Petroleum Petroleum namba wanaisoma, usichague petroleum

upo nje ya hii field ndo maana anakuja na data za uongo,, petroleum engineering kwa udsm tuu kuna wanafunzi zaid ya watatu ( kati ya 15 darasani ) wanadomeshwa na Swala hiv hii kampuni itawasomesha halafu iwaache?
kama nilivyokuambia mwanzo hiz kozi zipo tatu ( engineering ,chemistry na geology ) kwa upande wa chemistry module zao zinafanana na module za Bsc in chemistry ( tofauti kidgo sana ) hawa wanaweza Fanya kazi popote panapo husisha chemistry related skills, lakin. pia sehemu kama Ewra, Nemc, pura pia wanahitajika.
ni kwel kwa sasa soko la ajira za petroleum hasa engineering ni gumu ila sio kama hiv unavyowadanganya wengine
 
kunywa bia baridi nalipa
 
Kwa hiyo ww unazani wataajiriwa na hizo kampuni au, sasa ni kwambie mwaka 2014, kuna walio someshwa na BG na STATOIL kampuni zenye mtaji wa bilioni za Dolla na sio hivyo viswala lkn walipo rudi bongo holaaaaaaaaaaaa, wapo tu kitaaaa tu
 
Kwa hiyo ww unazani wataajiriwa na hizo kampuni au, sasa ni kwambie mwaka 2014, kuna walio someshwa na BG na STATOIL kampuni zenye mtaji wa bilioni za Dolla na sio hivyo viswala lkn walipo rudi bongo holaaaaaaaaaaaa, wapo tu kitaaaa tu
kwahyo wewe inatakaje ?? course zifutwe au?
 
Si rafiki sana nimerudi diploma nilisoma bachelor ya haya makitu no work at all nimemaliz Diploma juzi nataka nikasome bachelor tena

Pole sana mkuu,usikate tamaa. Bora mlivyopiga kelele humu mtakua mmewasaidia wadogo zetu kutoichagua hio course
 
Positive vibe.

Hata Uganda na nchi zingine za Africa kama Mozambique unaweza kupata ajira.

Tatizo la watanzania ni kutopenda kwenda kutafuta maisha nje.

Pia hii ngoma akiondoka huyu mjomba wa kazi tu inaweza kujibu na kumwaga mpunga wa hatari kama Mbuguni wametoboa chungu cha Tanzanite vile.

Maana wengi watakuwa wameikimbia hao wachache watatoboa mbaya.
 
Yees!!
This is men's talk.
Mimi najishangaa sisi wabongo tuna tatizo gani mimi nikiwemo.

Wakameruni na wanaijeria hadi wanawake wanapambana kwa staili hii uliyosema. Wametapakaa ughaibuni.
 
Usilete utani, huwez amini eti kazi za petroleum zinasumbua dunia nzima, mimi nina marifiki zangu Uganda huko wananitumia email kuniomba kazi hizo hizo na wamesoma petroleum, kazi zinasumbua dunia nzima hadi india, Irani, jamani wengine tuna marafiki huko, kama huamini hebu jiunge mtandao wa LINKEDIN, ili uone jinsi watu wanavyo ng'ang'aniana kazi. Kuna jamaa mmoja yuko Venezuela nchi yenye visima vya mafuta kibao alinitumia sms watsap kuniomba ajira
 
Wewe unaongea tu, mimi nipo kwenye hii field huu ni mwaka wa 10, najua vitu vingi kushinda wewe, from upstream, midstream to downstream, nazijua shughuri zote zinazo fanyika huko, sawa bwana mdogo, hapa petroleum ndio imelala, ni rahisi sana kuyataja hayo makampuni ya Ewura, Nemc, TPDC, lkn nakwambia ni RAHISI NGAMIA KUPENYA KWENYE TUNDU LA SINDANO KULIKO PETROLEUM ENGINEER KUINGIA KWENYE PETROLEUM INDUSTRY
 
sawa boss nimekuelewa,,, nifanyie basi ka mpango ka kuingia huko maana nimuhanga wa hii kitu
 
kwa hiyo madogo wasome nini?
maana ajira siku hizi Ni changamoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…