Peter Drury: Mtangazaji nguli wa soka

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
PETER DRURY NA KINYWA KILICHOTAKASA BURUDANI YA SOKA


Utamu wa Drury chumbani kwa David Cameroon.

Ukifika viunga vya St John's School katika utawala wa mama mpendwa Malikia wetu Elizabeth ndani ya Ufalme wenye jina kubwa ulimwenguni, wenye itikadi kali na ngumu; nazungumzia kule alikotengwa yule mjukuu pendwa wa mfalme.

Yes, katika kizazi cha karne ya 21 unakutana na vipaji vingi vinavyofurahisha mioyo ya mashabiki ulimwenguni, achilia mbali aina ya soka lenyewe linalopigwa katika nyasi tukufu za Mama Kipenzi cha Waingereza.

Hapa leo tutazungumzia huduma nyingine bora inayotolewa viunga hivyo na sauti yenye kubembeleza na kufurahisha mioyo za mashabiki wapenda soka na burudani. Hapa namzungumzia commentator (mshereheshaji), si mwingine ni PETER DRURY.

Akianza safari yake katika sebule iliyopambwa kwa maua mazuri na mapambaji akiwa mama yake Drury.

Siku moja mama yake mzazi alichukuwa pasi yake na kuanza kunyoosha nguo, na ndipo kiligundulika kipaji cha Drury.

Ushawahi fahamu jamaa ana taaluma ya Uhasibu? Nani aliemgeuza mawazo Drury mpaka kuwa mshereheshaji, si mwingine bali ni role model wake wajina mwenzie PETER JOHN enzi hizo John Akiwa BBC Radio na Drury akikomaa na uhasibu.

Vipi kuhusiana na safari yake kwa boss mmoja kutoka kule West London Ilivyobariki maisha yake?

Unakumbuka maneno yake usiku ule wa 13 June 2014 viunga vya Maracana? Vipi kuhusu usiku ule wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Roma na Barcelona, ntakupa maneno ya nusu finali hiyo.

Wakati Manolas anapiga msumari wa moto kwa Barca na haya yalikua maneno yake:

"Roma have risen from their ruins Manolas the Greek God in Rome, the unthinkable unfolds before our eyes, this was not meant to happen, this could not happen, this is happening, Barcelona extraordinarily eight minutes from elimination, Di Francesco does not know where to go, Iniesta does not know where to look, It is a Greek from Mount Olympus, who come to the seven hills of Rome and pulled off a miracle.

Licha ya uwepo wa washereheshaji wengi waliopita na waliopo kama Jim Beglin, lakini bado Peter Drury ni sukari isiochosha kutumia kwa kila mpenda soka na burudani.

Ichukie ikuburudishe, ukichoka inabembeleza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…