Pole sana ndio kukua huko haya sasa umeshawajua na wewe anza kumtafutia timing umlipishe kisasi.
Mimi kuna m'moja alinizingua tukiwa wadogo, tulikuja kutana ukubwani. Ameshazalishwa watoto wawili baba tofauti hana ramani. Yupo huko mkoa. Nikawambia huwa nakuja sana hapo mkoa.
Mixer kuna siku nilienda hadi kwa wazazi wake maana dada yake alishakaa kwetu so akanialika na yeye akatilia uzito. Nikamnunulia mama yake kitochi cha nokia 105,na baba yake nikamnunulia infinix. Walizipenda sana zawadi zao.
Demu si akaanza kuloa na mimi tena. Nikasema utajua haujui. Yaani mimi huyo uliyenikomoa leo hii nikupe tena moyo, utajua haujui. Nikamshonea mtoto wake uniform na kumtumia viatu na begi. Yeye nikamkuta anakaa nyumbani kwao nikampangishia nikawa nafikia hapo nikienda mkoani manyara kwenye shughuli zangu.
Huku na kule demu kajaa mazima akawa mimi ndio tumaini lake. Kuna kipindi alileta story za kutambulishana kwao nikamwambia hilo nimekubali ila awe na subira.
Sasa hiyo kitu inamtesa sana. Ila angejua hata sio level zangu. Sasa nimeshamsindikiza sana na sasa ni mwaka unaenda wa 9 analalamika tu kuwa kama sina nia na yeye basi nimwambie. Huwa namwambia kama mwanzo anaona hakunikosea kwa kufanya maamuzi binafsi basi hata sasa anaweza rudia tena ila sitojali. Anakosa cha kufanya anabakia kuvumilia tu. Nimemshika pazuri pimbi yule. Na sina mpango nae. Nitamsindikiza hadi afike 45 au 50 kisha nampotezea mazima akileta lawama nampa makavu live kuwa yeye aliponitenda kipindi kile alinifikiria why yeye anataka kufikiriwa.