mk4
JF-Expert Member
- Sep 11, 2012
- 285
- 328
Kumbuka miaka ya 90s kampuni ya vinywaji baridi ya pepsi ilipoteza soko Tanzania mpaka kupelekea kiwanda kufungwa kwa miaka kadhaa, sasa pespi wamekuwa na katabia kabaya sana ambacho wasipoanagalia watapoteza soko kama kipindi kile, mimi ni mnywaji mzuri wa kinywaji cha pepsi lakin ni kama mwaka sasa kila nikifungua soda ya pepsi unakuta chupa imevunyika kidogo kwa juu, utafikiri labda ni ufunguaji mbaya lakini nimejaribu mara nyingi lakini naona bado soda nyingi zimekuwa zina meguka kwa juu (sehemu ya mdomo wa chupa) nadhani tatizo ni chupa kuchakaa sana na wala kutofanya recycling kwa chupa zao kama wafanyavyo cocacola, mimi ni mnywaji mzuri wa kinywaji cha pepsi ningeshauri management iliangalie hili suala.