I am suprised kuwa Kiranga na OPP and even Mzee Mwanakijiji to some extent bado wanatumaini na mipango ya Mkukuta kuwa tutajenga shule na kuchonga madawati ili watoto wasikalie vitofa!
Labda niulize, kwa kumchunguza kwenu Mtanzania, leo simba na Yanga wakicheza, hata kiingilio kikiwekwa kuwa Shilingi Laki Moja, Uwanja utajaa, watu watachacharika kuitafuta hiyo Laki Moja na kwenda kuangalia mpira.
Leo akishuka Kofi Olomide au Beyonce kufanya onyesho na kiingilio kikawa Shilingi laki Mbili, watu watachacharika na kuzitafut hizo shilingi laki mbili, watabeba zege, kuzoa mavi na mengine mengi alimradi wapate nafasi ya kwenda kuburudika.
Leo hii ukiwaambia tusafishe mitaa na kujenga upya sehemu ili Denzel Washington au Wayne Rooney waje kukaa mwezi mmoja, tutajikusanya kwa dhati kuimarisha nguvu na kufanya kazi kwa bidii na ufanisi wa hali ya juu ili kutoa mandhari mazuri ya kuwa wakarimu!
Jiulizeni inakuwaje ni rahisi kwa watu kuchangia Harusi, Ubatizo, Kipaimara, Jando, Unyago, Mkole lakini inapofika kuchangia kununua madawati, tunakuwa wagumu na wakali kuchangia?
Nikirudi kwenye hoja na kumjibu Mzee Mwanakijiji kwenye swali lake la Walilotuashia Wakoloni, naamini kuwa Tanzania ya sasa tunakwenda kwa mabadiliko. Kama agenda ya mwaka huu kwetu ni change, basi hata michezo ikiisha na tukaachiwa reli, umeme na miundombinu yetu, tutaweza kuamka upya na kuendeleza nchi kwa kutumia miundo mbinu tuliyojijengea ili kufanikisha michezo hii ambayo kwa mipango ya kawaida tumekuwa tukifanya kigugumizi kuifanikisha!