Penzi la dhati lililounda kampuni ya Benz

101 East

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
1,057
Reaction score
2,221
Ukizungumzia mafanikio ya mwanadamu mbunifu,mchakarikaji,Mjasiriamali na mfanyabiashara basi ndani yake mapenzi ya dhati kutoka kwa mwenza wake yanachukua asilimia 70 mpaka 80 kuwa ndo chachu ya maendeleo hayo.

Leo Tuangalie penzi la dhati la Bwana Karl Benz mgunduzi wa gari na muanzilishi wa kampuni ya kubwa duniani ya uundaji na utengenezaji wa magari na mkewe Bi Bertha Benz mvumbuzi na mbia muanzilishi wa kampuni ya BENZ

Karl na bertha benz walifunga ndoa tarehe 20 July 1872 na kubahatika kupata watoto watano ambao ni Eugen (1873–1958), Richard (1874–1955), Clara (1877–1968), Thilde (1882–1974), and Ellen (1890–1973).

Hapo mwanzoni kabisa Kabla ya kufunga ndoa na Karl Benz,bertha Ringer alikuwa ni bint mchapakazi Alietokea katika familia ya wafanyabiashara matajiri katika mji wa Pforzheim jimbo la Württemberg nchini ujerumani.

Bertha alikuwa anamiliki na kuendesha kiwanda na kinu cha kuzalisha na kutengeneza chuma ambacho hakikufanikiwa kutokana na ugumu wa mazingira ya kibiashara kwa wanawake katika kipindi hiko

Bertha alifamiana na Karl Benz mnamo 1871 ambapo bertha alikuwa na umri wa miaka 22 na Karl 27 na kuanza kumchumbia na mwaka Mmoja Baadae walioana.

HAYA NI MATUKIO MAKUU MATATU ALIYOYAFANYA BERTHA NA KUKUBADILISHA HISTORIA YA USAFIRISHAJI DUNIANI

KUTOA HELA YAKE YA MAHALI ILI KUENDELEZA KAMPUNI YA BENZ
Mwaka 1871 Karl Benz uliingia ubia na kuunda kampuni ya makenika na bwana August Ritter hata hivyo ndani ya mwaka Mmoja tu wa uanzishwaji wa kampuni hii biashara ili fail na kukatisha matumaini ya Karl Benz katika uvumbuzi wa auto mechanic hata hivyo Benz alimpatia taarifa hizo mchumba wake bi bertha na kuamua kutoa hela yake ya mahali ili kununua hisa za August ili wao kama wanandoa kuwa na umiliki wa wote wa kampuni.

BINADAMU WA KWANZA KUENDESHA GARI UMBALI MREFU.
Karl BENZ Mara nyingi alikuwa anaunda na gari aina tofauti tofauti lakini alikuwa anahofia kulijaribu katika umbali mrefu Kitu ambacho kiliwafanya wakose soko mbele ya gari zinazovutwa na farasi.

Kitendo hicho cha mumewe kilimnyima raha sana bi bertha kwani kila alipomshauri Karl BENZ alionekana kutoafikiana na mawazo yake.

Asubuhi ya mnamo 5 August 1888 bi bertha BENZ alikuwa na safari ya kutembelea mama yake mzazi.kutoka katika mji wa Mannheim walikokuwa wanaishi kwenda mji wa Pforzheim umbali wa kilomita 106.

Bila ya kumjulisha mumewe bi bertha aliamua kuchukua gari ya BENZ model 3 na kuanza safari kuelekea Pforzheim.

Alifanikiwa kufika Jioni ya siku hiyo na kumtumia ujumbe mumewe kwa njia ya telegraph kumpa taarifa hiyo iliomshangaza si tu Karl Benz bali hata duniani kote kwa Mara ya kwanza gari lilotengenezwa kwa vyuma lisilotumia farasi lilitembea umbali mrefu isivyotarajiawa.

Tukio lilireta Matokeo chanya katika utangazji na utafutaji WA wa bidhaa Hii mpya duniani kitendo kilichompelekea bwana BENZ kupata umaarufu na soko la magari duniani.

UGUNDUZI WA BREKI,GIA YA MLIMANI NA MFUMO WA KUPOOZEA.
katika safari hyo bi bertha BENZ alikutana na changamoto mbali mbali na kuzitatua bila kujua kuwa ndo alikuwa anafanya ugunduzi.

Katika miteremko mikali BREKI za mbao zilifeli kulisimamisha au kupunguza mwendo wa gari kutokana na kulika kwa haraka hivyo basi bi bertha aliamua kutengeneza BREKI padi za mpira(rubber).

Mara kwa Mara injini ilipata joto la juu sana na kupelekea kuweka tenki la maji la kupoozea injini ingawa kipindi hiko hili halikuwa rahisi kuaminiwa.

Katika miinuko mikali gari ilishindwa kupanda milima kwa kuwa haikuwa na nguvu hata hivyo alipokuja kumueleza mumewe Kuhusu Hilo bwana Karl Ben alilifanyia kazi na kugundua gia namba moja na mbili kwa ajili ya kupandishia milima.

Mafanikio makubwa ya kuitangaza na kuipatia soko gari za BENZ yameletwa na mwanamke Huyu shupavu alietengeneza historia ulimwenguni kwa mahaba na mapenzi yake ya DHATI kwa mumewe hakutaka mawazo ya mumewe na mtaji wao wa biashara upotelee hewani.

Mnamo mwaka 1925 Karl Benz katika kitabu chake cha kumbukumbu aliandika hivi "Only one person remained with me in the small ship of life when it seemed destined to sink. That was my wife. Bravely and resolutely she set the new sails of hope."

"Mtu pekee aliyebaki na mimi katika Jahazi hili dogo la maisha wakati lilipokuwa linataka kuzama ni Mke wangu,kwa ujasili na maamuzi alibadilisha uelekeo na kuleta matumaini"

Hili Ndio penzi la DHATI lililoanzisha kampuni ya magari ya BENZ

Natumai tumejifunza Kitu.

Asanten




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesisimka sana na hii stry!dadeq!
Kweli there's a power of woman!...walah tuombe uzima tu🤒!
 
Sizani kama ni kweli tz kuna couple zinafanya makubwa na mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app


Zipo mkuu! Kuna couple iko dar!mume yuko bank mama ni mjasiriamali!wanaenda china kuchukua mzigo fulan..ila hela transactions zote lazima zijulikane!yaan ile ni zaidi ya couple!mume anaheshim hela ya biashara..mke pia anaiheshim!
....wako mbal sana!naamini wana zaid ya 700m!
 
Nipe story kidogo kuhusu kuongezeka jina la Mercedes kwenye kampuni ya benz

Sent from my TECNO LC6 using Tapatalk
 
Sizani kama ni kweli tz kuna couple zinafanya makubwa na mazuri

Sent using Jamii Forums mobile app

Habari ni nzuri, na yaonekana kuwa ya kweli kwa asilimia kubwa. Lakini tujaribu kukileta kitu kwa uhalisia wake bila kupotosha mahala popote katika tukio husika. Story ni nzuri, lakini ina dosari mbili:

(1)Wakati anasafiri mke wa bwana Benz alipata changamoto ya braking system; ambapo umesema zilizowekwa mwanzo za mbao hazikuhimili mteremkoni na hivyo ikamlazimu abadilishe na kuweka za rubber akiwa safarini.
Sasa mtu anajiuliza alijuwaje kama atakutana na tatizo hilo na hivyo kujiandaa nalo kabla ya safari? Na hivyo vifaa aliwezaje kuvipata immediately akiwa safarini?

(2)Tatizo la pili akiwa safarini lilikuwa ni engine kupata joto jingi (overheat), unasema alifanikiwa kuweka tank kwa ajili ya kupoza engine. Sasa haya maji yalikuwa yanapoza vipi bila kuwa na mfumo madhubuti wa kupozea (cooling system)?

Mimi nadhani ungesema hizo changamoto alikutana nazo wakati anasafiri na aliporudi alimueleza bwana Benz na hivyo kufanya maboresho (modification) kama ilivyokuwa kwa gearbox.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…