Peter Noni na Rostam - The EPA Connection

Kila ufisadi wa nchi hii utakisikia jina Chenge
 
Dah! Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi.
 
Kwa wale ambao wamesahau.. tulikotoka na watu ambao hawakutakiwa kupigishwa magoti...
 
Waridi ni harufu rangi zaweza kubadilika kutokana na hali ya hewa na vipindi vya siku
 
Duh! Interesting. Uchambuzi utadhani Maghufuli
 
Kwa kweli tunaelekea pabaya,maana kama walijua wazi wakimgusa Peter wamekusa serikali ndio maana wakaamua kumwacha.ila wajue kuna siku wataumbuka.Tuendelee kuomba mungu bila kuchoka watz
Uliona mbali sana Leo Peter yuko rumande keko
 
Rostam Aziz alisha usoma mchezo mapema kabisa kwamba,baada ya rafiki yake JK kumaliza mda wake wa uongozi atakayekuja kua Rais wa Tanzania hakuwa anajua ni nani! Maana calculations zake zilikua Lowassa,lakini baada ya Lowasa kupigwa chini na Swahiba wake Jk kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu hapo, ndipo palimfanya atambue kwamba mda wa yeye kwenda gerezani ushawadia,ndiyo naama aliachana na nafasi zake zote za uongozi ndani ya CCM.. Maana najua kama Rostam angekua Tanzania,lazima tu kisutu angepata na kujikuta anaenda zake gerezani kama Manji.

Pia akaenda Vodacom, akauza hisa zake zote za Mirambo Holdings,na wakati huu ndiyo mda ambao kina Mwakyembe (Kyela), Marehemu Sitta (Urambo),Anna Kilango,Fred Mpendazoe (Kishapu),Kimario (Vunjo), Lusas Selelii (Nzega) Stella Manyanya walikua na team yao kabisa yakupinga mafisadi... Na ndo kilichosababisha Harrison Mwakyembe kupata maradhi ya wakati ule,maana alipewa sumu na sumu ikaingi kwenye born marrow....

Kundi la mafisadi lililokua linapigwa vita ni Rostam Aziz (Igunga),Edward Lowasa(Monduli) Peter Maganga Noni, Edward Hosea aliyekua Mkurugenzi mkuu wa Takukuru na chain yote ya wizi wa pale EPA, maana michongo yote ya Edward Lowasa na Rostam Aziz ilikua inazimwa na Takukuru,kama mnakumbuka kulikua na uchotaji wa pesa za Kidoga Agriculture Zaidi ya 43B,Hii company ilikua ya Rostam lakin viongozi wa serikalio walikua wanaikingia kifua,kuanzia Mkulu mwenyewe,Zakia Megji aliyekuwa waziri wa fedha,hadi waziri mkuu Pinda alishawahi sema bungeni yuko tayari kusurubiwa lakini hayuko tayari kusemani kampuni ya nani..

Hapa hivi sasa hakuna anayejua Rostam Aziz yuko wapi, anafanya nini,zaidi tu ya Kampuni yake ya Caspian kuwepo hapa Tanzania... Chain ya ufisadi yataka moyo wa dhati kupambana nayo... Unaweza gusa watu ambao ni untouchable na ukajikuta unaishia pabaya tu......
 
And the party is going on ....King maker is again on the wheels of steel [emoji41][emoji41][emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…