Penny: Diamond kama chizichizi vile!

Penny: Diamond kama chizichizi vile!

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304


MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel Ten, Penniel Mungilwa ‘Penny' amefunguka kuwa sifa ya aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond' ni kama chizichizi lakini kwa undani zaidi ni mtu makini.

Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo mbali na kutamka kauli hiyo, alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha kwa kupeana nafasi.

Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja na ushee hivi, Penny alisema watu wote wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano, anakuwa makini sana.

"Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa ndani ni mtu makini sana. Anajua kulea, anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake anapokuwa nyumbani, anajali," alisema Penny na kuongeza:

"Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika maisha ya kawaida ni tofauti kabisa, mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake na si nyumbani."

Katika aya nyingine, Penny alitiririka na mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao limetawaliwa na misukosuko, walikaa chini kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja wao kufanya mambo yake, hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake kuwa sikutaki.

Alisema katika maisha huwa hapendi vitu vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya kwanza nchini China, hakuamini hadi walipokuja kukaa naye na kuzungumza ndipo walipoamua kupeana nafasi.

Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa Diamond amerudiana na Wema lakini yeye kwa sasa ‘bado yupoyupo sana', akakiri kuwa anatongozwa na watu tofauti na endapo ikitokea akaamua kuanzisha uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri, tofauti na zamani.

Chanzo: GPL

 
Kwa hiyo huyo Penny kayasema hayo kujiongezea umaarufu au hadhi mana lengo lake bado sijalibaini
 
Ndo ishakula kwako,saizi ndo unagundua kuwa huitaji mtu maarufu, kujisemesha ivo tu bado unaupenda umaarufu, alafu mara useme hakuna aliyemwambia mwenzie sikutaki,mara tumepeana muda kila mtu afikiri, mara tena nataka bwana asiye maarufu, kipi ni kipi....? Ila pole
 
Tushamsikiaa!!!! inaonyesha alipigwaa kibutii halafu bado anamsifia sifia angekua mtu makini angetulia na mwanamke mmoja inaonyesha dudu zao zina meno ndio maana domo hatulii mara huku mara kule
 
Tushamsikiaa!!!! inaonyesha alipigwaa kibutii halafu bado anamsifia sifia angekua mtu makini angetulia na mwanamke mmoja inaonyesha dudu zao zina meno ndio maana domo hatulii mara huku mara kule

wao ndo kama machizi chizi vile
 
Tushamsikiaa!!!! inaonyesha alipigwaa kibutii halafu bado anamsifia sifia angekua mtu makini angetulia na mwanamke mmoja inaonyesha dudu zao zina meno ndio maana domo hatulii mara huku mara kule

heeeeh kumbe kuna wanawake wana dudu.....

Majangaaaaaa
 
Wanawake ni watu wa hovyo hovyo sana,wakati mwingine hawana tofauti sana na wanasiasa.............hopeless kabisa
 
Wanawake ni watu wa hovyo hovyo sana,wakati mwingine hawana tofauti sana na wanasiasa.............hopeless kabisa

Tatizo umezaliwaa na mwanamke hujajishusha uwe na adabu kwa wanawake
 
Jipe moyo dada Penseli maana Diamond kwa Wema ndio Kigoma mwisho wa reli mamangu!
 
Umetudanganya Penny sio mtangazaji wa channel ten ni mtangazaji na meneja wa vipindi DTV
 
Back
Top Bottom