Pete za ndoa na mahusiano ya nje ya ndoa

Kajuni

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Posts
483
Reaction score
186
Mimi ninaamini kwamba lengo la pete za ndoa ni kuonyesha kwamba huyu mtu (Mwanamke au Mwanaume) ameoa ama ameolewa. Kinacho nishangaza na nimeshuudia hawa jamaa wenye pete wana mahusiano nje ya ndoa na mkononi ana pete kubwaaaaaaaa sasa je wahusika wanapokuwa wana anza haya mahusiano uzi tupa kando then wakifanikiwa wanazivaa? Je dada zetu na kaka zetu wana watamani watu walio ndani ya ndoa? au ni fashion? who is to blame?
 
Cha ajabu hapo nini sasa? Kwani wewe unapopanda daladala wakati umeona imejaaa! Huwa akili na macho unaviweka kando? This is bcoz common sense is not always common to all

Makubwa haya........nimekupata Trustme!!! hapo ulipo umevaa pete ya ndoa nini?
 
Kusema kweli Kajuni siku hizi si wanaume si wanawake,watu wanatoka nje ya ndoa kwa kwenda mbele,na katika kufanya uzanga huu walio wengi hawajali whether you are married or not,wanachojali ni nini wanapata katika mahusiano iwe raha ya mwili,pesa,kupandishwa cheo,kufaulu mtihani,kupewa tenda........sababu ni nyingi tu,ndo mana mkifumaniana badala ya kukimbilia talaka ni bora mkae chini mkiwa wawili muongee candidly si ajabu mkagundua kwa nini mwenzio ana stray.
 
Nilimsikia mmoja anasema wenye pete/Ndoa ndio wazuri kishenzi kufanya nao uzinzi.

Kama ni mwanaume hatokuwa msumbufu kumfuatilia na kumdhibiti sana mrembo, maana ana kwake!

Kama ni mwanamke basi atatekeleza kila unalomwomba au kumfanyia, maana anahofia akikataa unaweza kumsemelea na kumvurugia!... ha ha haaa!

Sifahamu ukweli wa hayo!
 
Umenena kweli mkuu! nafikiri hoja zako zina mashiko sana...i think we need research on this area.
 
shida ni kwamba pete za ndoa zinavaliwa hata wa wale wasio na ndoa na hivyo ni ngumu sana kujua kenge ni yupi na mambo ni yupi.

vie vile, wanaume wenye pete za ndoa wanapenda kuranda mitaani kwa vimwana, kisa, eti vimwana wakishaowaona wana pete za ndoa watajua jamaa wameshawahiwa na hivyo hawatawasumbua, sio simu wala sms za kuwakera wake zao!

Ila kwa watu wenye heshima zo, kuvaa pete za ndoa ni respect ya hali ya juu, wakware wanapita mbali, wanajua it is already occupied!
 
Cha ajabu hapo nini sasa? Kwani wewe unapopanda daladala wakati umeona imejaaa! Huwa akili na macho unaviweka kando? This is bcoz common sense is not always common to all

Mbona una hasira namna hiyo? Kama kitu kimekugusa tumia lugha nzuri ya kufikisha ujumbe sio unakuwa mkali kama nini mkubwa
 
Hili swali limenigusa sana huwa naangalia watu na kuwashangaa sana unakuta mtu na mpete wake huyoo G/H tena bila hata soni machoni mwake.

Mara nyingi mie husema kama mtu hujakuwa tayari kuoa na usioe. Yaanini kujipa tabu na kuumiza mwenzi wako
 
Na wakikutana na pete za ndoa wote mkononi watu hudhani wameoana kumbe wote wezi mweeeee
 
Hili swali limenigusa sana huwa naangalia watu na kuwashangaa sana unakuta mtu na mpete wake huyoo G/H tena bila hata soni machoni mwake.

Mara nyingi mie husema kama mtu hujakuwa tayari kuoa na usioe. Yaanini kujipa tabu na kuumiza mwenzi wako
Wewe humo G/H unafata nini na wakati hujaoa na una kwako? kwa nini usianze kuwa mwaminifu kipindi hiki ili ukiingia ndoani inabaki kutekeleza tu?
 
wala hujakosea ndivyo wanavyosema siku hizi....

mi nakumbia zamani ukiona mtu anapete unamuogapa kabisa na yeye kama ilikuwa
anataka kufanya uchafu pete kama inamsuta hiv.

siku hizi pete ni fashion...... ndoa si pete jamani
.
 
Wala haihuu!!!! Mbona mtu anajua kabisa fulani ni mume wa fulani, dada/rafiki yake lakini bado anakuwa na mahusiano naye. Kuna watu huwa wanatembea mpaka hata na baba zao, kaka zao hapo hata pete haihusiani, kama mtu ameamua kutembea na mtua anatembea tu awe na pete au hata hasipokuwa na pete, maana sio hata kupendana tena, bali ni kutembea.
 
tena wana ka-msemo kao ka methali.......''mwenda tezi na omo hurejea ngamani''.
 
Wewe humo G/H unafata nini na wakati hujaoa na una kwako? kwa nini usianze kuwa mwaminifu kipindi hiki ili ukiingia ndoani inabaki kutekeleza tu?

Mkubwa mie nimeoa nina miaka mitano ya ndoa. G/H nawaona na si mimi naingia huko namheshimu sana mke wangu siwezi kumwendea kichwa
 
Wewe humo G/H unafata nini na wakati hujaoa na una kwako? kwa nini usianze kuwa mwaminifu kipindi hiki ili ukiingia ndoani inabaki kutekeleza tu?

hapo umenena Gaga
 
pete halis ya ndoa huwa iko moyoni mwa mtu na si kidoleni.........
Leading post kwenye hii thread, kwa kweli kama hujaivaa moyoni hata kidoleni ni kama gamba tu
 
wala hujakosea ndivyo wanavyosema siku hizi....

mi nakumbia zamani ukiona mtu anapete unamuogapa kabisa na yeye kama ilikuwa
anataka kufanya uchafu pete kama inamsuta hiv.

siku hizi pete ni fashion...... ndoa si pete jamani
.

za masiku?:focus:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…