The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mchungaji Peter Msigwa amesema alishiriki wazi kumpinga Freeman Mbowe wakati akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, akisisitiza kuwa hakufaa kuendelea kuongoza chama hicho.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio cha Ebony FM leo, Msigwa amesema kuwa aliona mapema kuwa Mbowe alikuwa akikipeleka CHADEMA shimoni na aliamini kwa asilimia 100 kuwa angepoteza nafasi yake ya uongozi.
"Kumfanya Mbowe kuendelea kuongoza chama kile ilikuwa ni kukipeleka shimoni, hafai na tunapaswa kuwa na demokrasia," alisema Msigwa.
Ameongeza kuwa, msimamo wake dhidi ya Mbowe hauimaanishi kuwa waliokuwa madarakani hawawezi kuwa na makosa au kwamba hawezi kuwapa changamoto.
"Nitawawapa changamoto," alisisitiza Msigwa huku akieleza kuwa wengi hawakuamini mwanzo lakini baadaye walikuja kukubaliana naye kuwa Mbowe hakuwa na nafasi ya kushinda.