Pesa ni M-Pesa, Lipa kwa M-Pesa pata zawadi za papo hapo

Umeshawahi kufanya malipo kwa kutumia huduma ya Lipa kwa M-Pesa?

  • Total voters
    24
  • Poll closed .
Voda matapeli tu! Unaweka mb alafu wanaziiba wanakwambia zimeisha ndani ya mda kidogo
 
Voda kwenye utapeli nawapa 100% mnajitahidi kutuibia nimenunua Umeme toka mwezi wa 10 hadi leo hamja nitumia Token elf 50,000 ndio mmeniibia sio?

Voda wezi totaly mbs zao zinapukutika kama maji
 
Kwann mnapindisha ushahid kwa Kuuza namba ya BEN SAANANE wakat mnajua taasisi nyeti Za upelelez bado hazijatoa ripoti yeyote juu ya swala hili majibu tafadhari
 
Kwanza niwapongeze Vodacom Tanzania kwa kukimbia maswali ya waulizaji walotangulia, mnastahili tuzo kwa hilo[emoji2][emoji2]..
Swali la msingi Nawezaje zuia sms yenu ya PESA NI MPESA, BIKOSPORTS,TATUMZUKA zisiingie kwenye simu yangu?..
 
Voda nyie voda
Mungu anawaona
Yaani gharama za utoaji na utumaji Mpesa mko juu sana,acheni utapeli bwana maisha magumu msimnufaishe mkoloni.
Halafu niliwahi kosea kuhamisha hela kwa simbanking mkanizungusha mpaka nikawaachia,Haya chukueni bhana mfaidi.
 
Internet service yenu kwa sasa ni mbovu sijapata ona...rekebisheni hili
 
Mi toka 2007 natumia Voda hata zawad ya laki moja nikale Bata bad
Yaan me mama angu tangu enzi za Motorola Mshindi mpaka leo yupo voda, hata ofa ile special hakuna.....
mimi natumia mtandao fulan tangu mwaka 2008 mpk sasa, napewa ofa kibao kwa kua ni mteja wa siku nyingi na wakudumu, hua hadi pesa wananiwekea.
Voda hawajui kabisa kumshukuru mteja, inashangaza.
 
Voda kwenye utapeli nawapa 100% mnajitahidi kutuibia nimenunua Umeme toka mwezi wa 10 hadi leo hamja nitumia Token elf 50,000 ndio mmeniibia sio?

Weeeeh! una wachekea hao, elfu 50 ziondoke hivi hivi hahahaha me buku 5 tu nilipigia simu nikasema nikija huko ofisin kwenu mtalipa gharama zangu zote hadi muda wangu, baada ya dakika 5 wakatuma, ukiwachekea hawakupi kweli.
 
Hivi nyie vodacom kwann hamtoi special offer kwa wateja wenu wa muda mrefu?? mfano wenye namba 0754 obviously ni wa zamani kwanini hamjui kuwashukuru wateja wenu kwa kukaa na nyie miaka yote hiyo?? au kuna vigezo gani hua mnavifanya.
wakupe zawadi ya fala wao waliyemnyonya
 
vodacom, kwanini hamuanzishi huduma ya kulipa kwa mpesa online? kwa mfano, duka mtandao, ninauza vitu vyangu, ninayo website, watu wataviangalia na kuchagua, watalipia kwanza na automatically baada tu ya pesa kuingia kwenye account yangu mtu huyo atapata hiyo huduma. naongelea kama wanavyofanya amazon, alli express etc. yaani, transaction zinavyofanyika mpesa inaungana na account za benki zetu hivyo hamna haja ya kufanya kwa manual kama ilivyo kwa sasa. huduma hiyo ina ugumu gani kwetu au ni sababu gani, hamna uwezo au technologia kama hiyo bado kutokea? thanks.
 
Kila nikituma hela wanasema nimezawadiwa MB15 kumbe ni MB hewa. Vodacom acheni utapeli.
 
Hivi nyie vodacom kwann hamtoi special offer kwa wateja wenu wa muda mrefu?? mfano wenye namba 0754 obviously ni wa zamani kwanini hamjui kuwashukuru wateja wenu kwa kukaa na nyie miaka yote hiyo?? au kuna vigezo gani hua mnavifanya.
Hala vodacom malofa Sana kuna package yao ya pata double.... Nilikuwa najiunga kwa buku mbili napewa double baada YA Wiki kazaa wakapandisha dau natakiwa nijiunge kwa 10000 ndio napewa double. Sasa hvi nimeamia halotel...... Wabinafsi sana
 
ngoja nkulu aje ajibu kuwa umezawadiwa m8 kisha ushangilie baada ya kuulizwa unafanya kazi gani
 
Hivi nyie vodacom kwann hamtoi special offer kwa wateja wenu wa muda mrefu?? mfano wenye namba 0754 obviously ni wa zamani kwanini hamjui kuwashukuru wateja wenu kwa kukaa na nyie miaka yote hiyo?? au kuna vigezo gani hua mnavifanya.
Wanawake kila mahali mnataka ofa bar ofa hitelin ofa nyumban ofa vyuoni first class ofa sasa mpaka bundle mnataka za ofa loooh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…