Pre GE2025 Peter Madeleka: Mbowe amefika mwisho, hana jipya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakili wa Kujitegemea nchii, Peter Madeleka, amesema Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefikia mwisho wa mchango wake katika siasa za mageuzi na hana jipya la kutoa katika mazingira ya sasa ya kisiasa nchini.

Akizungumza na Jambo TV, Madeleka amesema kwamba siasa za mageuzi nchini zimebadilika kwa kiasi kikubwa, huku changamoto zikihitaji viongozi wenye uwezo wa kupambana na hali ngumu kwa mtindo wa "ulalo ulalo."

“Tunahitaji kiongozi ambaye anaweza kwenda na CCM kwa mtindo wa ulalo ulalo. Kwa haiba na historia ya Mbowe, si mtu wa aina hiyo. Mbowe ni kiongozi wa siasa za kistaarabu na maridhiano, lakini siasa za leo zinahitaji mtu asiye na cha kupoteza, mtu anayeweza kupambana kwa hali yoyote,” alisema Madeleka.

Akizungumzia historia ya mageuzi nchini, Madeleka alibainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, hali ya kisiasa imezidi kuwa ngumu, huku ukiukwaji wa Katiba na sheria ukishamiri. Alisema kuwa mazingira ya sasa yanahitaji kiongozi ambaye anaweza kuhakikisha haki za kikatiba zinalindwa kwa vitendo, si kwa maneno pekee.

“Tundu Lissu ni mfano wa kiongozi aliyelipa gharama kubwa kwa ajili ya siasa za mageuzi. Amepigwa risasi na bado anaendelea kupigania haki. Tunahitaji watu wa aina hiyo ambao wako tayari kupoteza kila kitu, hata maisha yao, kwa ajili ya kuimarisha demokrasia,” aliongeza.

Madeleka pia alikosoa hatua ya Mbowe kukubali katazo la kufanya siasa wakati wa utawala wa awamu ya tano, akisema kuwa kama kiongozi wa chama chenye malengo ya kushika dola, hakuwa na budi kupinga waziwazi hatua hiyo kwa mujibu wa Katiba.

Hata hivyo, alisifu mchango wa Mbowe katika siasa za mageuzi, akisema kuwa ameweka msingi mkubwa ambao umekiimarisha CHADEMA na kuvutia wafuasi wengi kutoka makundi mbalimbali ya kijamii.

“Namshukuru Mbowe kwa mchango wake mkubwa, lakini sasa amefika mwisho. Kama ilivyo kwa kocha wa mpira anayewajibika pale timu inaposhindwa, ndivyo ilivyo kwa Mbowe. Hii haimaanishi kuwa si kiongozi mzuri, bali ametimiza wajibu wake, na tunahitaji kiongozi mpya mwenye mtazamo tofauti kwa mazingira ya sasa,” alisema Madeleka.

Madeleka alihitimisha kwa kusema kuwa mabadiliko ya uongozi ndani ya CHADEMA ni muhimu ili kukabiliana na changamoto za kisiasa na kuhakikisha kuwa chama kinaendelea kuwa chombo madhubuti cha kuleta mageuzi nchini.Madeleka alikosoa hatua ya Mbowe kukubali katazo la siasa wakati wa awamu ya tano, akidai ilikiuka Katiba.

Hata hivyo, alisifu mchango wa Mbowe katika kuimarisha CHADEMA lakini alisema muda umefika wa kumpisha kiongozi mpya mwenye mtazamo unaoendana na changamoto za sasa. Alisisitiza kuwa mabadiliko ya uongozi ni muhimu kwa mustakabali wa chama na mageuzi ya kisiasa nchini.
Your browser is not able to display this video.


Pia, Soma:

Peter Madeleka: Wanasema ukitaka kugombana na Mbowe, gombea Uenyekiti wa CHADEMA

Mbowe arudisha fomu ya kugombea Uenyekiti CHADEMA
 
Tatizo mbowe ana mkataba na ccm ni ngumu kusikia
 
Si wapige kura mbona wanachambana tena. Waamue kupitia masanduku.
 
WACHA WARARUANE TU SI NDIYO ANAWATETEAGA?
 
hata kipindi cha dr slaa, mbowe alikuwa ananga'ng'ania hivihivi kugombea, hadi kelele zilivyozidi ndio akampa kugombea dr slaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…