Katika Uchunguzi wangu wa Kina, nimegundua kuwa Tatizo sio Vodacom Hapa, Tatizo ni UKABILA NA UKANDA ndio unatusumbua kwa sasa.
Wachaga walikuwa very influencial katika siasa za Tanzania, but they lost that status as the time was passing on. Ukiangalia utawala wa Mkapa uliwanufaisha sana wachaga, which has lost in Kikwete leadership. On other hand kwa Kuangalia political Map Rostam Aziz ni influential kwasababu alikuwa na good ties with the lake zone which politically always is a very big decider of Tanzania politics.
naogopa kabisa kufikiria hoja ya kikabila.. kwa sababu in that case watu wa magharibi watashinda hands down! Hapana.. hii ni kati ya watu wanaoamini kuwa utajiri wa nchi ni wa kwao peke yao na wale ambao wanataka tugawane utajiri huo.
Hivyo Vodacom naamini ni mahali kama pa recruitment.. haiwezekani:
Dr. Idris
Ngeleja
Noni
Rostam
n.k something is very wrong.. kama RA ameweza kukuamini kwenye Vodacom.. you have passed the test
Hayo mambo ya ukabila power etal.. ni spin, tena msitake kutuvuruga na kutupandikiza fitina ili tuache kushikama kuyaangusha mafisadi!
Hapo swala ni wezi wachache kuiba hela zetu na kutumia hizo pesa kuiweka serikali madarakni,na kibaya zaidi kuipangia uongozi hivyo kuifanya serikali nzima vibaraka wao kwani hawawezi kuwagusa kwa vile ndo wali waweka!
Hizo propaganda zenu ni za kubuni kuhisi na your wishful thinking!
turudi vitani wakuu, hakuna cha kabila la kijani wala blue, hapa ni mafisadi wote kurudisha kilicho chetu period!
Rwabugiri, si kwamba vita vya ufisadi havina maana. nalo ni jambo ambalo ukiluckulia peke yake lina maana kubwa ikiwezekana hata zaidi ya hiyo vita ya ukabila ambayo imetupeleka kwenye vita vya ufisadi. wasicghofahamu watu wengi ni hiyo connection ya vita vya ufisadi na kugombea power.
Hivyo, ni vma vita vya ufisadi viendelee kupiganwa lakini kuwa makini vinapiganwa kwa malengo gani kwa sababu si kila anayepambana na ufisadi anapambana kwa lengo ya kuuondoa ufisadi pekee
LeoKweli na Limbani msitupotoshe!
Hapa tunazungumzia vita dhidi ya ufisadi. It is a war between PATRIOTIC TANZANIANS against BOISTEROUS CORRUPT PEOPLE.
Hata humu jamvini ukifuatilia utaona kabisa kuna pande mbili. Wapo watetezi wa mafisadi ambao wanatoa hoja za kuharibu michomo dhidi ya mafisadi. Na wapo ambao wanajadili ufisadi kwa uchungu mkubwa wakinuia kuuondoa kabisa ili kuinusuru nchi na watu wake.
Hapa jamvini tuwatendee haki watanzania kwa kujadili kile ambacho kitaokoa uhai wa watanzania, kuyaboresha maisha yao na kuondoa umasikini unaowakabili.
Nchi hii ni tajiri sana. Lakini kutokana na tamaa ya baadhi ya watu ambao wana nafasi kubwa serikalini, wameamua kuuweka mfumo in such a way that watakula wao na marafiki zao na kuwaacha watanzania hoi kwa dhiki.
Huu ni unyama, upumbavu, uroho na ushetani ambao lazima tujenge utamaduni wa kuukemea bila soni hata moja usoni. Wanaotaka kuungana nami katika hili wajitokeze bila hofu.
Naipenda Tanzania
Nawapenda watanzania
Sijasema ukabila ni tatizo but what I was insisting is that Regional Politics is playing a very big role in this war against Ufisadi.
Hii ishu ya Mengi na RA is a mixed bag. We need to separate uchafu uliomo ili tuweze kufanya purification.
Tatizo,
Regional Politics
Business Intrest
Ufisadi UMEGAWANYIKA sehemu mbili, Personal na Wa CCM Hivyo tunatikiwa tuwe analytical ili tuweze kuutenganisha.
Therefore Huwezi ukaacha kuuongelea huo Ukweli.
utawala wa mkapa uliwanufaisha watu walio karibu na mkapa ie mramba, yona,mgonja, RA, manji na sio wachaga kama unavyosema wewe.
Mtu kama mengi unaemuongelea alitajirika sana kipindi cha mwinyi na wafanya biashara wengi wa kichaga walitajirika kipindi cha mwinyi kwa ajili ulikuwa ni uhuru kwa kila mtu
Lakini wakati wa mkapa mpaka umuone yeye na hao wakina mengi wote unaowaongelea wewe wamenyanyaswa sana na mkapa
hata kuna jamaa mmoja wa arusha (anaitwa Mrema) alitaka kununua 77 hotel na jamaa record yake katika biashara za hoteli ni nzuri, alilipa deposit na kila kitu mkapa akampa swahiba wa manji jamaa wa kempiski
kama angekuwa amewapendelea wachaga si Mrema angepata hiyo hoteli kihalali matokeo yake sasa hivi serikali inamplifa fidia ya hoteli nyingine.
wachaga wanapata hela sio kwa ajili ya ubaguzi bali ni washindani na mfano nenda moshi uwezi kukuta waindi wanafanya biashara kama mikoa mingine kwa ajili wao wachaga wameamka, hata ukienda arusha utakutana na wafanya biashara wengi wa kichaga
rostam sio kama ameiweka mfukoni kanda ya ziwa bali amewaweka mfukoni viongozi wachache muhimu, na huu sio ukabila
na lazima uwelewe kama mkwere ajasema wakina mramba watolewe kafara basi hosea hawezi kuanzisha, wala dpp pia hawezi. Ni mkwere ndio anachagua nani wa kumtoa kafara ili kupata public support lakini siona hata mmoja wao kama atafungwa. Mramba anajua madhambi ya watu wengi sana kutokana position yake aliyokuwa nayo kwa hiyo kumfunga ni sawa sawa nakuvujisha siri nyingi
Hivi umetumwa?
Kwa taarifa yako kawambie hao walo kutuma kwamba ueneze na kupandikiza hisia za ukabila, ili watu tuache kumuunga mkono Mzalendo Mengi katika vita ya kulikomboa taifa letu mikononi mwa mafisadi, kwamba 'tumekustukia'
Hapa ni kuwakaba mafisadi papa wote wakiongozwa na Fisadi papa Rostamu Azizi hadi warudishe nchi yetu na kila kilicho chetu period!.
I dont question how hard work is wachaga, I will be stupid to do that, because ukweli uko wazi this people are hard worker and market oriented.
Ninachojaribu kukufungua macho ni kwamba, Regional Politics zina play a big role katika hili swala, na ninajua una dispute but huu ndio Ukweli.
Ukiangalia kwa makini sana, Kuna watu wengi wenye pesa sana Kule maeneo ya Kanda ya ziwa But they never in politics and spotlight but in the past 5 years wameanza kuingia kwenye siasa.
Kuingia kwao kwenye siasa kumewafanya more powerfull based on their strategic location.
kilicho wapeleka huko walijua fika ccm ni kichaka cha majambazi. so ukiingia humo utafanya uchafu wote wa kuendeleza biashara zako bila kuguswa! hasa ukisha wachangia/wakatia kitu kidogo.
hebu niambie kama kweli waliingia politics ku gain power nani aliingia opposition kama siyo wote kuji sondeka kwenye kichaka cha ujambazi?
Narudia wito wangu, usitutoe kwenye mada, hakuna ukanda wala ukabila hapa, hii ni vita kati ya wakwapuaji mali na raslimali za taifa letu, dhidi ya wanyonge/wenye mali tulio ibiwa period!
Hiyo sumu yako ya ukanda na ukabila bahati yako mbaya imekutana na 'ant venom' sorry it will not work.
Usiseme nimetumwa , this is a free forums and people have rights to disagree I am not here just to take postion mimi ni more pragmatic than you think.
You see kumbe wewe Uko upande wa Mengi, Mimi Niko neutral I am trying to analyse the truth and you have an option to agree or disagree with me.
Kama mengi Yuko serious na Vita ya Ufisadi kwanini asiseme CCM ni mafisadi. He has his own intrest that why he is talking about Ufisadi.
Kumbuka ITV imeisadia sana CCM, and the main benefiery of Pesa za Uchaguzi is mengi as well through ITV Unatufanya hatujui hilo.Radio One ETC
What kind of neutral? unless sielewi maana ya kuwa neutral, utakuwaje neutral wakati uko upande wa kuspin kwamba Mengi anatumia vita ya ufisadi kurudisha power ya wachaga iliyo potea?
Come on man, msitake kututoa kwenye kiini, hakuna ukabila hapa wala ukanda, ni vita kati ya wezi (fisadi) na tulioibiwa watanzania wazalendo period!
Kama vyombo vyake viliisaidia CCM huko nyuma, yes, lakini nani alijua huko nyuma kwamba CCM imetekwa na mafisadi? I guess Mengi is not an angel kwamba alijua hilo
Lakini baada ya kujua kapiga about turn is that a sin? Ndiyo maana nampongeza na kumuunga mkono.
Tangiapo, yeye ni tajiri sana, hela aliyo nayo inamtosha kula kwa raha zake maisha yake yote atakayo jaliwa na Maulana, Ni uzalendo tu ndio unamsukuma kufanya hivo, na siyo hizo spin mnazo taka eneza kwamba ni ukabila mara ukanda nooooo.
Pili utakuwa hutaki kutambua ukweli kama unakataa kwa makusudi kuwa regional politics hazina tija. Nenda NEC CCM ukawaulize? watakueleza vizuri , Kamwulize Sumaye ? Kula za Kanda ya ziwa zilivyomkosesha Uraisi
therefore huo ndio ukweli
wacha uwongo hamna cha regional politics, sumaye watu wote walikuwa wamemchoka na ndio sababu ya kushindwa hata watu wa North hawakumpa kura sumaye.
sumaye jina lake lilikua limechafuka sana...
JK alishinda kwa kuwaalikuwa ametega na hataki kujishughulisha machafu yeyote ili asiaribu jina lake
Tatizo wewe una ajenda zako zingine za ubaguzi ili kupunguza ufisadi
Sumaye alikuwa kachafuka sawa lakini lazima ujue regional politics pia zilimwangusha, Wewe unakataa lakini mimi ninakueleza Ukweli Regional Politics they means a lot in CCM