Mi nadhani hizi nchi ambazo zinafuata misingi ya siasa za kijamaa, hakuna kitu kinacho itwa haki za raiya. Ni mara ngapi tumeshuhidia, hao tunao waita washukiwa wa uharifu wakipata kipigo wafikishwapo vituo vya Polisi?
Nani hakumbuki kipindi cha awamu ya kwanza ya uraisi Tz, raiya wengi walinyang'anywa mali zao kwa kisingizio cha wahujumu uchumi.
Nani hakumbuki pale JKT walipo ruhusiwa kusaidiana na polisi kulinda amani, na wakaanza kupiga raiya eti tu umekutwa na sabuni aina ya KODRAI au box la viberiti, dawa za meno (enzi hizo eti zilikuwa bidhaa adimu). Na mengine mengi ambayo yanaendelea mpaka leo hii.
Je ni wangapi leo hii wameshawahi kukamatwa na polisi bila kupigwa angalau vibao kama si mitama na ngwara!?
Ukikutana na polisi mstaarabu, akikufikisha kituoni, si ajabu kusikia aliyeko pale kauta, akikupokea kwa maneno makali... "yaani unarireta kituoni kama rinakuja arusini, ebu ripatie richai kwanza!"
Hapo ujuwe kibano, kisha ndio anauliza tatizo. Akigundua kuwa umekuja pale kituoni kuripoti kuibiwa ndio anajitia mstaarab, "sasa mbona ukusema mapema, iri ni rijeshi ra polisi bwana hatutaki muchezo"