Pre GE2025 Peter Msigwa na Upendo Peneza wajifunze kutoka kwa Hayati Edward Lowassa

Pre GE2025 Peter Msigwa na Upendo Peneza wajifunze kutoka kwa Hayati Edward Lowassa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262


Wanasiasa Peter Msigwa na Upendo Peneza wamehamia CCM hivi karibuni kutoka CHADEMA chama kulichowalea na kuwakuza hadi kufikia ngazi ya ubunge na kuwa miongoni mwa wanasiasa maarufu hapa nchini kutokana na michango yao bungeni.

Pia soma: CCM kuubeba msiba wa Lowassa bila kumuomba kwanza msamaha kwa mliyomtendea ni aibu

Baada ya kuhamia CCM wapewa tenda ya kuwakashifu viongozi wa juu wa CHADEMA hasa mwenyekiti wake Freeman Mbowe na CHADEMA kwa ujumla. Kwa kifupi wanasiasa hawa wameamua kuukata mkono uliowalisha na kuwakuza hadi kufikia hapo walipo.

Pia soma:

~ Upendo Peneza ahamia CCM, awananga CHADEMA
~ Upendo Peneza: Wakati naingia CHADEMA haikuwa kubwa kiasi hicho

Ushauri wangu kwao ni kuwa hebu wajifunze siasa za kistaarabu alizozionesha Marehemu Edward Lowassa. Lowassa baada ya kuhama CCM na kuhamia CHADEMA hakuwahi kwatukana wala kuwakashifu viongozi wa CCM akiwemo mwenyekiti wake na CCM kwa ujumla ingawa wao wakiongozwa na Nape walimchafua sana lakini yeye hakuwahi kujibizana nao. Yeye alishughulika na CHADEMA.

Pia soma:

~ Kuelekea 2025 - Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM
~ Zembwela: Mchungaji Msigwa leo ndio anaiona Chadema ni Saccos ya mtu mmoja baada ya kushindwa kutetea cheo chake Kanda ya Nyasa

Baadaye alihama CHADEMA na kurudi CCM. Vivyo hivyo hakuwahi hata siku moja kufungua mdomo kumkashifu mwenyekiti wa CHADEMA wala CHADEMA yenyewe mpaka alipofariki. Kama wanasiasa hawa wanaakili zao na si za kushikiwa wanapaswa kujifunza na kumwiga Lowassa. Kuhama chama ni haki yao kikatiba hivyo hakuna haja ya kuuvunja vunja mwamvuli uliokusitiri wakati wa mvua. Siasa ni maisha hamjui jesho mtakuwa wapi.

Hao CCM mnaojiona mmefika ni viongozi tu ndio wanaowatumia kama kondom kazi ikiisha mtapotea kabisa katika ulimwengu wa siasa na msifikiri wanachama wa CCM wanawapenda sana kwasababu wakati wao wakipambania chama chao ninyi mlikuwa mnawatukana kuwa ni akili ndogo lakini leo mmeungana nao kwa tamaa ya vyeo sasa msidhani wanafurahia ujio wenu kuja kuchukua vyeo ambavyo nao wanavitaka.

Na kosa wanalolifanya CCM ni kuwapa majukwaa na nafasi kubwa wakimbizi kutoka CHADEMA huku wakiwaweka nyuma wanaccm waaminifu waliokipigania chama chao lakini wanaona wageni wanakuja na kupewa nafasi zao. Machozi yao yatakuwa laana kwao. Time'll tell
 
Back
Top Bottom