya kabla ya kufikia maamuzi hayo makubwa”akasema Peniela
“ Hakuna muda wa kusubiri sana peniela.Ngoja ngoja yaumiza matumbo.Mimi ninakupenda na kwa sasa hakuna kizuizi chochote kinachonifanya nisifunge nawe ndoa.Flora tayari amekwisha kwenda kwa hiyo nina uhuru wa kufanya kila ninachokitaka” akasema Dr Joshua
“ Dr Joshua ni mapema sana kuanza kufikiria masuala kama hayo.Lakini usijali tutapata wasaa mzuri tutaongea na kuyaweka sawa” akasema Peniela.
“ Ok peniela nitakupigia tena baadae ili tuongee kwa undani zaidi kuhusu suala hili”
“ Hapana usinipigie baadae Dr Joshua nimechoka sana leo na ninahitaji kupumzika”akasema peniela wakaagana na dr Joshua akakata simu
“ Huyu mzee anaonekana kifo cha mkewehakijamgusa kabisa.Hainiingii akilini eti hata mkewe hajamaliza siku moja kaburini tayari ameanza kufikiria masuala ya kuioa.laiti angenijua wala asingeongea upuuzi ule .Lakini mbona ninaanza kuingiwa na shaka sana kuhusiana na kauli hizi za Dr Joshua? Toka kipindi kile hata mkewe bado hajafariki alikuwa akinitamkia kwamba mke wake atakufa hivi karibuni na mimi nitakuwa first lady.Ninapatwa na wasiwasi kwamba ya wezekana kifo cha dr Flora kikawa ni cha kupangwa ili mambo anayoyataka Dr Joshua yaweze kutimia” akawaza peniela wakati aiingia chumbani.Akaiweka simu mezani na kupanda kitandani akajilaza pembeni ya jaji Elibariki
“ Elibariki kuna kitu nataka kukuuliza” akasema Peniela
“Uliza Penny”akasema Elibariki
“ Nini kilimuua Dr Flora? Akauliza Peniela na kumstua sana Elibariki
” kwa nini unauliza hivyo Penny?
“ Ninahitaji tu kufahamu” akasema Penny
“ Dr Flora alikufa kwa shinikizo la damu”
“ Are you sure? Akauliza penny
‘ yes I’m sure” akajibu jaji Elibariki na kuendelea kushangaa kwa nini Peniela alimuuliza maswali kama yale.

NI BIASHARA GANI AMBAYO DR JOSHUA NA WENZAKE WANATAKA KUIFANYA? TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
NMkuu unanifukuzisha kazi hivihivi sijalala kabisa na nina kazi nyingi mno ofisinilakini kila saa nafungua kusoma episode mojamoja ....najionea huruma mno nimepatikana.Naona kama enzi za Willy Gamba zimerudi.keep it up ..tunyooshe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…