KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Nimekuwa nikiamini ktk mafunzo ya aina mbili hapa duniani..
Moja ni kufunzwa na watu/mtu.
Na pili ni kufunzwa na dunia/mazingira.
Ni vyema kuutumia uwepo wetu wa ufahamu ktk kujifunza,kuelimika na kutenda.
Sio kwamba naifahamu pesa kiundani sana!,la hasha!.. ila nimeikuta lkn pia kuikuta haimaanishi nisiijue!.
Pesa tunaitafuta ili tutatue vinavyoweza kutatulika na pesa.
Lkn je, ulishawahi jiuliza pesa inataka nini?
Nimeshashuhudia watu wakiwa na pesa na tena kurudi chini Kama alivyokuwa jana!..
Hata wewe unaesoma hapa unaweza ukawa shuhuda wa wewe mwenyewe au mtu mwengine!.
Tunaweza kuteleza mara moja au mbili na tukainuka jumla ila sio wote wanaoweza kuinuka!..
Pesa inataka kile ambacho haukukijua wakati unaanguka!!.
Kuwa na pesa kunahitaji uwe na elimu juu ya pesa ili uweze kuimudu pesa hiyo!.. Ni sawa na kusema uwe na pikipiki wakati hujui kuiendesha hapo kaa ukijua utaanguka tu!!..
Pesa inahitaji elimu ambayo itakufanya ujue kwanini pesa..?
Kwanini utumie pesa..?
Kwanini utafute pesa..? Na swala la msingi zaidi ni kivipi utaitumiaje pesa kupata pesa..?
Hapa wengi tunaanguka!..
Labda nitoe mfano huu ili nieleweke vyema.. mtu unasomea ualimu but ukimaliza unakuta ajira huku mtaani hola!.
Unapambana unafanya vitu vyako unajichanga then unaanzisha biashara but huna elimu ya biashara!.. kaa ukijua huko ni sawa na kubeti na kwenye kubeti huwa kunamatokeo mawili.
Pesa inahitaji taarifa sahihi..
Ili uweze kuimudu pesa yako ktk kukuletea pesa ni lazima uwe na taarifa sahihi ilikusudi uweze kufanya maamuzi sahihi..
Ukitaka kufanya biashara kaa ukijua sio mtaji tu ndo utakuletea faida au mfanyakazi mzuri ama huduma nzuri n.k hayo sio pekee tu!.. taarifa ya nini kinahitajika,muda gani,mahali gani na kivipi huo ndio msingi wa kwanza utakaoweza kukuletea pesa kwenye pesa.
Pesa inahitaji nidhamu..
Ulishawahi kuona mtu fulani akipata fedha anabadilika..?
Huyo anaweza kuwa ni wewe au Yule ama Mimi!!
Ndio pesa hubadili tabia ya mtu hata kwa nusu saa tu!.. kutokuwa na nidhamu ya fedha ndipo hufanya kujiuliza kuwa pesa hii imeishaje??!
Pesa inahitaji nidhamu ya aina yake haswa kwenye utulivu wa akili,hupaswi kuwa mwenye pupa katika utumiaji wa fedha kwa maana fedha inahitaji swali kwanini kwa mtumiaji makini.. ila inahitaji upumbavu kidogo tu ili ikupeperuke!.
Ipo hivi Kama utaendelea kureact tabia zilezile za matumizi mabovu jua kamwe hautabadili chochote.
Pesa inahitaji uvumilivi..
Uvumilivi kwa maana nyengine ni muda.. na sio muda tu bali muda muafaka na sahihi!..
Wengi wao tumekuwa tukishindwa kuwa wavumilivu haswa pale tunapopata miburungutu.. sometimes pesa inahitaji kutunzwa tu ama kuwekezwa huku ikisubiri muda muafaka na sahihi ili ije iungane na taarifa sahihi zenye nidhamu, uvumilivi ili iweze kuja kuleta pesa nyenzake..
Naomba niishie hapo.. mengine tutaelewashana kadri mjadala unavyoenenda..