Pete ya ndoa!

Pete ya ndoa!

BORNCV

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
242
Reaction score
46
Hivi kwa nini pete ya ndoa inavaliwa mkono wa kushoto, mkono wa kulia inakuwaje?
 
Hii ushasema mkono wa kulia alafu unataka ubebe maurembo kwenye swali lako kuna jibu mbona.
 
Pete ni pete ! Ivae kwenye kidole gumba, vidole vya miguuni haitobadili maana kutoka kua pete ikaitwa jina jingine.
Na kidole mahsusi kwa Pete kiwe kimevikwa pete ama laa kitabaki kuitwa kidole cha pete.
 
hata mkono wa kulia pete za ndoa zinavaliwa, mi nshaona watu kibao.
 
Ni makosa kwa pete ya ndoa kuvaliwa kidole cha mkono wa kulia.
Wengi huvaa pete (hata wale wanaovaa katika kidole sahihi) lakini hawajui maana yake halisi.

Nijuavyo mimi sababu kubwa ni hizi:
1. Inasemekana kati ya vidole vyote kumi vya mikono ya mwanadamu (normal person), kuna mshipa mmoja tu wa damu uliotoka moja kwa moja kwenye kidole hicho cha mkono wa kushoto hadi kwenye moyo (Vidole vingine vina mishipa lakini haijaenda moja kwa moja kwenye moyo bali imetengeneza matawi wa arteri kutoka mahali fulani).
Na kama tunavyojua kuwa moyo ndio kama ishara ya feeling za upendo, wayahudi walivalishana pete katika kidole hicho kama ishara ya upendo. Na hii ikaendelea hadi leo japo wengi hawajui maana yake na ilianzaje.

2. Katika hali ya kawaida mnapotaka kuvalishana pete (watu wengi ni right handed), mkono wa mpenzi/mwanandoa mwenzio unaoweza kuukabili kwa haraka na kwa wepesi ni mkono wa kushoto hivyo ikawa rahisi zaidi kwa watu kuvalishana pete katika mkono wa kushoto.
 
Mkono wa kulia haupatani na uwongo, kwani ndoa nyingi zimetawaliwa na uongo mwingi, hivyo unatumika mkono wa kushoto kwa sababu huo hauna tatizo na uwongo..............
 
hahaha nimeipenda hii!
 
Weeh dingi siku hizi hicho kijiwe kipya cha kahawa ungekihama! Kwa hiyo wewe unamdanganya maza? Kesi ya 2 kwa leo!
Mkono wa kulia haupatani na uwongo, kwani ndoa nyingi zimetawaliwa na uongo mwingi, hivyo unatumika mkono wa kushoto kwa sababu huo hauna tatizo na uwongo..............
 
Mkono wa kulia haupatani na uwongo, kwani ndoa nyingi zimetawaliwa na uongo mwingi, hivyo unatumika mkono wa kushoto kwa sababu huo hauna tatizo na uwongo..............
Hii inakaribia kufanana na ukweli...
 
Mkono wa kulia haupatani na uwongo, kwani ndoa nyingi zimetawaliwa na uongo mwingi, hivyo unatumika mkono wa kushoto kwa sababu huo hauna tatizo na uwongo..............
Kabisa kabisa ndo nyingi sana zimetawaliwa na uwongo, lakini usisahau kitu nani muongo pale, ni mkono au mdomo.

@thread poster, pete ni tamaduni tu, haina umuhimu wowote.
 
Nafikiri ni kwa sababu mkno wa kulia unatumika kwa shughuli nyingi ikiwemo kulia chakula, kusalimiana, kusafishia vitu mbali mbali, nk hivyo pete ingevaliwa kulia ingeleta a lot of inconvinience! Imagine umeshika nyundo unapigilia bati au unanyoosha bati au unapasua mawe na mkono huo huo umevaaa pete, ni ngumu kidogo!
 
Nadhan ni mapokeo tu. Mimi nimeona nchi za Scandinavian wao wanavaa pete ya ndoa kwenye mkono wa kulia. Sijafuatilia kujua sababu ila nadhan inatokana na mapokeo yao hasa kwenye imani sababu majority ni Christians.

Hivi kwa nini pete ya ndoa inavaliwa mkono wa kushoto, mkono wa kulia inakuwaje?
 
Nafikiri ni kwa sababu mkno wa kulia unatumika kwa shughuli nyingi ikiwemo kulia chakula, kusalimiana, kusafishia vitu mbali mbali, nk hivyo pete ingevaliwa kulia ingeleta a lot of inconvinience! Imagine umeshika nyundo unapigilia bati au unanyoosha bati au unapasua mawe na mkono huo huo umevaaa pete, ni ngumu kidogo!

Au unapikicha vipikichwavyo viliokua laaiiyni , pete disturbance !
 
kwa mkono wa kushoto haukabiliana na mikiki mingi..mkono wa kulia uko busy kuliko mkono wa kushoto..kwa wale wanaotumia mkono wa kushoto inakuwaje?
 
1. Inasemekana kati ya vidole vyote kumi vya mikono ya mwanadamu (normal person), kuna mshipa mmoja tu wa damu uliotoka moja kwa moja kwenye kidole hicho cha mkono wa kushoto hadi kwenye moyo (Vidole vingine vina mishipa lakini haijaenda moja kwa moja kwenye moyo bali imetengeneza matawi wa arteri kutoka mahali fulani).
Na kama tunavyojua kuwa moyo ndio kama ishara ya feeling za upendo, wayahudi walivalishana pete katika kidole hicho kama ishara ya upendo. Na hii ikaendelea hadi leo japo wengi hawajui maana yake na ilianzaje.

Alaa.. Kumbe ndio maana ukienda hospitali kupima damu huwa wanang'ang'ania kidole hiki..
 
Back
Top Bottom