Penzi ni nini hasa

Jpinduzi

Senior Member
Joined
Feb 26, 2011
Posts
136
Reaction score
68
Penzi halina dawa, penzi halihusiani kabisa na kufanya ngono (hivyo kubinuka aina nyingi za mibinuko haina maana ndio utapendwa au unapendwa zaidi) penzi huja kiasili huhitaji kulazimisha wala kwenda kwa Mganga....Penzi huhitaji na huchukua Muda.

Lakini je, penzi ni nini hasa?

Watu wanasema penzi halielezeki au halina tafsiri maalumu kwamba kila mtu ana maelezo yake kuhusu penzi na maelezo hayo hutegemea zaidi na uzoefu wake.

Mimi nadhani penzi ni hisia zenye nguvu ya ajabu za mtu Fulani juu ya mtu Fulani, hisia hizo hazijalishi muonekano (mavazi, sura, umbile n.k), utajiri, umri, Elimu, aina ya maisha au tabia.

Hisia hizo humfanya mtu ashindwe kufanya mambo ya kawaida ambayo huyafanya kila siku kwa vile kichwani anakuwa anamfikiria yule ampendae, hisia hizo zinaweza kupelekea mtu kubadilisha personality na tabia yake hasa pale unapofanikiwa kuwa na huyo ampendae.

Unapofanikiwa kuwa/mpata yule umpendae huwa unapata raha ya ajabu kila unapomuona, inakuwa ngumu sana kuwa mbali nae. Hisia hizo zikikomaa hukufanya uhisi maumivu yake ikiwa anaumwa, umemuudhi au kaudhiwa na mtu mwingine, anapokuwa na huzuni mpenzi wako hakika utahisi huzuni n.k.
 
Mtasema mengi. Lakini kikubwa ni ku-do bana.
 
Kwa kifupi penzi ni hisia ziletazo raha na faraja ya moyo.
 
Ni kikohozi, na usipokohoa huna koo. Na kama huna koo maana yake huna kichwa.
 
mtoaa madaa i guess u inlove...ila mapenziii ni upepo,hatulioniii ila tuna feel,huwezii juaa rangii,shape ya mapenzi,ilaa linapo kupitiaa una hisiii limepitaaa,na upepo kumbukaa una pitaaa...so ndo maana mapenziii yanapitaaaa,naamini linalo dumu ni penzi la mama kwa mwanae
 
Tafsiri halisi ya penzi, anayo yule anayependa!
Kama unabisha muulize mtu yoyote mtu wako unampendea nini, kila mtu atatoa sababu zake tofauti!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…