Leo nikiwa napitia chapisho lisemalo "the last days of JMKariuki" nimekutana na jina la Peter Kinyanjui alias Mark Twist. Kwa wale vijana wa zamani watakumbuka jinsi huyu Mark Twist alivyokuwa mashuhuri kwa namna fulani katika mitaa ya DSM miaka ya 80 na kuendelea. Kilichonifanya nimlete hapa jamvini ni jinsi Mark Twist alivyohusishwa na kifo cha JM Kariuki aliyekuwa mtu mashuhuri sana Kenya wakati huo. Huyu jamaa alipotelea wapi au kesha tangulia mbele ya haki?