Wanabodi nawasalimu kwa heshima.
Naomba nitoe pole kwa wanajamvi wote kwa mihangaiko ya hapa na pale.
Pili naomba niwaeleze serikali yangu kua kila senti wanayolipwa hawa vijana wetu wailipie kodi ili serikali ichukue chake na wao wabaki na chao.
Kwa mfano msanii wa muziki ana show masasi na mwandaaji au promoter wamekubaliana kulipana milioni 10 kwa show hiyo, inatakiwa TRA ya masasi ihakikishe imepata 18% ya hiyo milioni kumi ndio tutaweza kukuza sanaa yetu.