Personality ya Kikwete inatusaidia

- By kesho ninaweza kuwa angalau na makadirio, lakini kwa haraka haraka naamini angalau Dola kuanzia laki tatu mpaka tano, I could be wrong, lakini my experience na hii misafara inaniambia I am right.

FMES!
na wabunge wanaposafiri nje ya nchi wanatumia pesa ya nani? mfano nasikia malecela atakwea pipa kwenda majuu hivi karibuni......
 

Kwa ujumla nakubaliana na hoja zako ingawaje ningependa kujiridhisha zaidi katika haya:
Hivi kama ni usuluhishi wa Mgogoro wa Wakenya si mzee wetu BWM na Mama Mandela, Kofi Annan na wengine wangeweza kustahili pia sifa hizo kwa kuwa walikuwa pale fulltime wakati mkulu wetu alikuwa akiingia na kutoka, kama sijakosea sana?

Ni kweli Mh Rais hakuwa pale full time lakini tunajua kuwa isingekuwa rahisi kwake kuweka kambi pale katika kutatua ule mgogoro ilhali yeye pia anashughuli za kila siku hapa Tanzaia kama kiongozi wa nchi. Lakini alikuwa pia ni sehemu kubwa ya upatanishi ule kwani alikuwa akishiriki kwa kupewa mlishonyuma na kuweka mikakati ya pamoja na wale waliokuwepo katika field. Hata hivyo mara kadhaa alisikika akiongelea maendeleo ya upatanishi ule na pia aliweza kutoa kauli nzito kwa viongozi wa Kenya iliyoungwa mkono na Marekani hasa pale akina Annan na wenzie walipokatishwa tamaa na mchakato wa upatanishi uliosababishwa na viongozi wa Kenya waliokuwa wanavutana. Baada ya hapo wakenya waliendelea na majadiliano na akina Annan na Kikwete aliwajoin walipofikia hatua za kukamilisha.
Hata hivyo kwa vile thread hii ilibeba habari zinazomhusu JK basi ilikuwa ni sahihi to account kwa yale ambayo yalikuwa yanaendana sana na JK. Zaidi ya hapo pongezi za kufikia tamati ya mgogoro hazimwendei JK pekee zinawaendea wale wote walioshiriki katika usuluhishi ule ikiwa ni pamoja na viongozi waliokuwa katika mtafaruku.

Hii ya chati ya kupanua haki na Uhuru wa kujieleza si tunaweza tukampa zaidi mzee wetu Ruxa??

Ni kweli kuwa Mzee wetu Alhaj Mwinyi anahusika sana katika kuleta uhuru wa kujieleza na demokrasia. Kwani katika kipindi chake mfumo wa vyama vingi vya siasa ndiyo ulianza licha ya takwimu kuonesha kuwa wananchi wengi hawakutaka mabadiliko hayo. Lakini kama alivyopenda kusema Mzee Mwinyi kuwa 'Kula zama na kitabu chake' kwa maana kila uongozi una mambo yake maalumu inayafanya. Kwangu mimi nimeona kuwa tayari demokrasia imekuwepo lakini katika kipindi cha JK anafanya kazi ya kuipanua. Kwa mfano katika hotuba yake alipokuwa anahutubia bunge kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa rais alisema kuwa atahakikisha kuwa vyama vya upinzania vinapata nafasi ya kutosha ya kufanya kazi zake na kuiamsha serikali pale inapolalala. Tumeshuhudia hoja nyingi nzito zikitoka upande wa upinzani nje na ndani ya bunge, tumeshuhudia wananchi wanavyojitokeza kwa wingi katika chaguzi ndogo wakipiga kura kuchagua viongozi wa kambi za upinzani. Tumeshuhudia wananchi wakifanya harakati mbalimbali za kisiasa na wanasiasa kama vile 'operesheni sangara' nk. Tumeshuhudia mara kadhaa JK akipewa hoja za kum-critisize na hata za kumkejeli, lakini wakati wote ameendelea kusema kuwa ataendelea kupanua uhuru wa kujieleza na kusisitiza mapungufu yatokanayo ni kwa sababu ya uchanga wa demokrasia yetu. Hata kama amekuwa akichukizwa na baadhi ya kejeli, lakini ameonesha uvumilivu kwa kujua hali halisi ya uchanga wa demokkrasia yetu. Lakini pamoja na yeye kuvumilia ameendelea kusisitiza kuwa wananchi wajenge tabia ya kuvumiliana hasa pale wanapotofautiana kimitazamo na kuheshimu uhuru wa mtu mwingine. kwani uhuru wa mtu moja huishia pale ambapo wa mwingine unaanza.

Hili la Vita dhidi ya magonjwa ya Ukimwi na Malaria linaweza kukubalika ingawaje pia inawezekana pengine kina BWM walilifanya kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Suala la kupambana na vita dhidi ya magonjwa mbalimbali hili limekuwa likifanywa na viongozi wote waliokuwepo madarakani tena kwa ufanisi mkubwa sana. Tathmini yangu ni kuwa hakuna kiongozi aliyedharau kuweka nguvu kubwa katika suala hili la kupambana na magonjwa au sekta ya afya. Kila aliyekuwepo madarakani alijitahidi kutoa mchango wake mkubwa kadri ilivyowezekana. Hata hivyo, kiongozi anaweza kukosa sifa katika suala hili endapo hataweka msukumo katika yale yaliyoanzishwa na wenzake, kwahiyo basi pale alipofikia Mh Mkapa ndipo JK alipoanzia, swali je alipoanzia JK amepaacha kama palivyo? jibu ni hapana tumemwona jinsia ambavyo na yeye anavyolishughulikia kwa kulipa kipaumbele mkubwa.

Hili la Vita Dhidi ya Rushwa??.....Mmmmmmm??

Vita dhidi ya rushwa kwa kawaida duniani pote ni tatizo kubwa na inahitaji umakini wa hali ya juu katika kukabiliana nayo. Tathmini yangu ninaona kuwa Mh Rais yuko in the right track kwa maana kazi ya kupambana na rushwa inaendelee kwa ufanisi wa kuridhisha. Tayari kuna kesi ziko mahakamani zinaendelea, kuna baadhi zimekwishaamuliwa, na huenda kuna nyingine zitafuatia wakati wowote utaratibu wa kuzifikisha mahakamani utakapokamilika. Hata hivyo pamoja na tuhuma nyingi ambazo huwasilishwa katika Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa sio zote ambazo zinakuwa za kweli au kuwa na ushahidi wa kutosha wa kufikisha kesi mahakamani. Tanzania pamoja na mambo mengine inazingatia utawala bora na kuheshimu haki za binadamu. Si vizuri kumburuza mtu mahakamani endapo hakuna ushahidi wa kufanya hivyo kwani hilo litakuwa ni kosa la kutokuwa makini na kuzingatia haki ya za binadamu.

As for Chuo Kikuu Dodoma, haiwezekani kuwa hii ni mipango ambayo alipoingia Ofisini ilikuwa ni suala la kuikamilisha tu?? Tujuzane Mkuu!

Katika hili la mwisho nadhani linajibika kama lile la afya kwani JK anachofanya ndiyo sahihi kutoa msukumo wa nguvu katika suala la Elimu kutoka pale viongozi wengine waliopita walilifikisha. Kama angelirudi nyuma katika hilo basi tungemwona ameshindwa.

Kwa kumalizia Mkuu nimependa sana kujadili hoja zako kwani umetoa chachu ya kunifanya niende ndani zaidi katika kukujibu.

May God bless you!
 
Kwani personality ni kitu gani?

What Is Personality?

Almost everyday we describe and assess the personalities of the people around us.

Components of Personality
While there are many different theories of personality, the first step is to understand exactly what is meant by the term personality. A brief definition would be that personality is made up the characteristic patterns of thoughts, feelings, and behaviors that make a person unique. In addition to this, personality arises from within the individual and remains fairly consistent throughout life.

Some of the fundamental characteristics of personality include:

  • Consistency - There is generally a recognizable order and regularity to behaviors. Essentially, people act in the same ways or similar ways in a variety of situations.
  • Psychological and physiological - Personality is a psychological construct, but research suggests that it is also influenced by biological processes and needs.
  • Impact behaviors and actions - Personality does not just influence how we move and respond in our environment; it also causes us to act in certain ways.
  • Multiple expressions - Personality is displayed in more than just behavior. It can also be seen in out thoughts, feelings, close relationships, and other social interactions.
Kikwete pamoja na weakness zake ni lazima tukubaliane kwamba ana personality nzuri sana, kwa namna nyingine anaonekana kama president.
 
Kikwete pamoja na weakness zake ni lazima tukubaliane kwamba ana personality nzuri sana, kwa namna nyingine anaonekana kama president.



What this has to do with our life as Tanzanians? to hell wih his personality if he cant perfom his duty as a president ebo!
 
Ni bora kuwa na president mwenye sura kama ya Remmy Ongala lakini ana shusha nondo na kuwajibika kisawasawa.
 
..tafuteni video clip ya mdahalo wa IMF/WB uliofanyika Benki Kuu ndiyo mtaelewa wale wenye mashaka na uwezo wa Raisi wetu.

..kwa kweli wa-Tanzania tuliaibika kutokana na performance ya Raisi wetu. ilifika mahali washiriki ktk mdahalo, ambao ni wageni wake[Kikwete], na amewazidi kiwadhifa na kiuzoefu, wakawa wanapangua na kukosoa hoja za Raisi wetu waziwazi bila hata kutumia lugha ya kidiplomasia.

..sijui Trevor Manuel, Dr.Kaberuka, Dr.Ngozi Okonjo, na washiriki wengine wa mdahalo, pamoja na wale walihudhuria mkutano ule, walikwenda kutoa taarifa gani kwa wakubwa wao kuhusu Raisi wetu.
 
Ni sawa kabisa Pundamilia lakini wengine hawaoni ni watu wenye uelewa Duni kabisa.Nashaka hata kama wanasoma magazeti yetu wanasikiliza habari katika redio na TV zetu, pengine huangalia mchezo wa redio ndio maana hawaoni jinzi TZ inavyopiga maendeleo.Badala yake kuteremsha matusi dhiidi ya Rais wetu.
 

In my life, I will avoid to make such kind of comment, however will you tell these 'uelewa duni watu' what makes you to think Tanzania is developing? any proof?

Mkuu, umesema vizuri kuwa watu pengine hawasomi magazetI, kufuatilia TV etc, lakini kwa uelewa wangu mdogo sana inaonyesha Europe walikuwa na mapinduzi ya viwanda karne ya 17 na 18, ikawafanya kuja Afrika kutafuta malighafi!

Hivi TANZANIA kuna mapinduzi ya viwanda yaliyowahi kwisha kufanyika?? lini na wapi, viwanda vinhi vya wageni, let we are in globalisation era, only competetion with other developed countries ni kuwa na viwanda vingi!



Viwanda gani tulivyonavyo? au kujenga mahoteli, majengo marefu ya kupanga, internet surfing, kuangalia Manchester na Barcelona ndio maendeleo? kuua kilimo kwkako wewe ni maendeleo??

umeshawahi kuwaza mtu wa kawaida wa Tanzania atakuwa na hali gani miaka 50 ijayo, wakati kila kitu kinaenda kwenye ubepari, huku hakuna nguvu zozote za kumuinua huyu mtanzania wa kaiwada ili awe katika global stage of competition??


Muanzisha maada alichosema ni kuwa amemtukana rais, RAIS SIO MR.TANZANIA huyu!
 

Kwenye jukwaa la lugha kuna mada kuhusu kingereza cha kitanzania! Nimepata kusikia watz wengi tu wakilitumia neno 'personality' (kwa makosa!) kama jinsi mleta mada alivyolitumia. Tatizo watanzania tunahusudu sana lugha za kigeni hata pale tunapoweza kujieleza vizuri zaidi kwa lugha yetu ya kiswahili.

Mtoa mada angesema tu 'Sura ya Kikwete inatusaidia'🙂, tungemwelewa pia.
 

hebu toa mifano basi ku-backup your points
 
mi najuta kuwa na rais wa namna hii.sina la kufanya nabaki kucheka tu
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…