PESA NI SILAHA; VITA YA MAISHA. MBINU ZA KIMEDANI. CHUKUA MOJAWAPO!
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Kuna mahitaji yanayoleta kuhitajiana.
Kuhitajiana kunakoleta mahusiano.
Mahusiano mchezo wa maslahi.
Maslahi yenye kutimiza ndoto na malengo ya watu.
Mahitaji ni tafsiri ya utegemezi, upungufu na kutokukamilika.
Mahusiano na muingiliano wa watu. Huyu anahiki lakini hanakile. Anahitaji kile cha mwenzake kwani kwake ni hitaji.
Yapo mahitaji ya lazima,
Yapo mahitaji ya Muhimu,
Yapo mahitaji ya anasa.
Mahitaji ya mwili huleta vita ya nje ya kimwili. Kupigania rasilimali ambapo huitwa mahitaji.
Kwenye vita kuna silaha.
Katika vita ya maisha ya kupigania rasilimali silaha kubwa zaidi inayotegemewa ni PESA
Pesa ni silaha ya uhakika katika kukupa ushindi wa rasilimali.
Kadiri unavyokuwa nayo ndivyo ushindi wako katika vita ya maisha unavyoongezeka.
Elewa, mwanadamu ameumbwa akiwa mhitaji. Asilimia kubwa ya mahitaji ya mtu yapo kwa watu wengine.
Kuanzia elimu, ujuzi, akili maarifa, huwezi kumiliki elimu zote. Ila pesa itakusaidia kutumia elimu na ujuzi, na maarifa ya watu wengine.
Zingatia Kwenye vita hakuna Msamiati HURUMA.
Vita ni silaha.
Silaha ni matumizi,
Kwenye vita kuna kanuni nyingi lakini kanuni namba moja ni USHINDI NI USHINDI bila kujali ushindi huo ni haramu au halali.
Kwenye vita yoyote target ya mashujaa ni ushindi tuu. Kwa mbinu na gharama zozote.
Ikiwa ushindi ni ushindi katika Vita hii itamaanisha Silaha utatumika yoyote ilimradi ushindi upatikane.
Pesa ni pesa bila kujali imepatikanaje.
Ingawaje kimaadili inaweza isiwe na maana nzuri lakini kwenye pesa kanuni zake kidogo ziko complicated.
Kwenye vita hakuhitaji Sana maadili. Kwa sababu vita yenyewe sio maadili.
Vita ni kinyume kabisa na maadili.
Ukishasikia neno vita basi jua upo kwenye rank ya juu ya ukosefu wa uadilifu, upo kuzimu, ndio maana ushaambiwa vita haina Macho.
Huwezi leta maadili yako kwenye vita. Vita haina huruma.
Ukitaka Amani jiandae kwa vita.
NA vita ni;
silaha.
Mbinu.
Ujasusi
Propaganda n.k
Pesa kama silaha zingine katika vita za maisha inahitaji mambo yafuatayo ili uwe nayo;
1. Mkondo mkubwa wa kuvuta pesa na kuteka pesa za wengine zije kwako.
Lazima utengeneze Strong Channels ambazo zivute pesa kwa watu wengine zije katika mkondo wako
Money piracy ni kanuni muhimu Sana katika upatikanaji wa pesa.
Strong channel unasifa zake lazima uwe na uwezo wa kuteka channel zingine iwe kwa hiyari au kwa nguvu ziingize pesa kwako.
Kwenye Jiografia kuna kitu kinaitwa River Capture na kwenye River capture kuna mchakato unaitwa River Piracy.
Kwenye pesa kuna Money Capture, na mchakato unaoitwa Money Piracy.
Katika uharamia wa pesa ambapo Mkondo mkubwa wa pesa unameza mikondo midogo ndio hupelekea watu wengi kujiingiza kwenye serikali na madaraka kwa sababu huo ni sehemu ya mikondo mikubwa ya fedha.
Jinsi ya kuchimba Mkondo wa Fedha
1. Lazima ujue pesa ni silaha na sio Mungu hivyo pesa haiabudiwi ila inatumika kama silaha.
Silaha inatafutwa, inalindwa kwa gharama zozote, na inatumika kwa matumizi yanayofaa.
Wengi huiabudu pesa badala ya kuitumia vizuri na kuilinda.
2. Rafiki zako wa sasa huamua pesa yako ya baadaye.
Vk
Kama unampango wa kuwa na kipato Fulani basi elewa kipato chako kinaathiriwa na wanaokuzunguka.
3. Kuwa the best katika eneo lako la ujuzi unalotoa huduma.
Jitahidi kila siku kuwa bora kuliko yeyote katika eneo lako la ujuzi. Kama ni Fundi nguo hakikisha eneo ambalo upo wewe upo kwenye top ten. Kisha pambana uwe top 3 kisha itafute namba Moja.
4. Tengeneza uhitaji wa watu kwako(jipe thamani)
Ukishakuwa best automatic watu watakuhitaji. Kadiri watu wanavyokuhitaji ndivyo thamani yako inavyoongezeka. Kadiri thamani yako inavyoongezeka ndivyo mkondo wako wa pesa unavyokuwa Mkubwa.
5. Linda Reputation yako.
Zingatia competence= Confidence
Kadiri unavyokuwa mahiri ndivyo kujiamini kunavyoongezeka.
Umahiri na weledi hautoshi bila uaminifu.
Ni jukumu lako kujenga na kulinda reputation yako.
Sifa njema watu wanazokujua nazo hakikisha unazilinda. Hizo ndio pesa zako.
Huduma unayoitoa ibaki kwenye ubora uleule.
6. Don't focus on what you can't Control
Usizingatie wala kufuata mambo ambayo huyawezi au huwezi kuyadhibiti.
Jambo lolote ambalo unajua kabisa huna nguvu za kulidhibiti usijiingize kwalo.
Kwenye uharamia wa pesa huwezi mfanyia mtu aliyekuzidi nguvu. Utajikuta were ndiye unafanyiwa uharamia. Unakuwa captured na kuwa mhanga
7. Kwenye pesa Hakuna adui.
Utakachoangalia ni maslahi yako tuu. Fanya biashara. Angalia faida. Maswala ya kususa susa au kuleta hasira kwa baadhi ya watu ambao unaweza kushirikiana nao kupata pesa zaidi ni dalili hauna akili za kushinda vita ya maisha.
Umaskini ndio adui yako.
8. Usioe Mwanamke Maskini
Kumbuka mwanamke ni mwadani wako. Anaweza kuwa adui namba moja kwako.
Elewa mwanamke ni moja ya rafiki au MTU wako wa karibu. Future ya pesa zako pia zitaamuliwa na mwanamke utakayemuoa.
Kwenye familia kubwa Kuoa na kuolewa NI moja ya vitu vinavyoangaliwa Sana kwani huathiri uchumi wa familia kwa namna chanya au hasi.
Mwanamke maskini sifa yake kuu ni tegemezi. Pili anategemea uzuri wake na Hana cha ku-offer zaidi ya Ngono.
9. Tengeneza Network yenye tija.
Kuanzia kwenye serikali, mashirika, wataalamu, viongozi wa dini, wafanyabiashara.
Hakikisha network yako umeiseti vyema kabisa.
Uwe na tija kwao. Yaani uwe na chaku-offer kwao ndio maana nikakuambia hakikisha uwe the best katika eneo lako.
Lakini pia wajivunie kufahamiana na wewe kwani unatija kwao kama wao walivyo na tija kwako.
Jinsi ya kutengeneza Network;
a) Kuza huduma, kipaji, karama na ujuzi wako. Kihitajike.
b) kuza jina Lako.( Brand yourself)
c) Chunga Mdomo na uume/Uke wako.
Ukiweza kuchunga hayo mambo mawili upo kwenye nafasi nzuri
Sio kutanguliza ngono. Binti umeitwa kwenye mkutano au kongamano Fulani, unaombwa namba, usitaniwe kidogo unaachia mapaja kikahaba. Au hujataniwa lakini unajilegeza legeza kijinga.
Binti lazima uelewe saikolojia ya sisi wanaume. Sisi kukutongoza kwa sehemu kubwa tunakutania au kukujaribu tuu. Hatumaanishi.
Na kijana sio umekutana na mwanamama au dada amenyooka, pesa IPO. Anang'aa! Anakuchangamkia kwa ukarimu wewe unawaza ngono tuu. Unamletea upuuzi wako. Network haijengwi hivyo. Huko ni kujichoresha.
Unaombaomba pesa kama mjinga.
Unalialia shida. Hivi Nani alikuambia anahitaji kusikia shida za wengine. Kama were hutaki shida zako Nani anazitaka. Wewe ndio mwenye wajibu wa kupambana na shida zako. Kutangaza tangaza matatizo yako ni kuua network ambayo ungeitumia kwa mambo mengine ya msingi.
Unalaumulaumu watu wengine. Unaeleza jinsi ulivyoonewa au kudhulumiwa lakini huelezi madhaifu yako. Nani atataka kuwa karibu na MTU WA aina hiyo?
d) Shiriki kwenye shughuli na matukio ya kijamii, kisiasa na kiuchumi
Usijifungie ndani, shiriki ushirikishwe.
Nenda kwenye shughuli na matukio yanayohusu kile unachokifanya.
Onyesha ambacho unaweza kufanya chanye manufaa kwa wengine. Kuwa na tija.
Kamwe usiwe mtu wa kalaumu wengine.
e) Usifosi kukubalika.
Usilazimishe watu wakukubali. Sio KAZI yako.
Kazi yako ni kuonyesha uwezo, ujuzi, na kile kizuri ulichonacho.
Kwa kumalizia, kupata pesa sio tatizo ila matumizi ya pesa ndio tatizo la wengi.
Acha nipumzike, ratiba leo ni ugale, dagaa Mlenda. Wenye kupenda karibuni.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam