Penny akubali kushea penzi na wema

Penny akubali kushea penzi na wema

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Stori: Imelda Mtema
MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.
Penny katika pozi na Wema.
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, aliliambia gazeti hili maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye amerejesha uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji huyo mpenda vidosho.
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
“Ninampenda Diamond na sitaki kumpoteza. Nia yangu ni kumuona akiwa na furaha. Kama Diamond anaona kuna msichana mwingine wa kutoka naye na kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.

Wema Sepetu 'Madam 'na Peniela Mwingilwa ‘Penny’.

Kumekuwa na habari zisizo shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko Ughaibuni.
Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka
 
Hat asipokubali kwani yeye ndo nani?? Si hawara tu kama ao wengine,hana jipya Huyo mapovu yanamtok bure atafute zezeta mwenzie tu atulie
 
Huyo dimond sijui ana kipi cha kupagawisha wasichana au ndo skendo za umaarufu.
 
Ndo maana wakamwita sukari ya warembo.
........... Kama huna moyo inakubidi uanze.
 
Wanamchafua tu Penny huyo mwandishi Imelda alieandika hiyo habari ana njaa kama nini na wema sepetu ndio anaemuweka mjini
 
Duh wewe noma hadi imelda unamjua?? Yule dada mweus mweus ivi?? We mwache tutamwanzishia thread ya madudu yake hadi akimbie,kuna uyo na mwenzie mnaly sijui na shakoor jongo hao ndo vinara wa umbea grobal publisher,yao wanayoyafanya aah,ngoja na sisi umu tuanzishe magazeti yetu,watatukoma
 
wanamchafua tu penny huyo mwandishi imelda alieandika hiyo habari ana njaa kama nini na wema sepetu ndio anaemuweka mjini

lakini si peny mwenyewe alikubali kuhojiwa na hao wambea wa bamaga. Angekaa kimya tu ingesaidia.
 
Duh wewe noma hadi imelda unamjua?? Yule dada mweus mweus ivi?? We mwache tutamwanzishia thread ya madudu yake hadi akimbie,kuna uyo na mwenzie mnaly sijui na shakoor jongo hao ndo vinara wa umbea grobal publisher,yao wanayoyafanya aah,ngoja na sisi umu tuanzishe magazeti yetu,watatukoma

Me simpeeendiii....ukimuona jinsi alivyo huwez amini km yeye ndo anayehusika na kusambaza huu udaku..walah yule dada anastahili tindikali kazidi
 
Me simpeeendiii....ukimuona jinsi alivyo huwez amini km yeye ndo anayehusika na kusambaza huu udaku..walah yule dada anastahili tindikali kazidi

Duh. ....
 
Back
Top Bottom