Peter Kupaza, Mtanzania aliemuua dada yake nchini Marekani

Nataka kuamini hili ila je damu iliyokutwa chooni? Na kwanini jamaa adanganye kuhusu dada kurudi nyumbani? Hapa tuseme ishu ni visa.

Kwanini alimdanganya mwanamke mwingine?



Kuna maswali mengi yanayokosa majibu.
 
Dada kapotea miezi kadhaa haujafanya jitihada zozote za kumtafuta.

Peter amehusika kwenye hili.
 
Kwenye hii case mhusika ni huyo mtalaka wa kizungu...ila Kupaza kajichanganya katika kutoa taarifa za uongo
 
Shida jamaa hakuwa "MKWELI"
kupaza alidanganya,.
Hyo ilishamfunga mapema
 
Shida jamaa hakuwa "MKWELI"
kupaza alidanganya,.
Hyo ilishamfunga mapema

Ila kiukweli kabisa wabongo wengi wanaoishi mtoni ni waongo waongo balaa..! Nadhani ni kwavile wengi wanaishi kule kimagumashi kwahiyo mda wote hua wanakua na wenge na wanadhani kila kitu unaweza kutumia saundi za kiswahiliswahili ukachomoka.

Huyu jamaa inawezekana wala hakuua, kilichomfunga ni uswahiliswahili mwingi, uongo uongo na saundi mingi alidhani yupo kwao Tanga.
 
Ushahidi pekee ambao uko solid ni wa Peter kutoa taarifa za uongo zinazoonyesha kwamba ndg yake amesharudi TZ na kuthibitisha kwamba ameongea na hata wazazi wake! Otherwise ushahidi mwingine hasa ule unaotolewa na Mtalaka mwenzake unaonekana ni wa kulipa kisasi zaidi kutokana na mahusiano yasiyo na Afya kati ya Peter na binamu yake na kupelekea ndoa yao kuvunjika so, ukiisoma kwa makini kesi hii Kuna uwezekano pia ikawa plot ya revenge kutoka kwa Mtalaka mwenzake
 
Ebu tuangalie kwa jicho lingine.
Ukute kweli kwamba ilikuwa ni kisasi cha mtalaka wake.
Huyo mzungu aliekuwa aki randaranda... wakili alie mwakilisha jamaa wote walipangwa.

Ukizingatia kwamba bint alieuwawa alishafikiri kurudi TZ, haishindikani kwamba mtaliki wa kaka yake(huyo mzungu ) alitumia shida yake hiyo kumvuta karibu na kutekeleza hayo mauaji.

Wakati mwingine elimu duni na ulimbukeni ndio uliopelekea hata jamaa kutoa maelezo yasiyo sahihi.

Kwa ujumla wote hatujui, ukweli umebaki kati ya Peter, mtaliki wake na marehemu .

RIP binamu yake Peter!
 
Wakati huo jamiiforums ilikuwa inaitwa jamboforums, hii kitu kweli ya zamani
 
Acha hizo wewe, huko bongo watu ndio waongo waongo hadi ma vyeti feki ya kumwaga. Nafikiri bongo inaongoza afrika mashariki kwa waongo na wapumbavu wengi.
 
Hata kwa nilivosoma hapo, mbona sababu ya jamaa kufanya hivyo haijaanishwa!!

Na hapo mwisho ni jopo limekaa likhalalisha kua mwamba ndo ana hatia(ushahidi wa kimazingira) ila ni kama bado una mashaka ndani yake, sio wa moja kwa moja.

Mtalaka wa jamaa atakua na mkono katika hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…