Katika maisha siku zote epuka kutembea na mke wa mtu; utakuwa salama kwa asilimia 80. Ukitaka kuona uchawi, ukitaka kuonja kifo, ukitaka kukosa mahali pa kuishi anza mchezo wa kutembea na wake za watu!
La kujiuliza hapa ni je wewe utakapokuwa umeoa na ukagundua kuna jamaa anatembea na mke wako, utamfanya nini? Basi hilo utakalofikiria ndilo nawe utafanyiwa.
Huyo mama ukizidi kuwa naye karibu halafu ukazidi kumkataa kama tunavyokushauri, ataamua kuvunja urafiki wako na mumewe kwa kumwambia kuwa wewe unamtaka, halafu itakuwa vagi kweli.
Acha kabisa kuwa nae karibu ikibidi punguza urafiki na mumewe. Kijana yaliwahi kutukuta sie!
Kumbuka, waweza kumchagua rafiki lakini huwezi kumchagua jirani