Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Habari zenu wanabodi,
Kwenye mahojiano na Chief Odembo kwenye kipindi cha Medani Za Siasa, Mch. Peter Msigwa amezidi kutupia mawe Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Msigwa kwenye mahojiano hayo alifananisha CHADEMA na SACCOS kutokana na namna ambavyo chama hicho kinaongozwa kama biashara,
Kuhusu Mbowe, Peter Msigwa alisema:
Soma pia:
- Kuelekea 2025 - Yaliyojiri kwenye mahojiano kati ya Chief Odemba na Peter Msigwa kwenye kipindi cha Medani za Siasa
Mchungaji Msigwa: Mbowe Mwenyekiti uliyekaa sana Madarakani tukutane Mahakamani

"Nimeshazungumza sana hata kwenye vikao vyangu kwamba CHADEMA imekuwa kama SACCOS, imekuwa ni mali ya mtu. Nilishawauliza sana kwenye chama kwamba CHADEMA digital ni mali ya nani. ? Hela za CHADEMA digital zinaenda kwa nani, ni mali ya nani ?
Join the chain. Wakati huu ukiangalia tunakusanya hela za join the chain, kuna namba nyingine ya mtu binafsi iliwekwa. Hela badala ya kuingia kwenye chama zikawa zinaingia kwa mtu binafsi
Kuhusu Mbowe, Peter Msigwa alisema:
Mbowe anakimbiwa na kila mtu, watu wote wenye akili wanamkimbia Mbowe. Anabaki na watu chawa. Wameondoka wakina Zitto, wameondoka wakina Kitila, wameondoka wakina Safari , wakina Marcos, wakina Kitila sasa hivi tumeondoka. Wakina Cecil Mwambe wameondoka. Wakina Silinde wameondoka, wakina Jualikali wameondoka.