Peter Msigwa ni sawa kuhama chama lakini haikupaswa kufanya hivyo

Peter Msigwa ni sawa kuhama chama lakini haikupaswa kufanya hivyo

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Unapokisema vibaya CHADEMA huwakomoi akina Mbowe na Mnyika TU bali unaudhi wafuasi wengi sana wanaokiamini CHADEMA na wanaoamini siasa za vyama vingi. Wapo watanzania wengi tunaoamini vyama vingi vyenye nguvu vinavyoshimdana kwa hoja na sera nzuri za kuwatumikia wananchi ni faida kwa nchi na wananchi wakiwemo hata wafuasi wa CCM wenyewe.

Msigwa anajua kuwa CHADEMA inao wafuasi wengi sana wanao kiamini CHADEMA ambao wamemfikisha hata yeye pale alipo. Hata magauni ya mke wake bila shaka Yana uhusiano na chadema kwa namna yalivyopatikana.

Unaweza kuhama chama bila kuhatarisha uhai wa chama, viongozi na wanachama wa chama ulichokihama, unless ulikuwa pandikizi kwenye chama hicho.

Unataka kusema kuwa wewe unaamini kwenye fikiria za chama kimoja? Ni nchi gani yenye chama kimoja inayokuvutia sana wewe kwenda kuishi huko?

Vitendo na maneno baada ya kuhama chama yanahatarisha maisha ya chama, viongozi na wafuasi wa CHADEMA, unakubaliana na hilo?

Umeingia kwenye orodha ndefu sana ya watanzania ambao walipinga na kudhoofisha demokrasia nchini kabla na baada ya uhuru. Wajukuu na vilembwe vitakuja kukusoma kama mchungaji msaliti na mpenda madaraka uliyekubali kuwasaliti wanachadema wooooote nchini kwaajili ya kunyimwa uenyekiti wa Kanda ya nyanda za juu kusini.
 
Anashangaza,like amechanganyikiwa.

Yeye akijenge zaidi chama chake kipya kwa kuyaeneza mazuri yake.
Nani aliyemwambia kutukana,na kuponda CHADEMA ndo credit kwake. Zaidi ya kujidhalili na kupata aibu kwa watanzania wanaojielewa.

Mchungaji wa hovyo hah
 
CCM wanamfanya kikaragosi. Ubunge kwa miaka kumi kupitia wafuasi wa CHADEMA. Wewe huogopi kuwasaliti? Kuwasaliti Watu waliokupigia na kulinda kura zako kwa hatari na mateso wewe huogopi?
Anashangaza,like amechanganyikiwa.

Yeye akijenge zaidi chama chake kipya kwa kuyaeneza mazuri yake.
Nani aliyemwambia kutukana,na kuponda CHADEMA ndo credit kwake. Zaidi ya kujidhalili na kupata aibu kwa watanzania wanaojielewa.

Mchungaji wa hovyo hah
 
Hajahama Kwa hiyari, ni mpango mkakati wa kuidhoofisha CHADEMA. Unajua kitendo Cha wakina Nasari, lijualipole, Msigwa na wengineo kuhama Kuna wanachama wengi sana wa Chadema wamekatishwa tamaa coz mtu anajiuliza juzijuzi tu tunampigania mtu Fulani then Leo kahamia ccm inamaana wapinzani hawana msimamo. Hiyo ni technique ya kuwavunja moyo wafuasi wao na hapo ndio chama tawala kinaendelea kuishika dola. Amini ukisikia mtu yoyote anakwambia hatopiga kura Kwa sababu mbalimbali zikiwepo sijui wizi wa kura, hakuna tume huru ujue huyo asilimia tisini yupo upinzanzi.
 
Demokrasia duniani haikujengwa kwa kutumia dialogue (majadiliano). Ili jogoo apate nafasi ya kumpanda mtetea katikati ya majogoo wengine Kuna kubwa ameifanya, la sivyo hagusi mtetea hata mmoja.
 
Madhara ya msigwa kunywa ulanzi utotoni ndo yanaonekana sasa
 
Back
Top Bottom