Pesa za Bure Zasababisha Vurugu

Pesa za Bure Zasababisha Vurugu

Nyundo_tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
640
Reaction score
20
November 16, 2009

Maelfu ya watu nchini Ufaransa waliokuwa wakisubiria kwa hamu kujipatia pesa za bure ambazo zingetolewa na website moja nchini humo walianzisha vurugu kubwa baada ya website hiyo kushindwa kufanya hivyo.

Watu zaidi ya 7,000 waliokuwa wamekusanyika kwenye mnara wa Eiffel jijini Paris wakisubiria kupewa pesa za bure, walianzisha vurugu kubwa na kupindua magari yaliyokatiza mbele yao baada ya kukasirishwa na hatua ya website iliyotangaza kugawa pesa za bure kuahirisha kufanya hivyo.

Ghasia hizo zilianza baada ya kampuni ya internet ya Rentabiliweb kushindwa kugawa dola 64,000 kama ilivyoahidi kwenye mtandao wake.

Rentabiliweb iliahidi kugawa mapochi 5,000 yakiwa na pesa kati ya dola 7 na dola 799.

Watu 10 walikamatwa na polisi na tisa kati yao walihifadhiwa rumande kufuatia ghasia kubwa zilizosambaa kwenye mitaa mbali mbali ya Paris.

Vijana wenye hasira waliofika kwenye eneo hilo kujipatia pesa za bure, waliwashambulia polisi walioizuia kampuni hiyo kugawa pesa zake.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba iliiamuru kampuni Rentabiliweb kuahirisha tukio hilo kwakuwa watu wengi sana walijitokeza na kusababisha hali ya usalama kuwa duni.

Rentabiliweb ambayo inamiliki pia tovuti ya Mailorama.fr ilisema kuwa pesa ambazo walikuwa wamepanga kuzigawa bure, zitatolewa kwa mashirika ya hisani.


Source: News Agencies
 
Back
Top Bottom