Pete ya uchumba

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Hivi haya mambo ya pete ya uchumba yalianzia wapi na maana yake nini? Ni lazima kumvisha mchumba pete ya uchumba (engagement ring?

Kuna dada mmoja aliona vidume vinamzingua akanunua pete akampa kijana mmoja aliyekuwa anakula naye maraha amvalishe. Kuna sababu ya msingi ya kusumbua akili (to be obsessed) kiasi hicho?
 
Wala haina maana yoyote siku hizi zamani ilikuwa inamaanisha kuwa thatt one is already taken but nowdays even wasiokuwa taken wanazivaa na wale walokuwa tayari taken wanazimisuse...wakiruhusu kuinfidelate na wasiowavisha.
 
ni mampambo tu sasa maana yake ishakwisha long ago
 
Sijui siku hizi ila kwa nini akina dada walikuwa wanalishikia kidedea hilo suala. Kwenye miaka 90 nilikaribia kulimwa kubuyu baada ya kumwambia GF wangu kuwa sioni maana ya engagement ring.

Pia na huyo dada (alikuwa school mate wangu) ambaye aliamua kujihudumia baada ya wanaume kumzingua. Nadhani wasichana walikuwa wanahangaikia hizo pete au?

ni mampambo tu sasa maana yake ishakwisha long ago

Inawezekana kwa sasa. Siwezi kujua kama hali ya zamaini imeisha, kwani nilishastaafu kustaafu hayo mambo zaidi ya decade moja iliyopita.
 
Inawezekana maana yake imeanza kupotea lakini bado ina umuhimu wake, kwa wanao heshimu ni alama ya upendo mkuu na kwa wasio heshimu atleast wanajua kwamba wanaiba vya watu so wanakua waangalifu
 
Inawezekana maana yake imeanza kupotea lakini bado ina umuhimu wake, kwa wanao heshimu ni alama ya upendo mkuu na kwa wasio heshimu atleast wanajua kwamba wanaiba vya watu so wanakua waangalifu

siku hizi utakuta hata watoto wa shule wamejivalisha wenyewe hapo utakuwa unamuibia nani kama utajitwalia mwanakondoo?
 
siku hizi utakuta hata watoto wa shule wamejivalisha wenyewe hapo utakuwa unamuibia nani kama utajitwalia mwanakondoo?

Haaaaaaaa FL1, hayo ya kweli kabisa?

Ila kwa jinsi hiki kizazi kilivyokengeuka na kuchakachuliwa siwezi kushangaa.

Kazi tunayo watu wa miaka ya 47!
 
Ni kama urembo vile. huwa inapendezesha kwenye vidole vya wadada. Siku hizi haimaanishi kuwa mvaaji ameshabukiwa.
 
Ni kama urembo vile. huwa inapendezesha kwenye vidole vya wadada. Siku hizi haimaanishi kuwa mvaaji ameshabukiwa.

Kwa maneno mengine imepoteza maana yake, au? Sasa kwa nini watu wanaendelea kuwapa wachumba wao?
 
Nimepata hayo maelezo kutoka kwenye mtandao.

Wala haina maana yoyote siku hizi zamani ilikuwa inamaanisha kuwa thatt one is already taken but nowdays even wasiokuwa taken wanazivaa na wale walokuwa tayari taken wanazimisuse...wakiruhusu kuinfidelate na wasiowavisha.

n kuna ambao wanawavalisha wanzao then wanawaacha kwenye mataa. yaani hiki kitu siyo serious kabisa kwa sasa
 
Inakera sana sana kufake status yake mpaka maana inapotea.

Ngoja niwape kisa kimoja:

Kuna mkaka mmoja(sasa hivi ameoa) alimsumbua sana mdada mmoja ambaye wote walikuwa wanaishi jirani huko Magomeni, ilifika mahali dada alichukua uamuzi wa kuvaa pete ya uchumba na kumueleza kwamba ana mchumba,ilifika mahali kaka wa watu alikata tamaa na alichukua uamuzi wa kuhama Magomeni na kuhamia Tegeta, bahati nzuri huyo kaka alikuwa na kazi nzuri tu kipindi hicho.

Siku moja katika pita pita yake mitaani maeneo ya Lufungira alishtuliwa na mdada mwingine ambaye naye alikuwa jirani maeneo ya Magomeni, alimwuliza mbona haonekani mitaa ya magomeni? na akamuongezea kwamba kuna mdada (yule aliyemsumbua) anamtafuta kweli na hakupata bahati ya kumpata yeye(huyo kaka). Alichomjibu, "mwambie nimeshaoa!".

Ilipita kama wiki tatu hivi, yule dada kumbe aliambiwa na watu kwamba anafanya kazi kampuni fulani (ofisi kapuni) kutokana juhudi zake za kumtafuta huyo kaka, bahati nzuri mdada alimpata na waliongea mengi, katika maongezi yao huyo dada alimwuliza kwanini alihama pale,alichomjibu, "Kuna mmoja aliniudhi sana,akajitambulisha kwamba ni mchumba wa mtu kwangu!"

Dada aliomba msamaha kwa kile kitendo cha kufake kwamba ni mchumba wa mtu, na alimpa sababu kwamba alifanya vile ili kumfanya huyo asiendelee kumfuata, kumbe alimsoma mwanzo mpaka mwisho na alijua kwamba hana boyfriend. Huyo kaka alikuwa na nia ya kumuoa huyo dada kabisaaa!!

Lkn hakumuoa huyo dada alisema hajui kama huyo dada alisema ukweli au la, maana hakumfuatilia tena.

Nimegundua kufake kwa pete kunafukuza wanaume wa ukweli!
 
ni kweli kabisa,mwanaume atakayefuta japo anaona umevaa hiyo pete si mtu mzuri na wala si muoaji.
anyway,sielewi kwanini mtu ujipe status usiyo nayo.
 
ni kweli kabisa,mwanaume atakayefuta japo anaona umevaa hiyo pete si mtu mzuri na wala si muoaji.
anyway,sielewi kwanini mtu ujipe status usiyo nayo.

Kwani hii biashara ikiachwa kutakuwa na madhara?
 
Inawezekana maana yake imeanza kupotea lakini bado ina umuhimu wake, kwa wanao heshimu ni alama ya upendo mkuu na kwa wasio heshimu atleast wanajua kwamba wanaiba vya watu so wanakua waangalifu
Unamaanisha mwizi ni nani? Anayevaa ring, au ni third party?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…